Wednesday, 31 December 2014

WADAU MAONI YENU KWA AJILI YA KAZI MPYA KATIKA MWAKA MPYA NA MUONEKANO MPYA


HABARI ZENU WADAU WA NISHA'S FILM PRODUCTION KAMPUNI YENU MUIPENDAYO YA MWANA DADA SLMA JABU NISHA INATARAJIA KUINGIA MZIGONI KAMA ILIVYO KAWAIDA YETU HUWA TUNAPENDA KUWAPA NAFASI AU KUCHAGUA KILE KITU AMBACHO MNAKIPENDA KWANI NYIE NDIO WATEJA WA KAZI TUNAZO ZIFANYA. WEWE KAMA MDAU TUNAOMBA UTUTAJIE MSANII GANI WA KIUME UNGEPENDA ACHEZE NAYE KATIKA MOVIE YAKE MPYA AU KITU GANI AONGEZE. MAONI YENU TAFADHALI

SALMA JABU NISHA'S BLOG: MAREHEMU JUMA KILOWOKA (SAJUKI) KUSOMEWA DUA 02/01...

SALMA JABU NISHA'S BLOG: MAREHEMU JUMA KILOWOKA (SAJUKI) KUSOMEWA DUA 02/01...:   02.01.2015 kutakuwa na dua itakayosomwa kwenye kaburi lake kisutu Dar es salaam kuanzia saa nne asubuhi,na badae kutakuwa na dua ny...

MAREHEMU JUMA KILOWOKA (SAJUKI) KUSOMEWA DUA 02/01/2015


02.01.2015 kutakuwa na dua itakayosomwa kwenye kaburi lake kisutu Dar es salaam kuanzia saa nne asubuhi,na badae kutakuwa na dua nyumbani Tabata pamoja na chakula cha mchana kwa watakaojaliwa naomba tuungane pamoja kwenye dua hii, R.I.P Juma Kilowoka Sajuki

Sunday, 28 December 2014

NISHA AJISAFISHA NAFSI KUUANZA MWAKA MPYA SAFI AMA NENEEEEEEEE!!!!!!

Kila binaadam anaijua leo kesho haijui,tumebakisha siku chache inshaallah mwaka uishe,sijui km ntafika au sifiki. Kikubwa leo hii ambayo nimeiona naomba nichukue fursa hii kumuomba msamaha kila ambaye nlimkosea,Iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi,. Sitokuwa mpya mwaka 2015 coz ni yule yule ila ntakuwa na amani ya roho nikiwa safi kwa kila mmoja... amani idumu,nawapenda nyoteee,mashabiki zangu na wasio wangu pia nawapenda.. mm binafsi nimemsamehe kila mtu alonikosea.. NIKISEMA WOTE NAMAANISHA WOTE MNISAMEHE NA TUFUNGUE UKURASA UPYA. Happy new year ingawa haijafika... kesho ntathanx kwa ajili ya#HAKUNAMATATA ambayo itakuwa imetimiza week tangu itoke tukijaaliwa.

Friday, 26 December 2014

HAKUNA MATATA YALITIKISA SOKO LA FILAMU

 HAKUNA MATATA ni filamu inayotoka katika kampuni ya Nisha's film production ambayo imeingia sokoni mwezi huu tarehe 22  ndio filamu inayoongoza kununuliwa sana katika filamu zilizo toka mwezi huu.
 Dogo mmoja kutoka Dodoma akiwa amejipatia nakala zake za HAKUNA MATATA hao ndio mashabiki wakubwa wa msanii SALMA JABU NISHA.
KIJANA OTHMAN THINEY KUTOKA DAR ES SALAAM YEYE NDIO MTEJA WA KWANZA KWANI ALIKWENDA KWENYE MADUKA YA STEPS SAA KUMI NA MBILI NA NUSU ALIONA KUSUBIRIA MACHINGA ATACHELEWA UTAMU WA HAKUNA MATATA

Tuesday, 11 November 2014

Happy Birthday Manager Wa Nisha's Film Production.

Leo ni birthday ya production manager wa Nisha's Film Othmani Thiney Mungu akubariki katika kila jambo

Make Money at : http://bit.ly/best_tips

Nisha Kutwaa Tuzo ya Oscar 2015 !

kwa tetesi zilizotufikia hivi punde,filamu ya mwanadada,mwanaharakati anayejituma sana na asiye na ma-scandal kwenye kiwanda cha filamu Tanzania superstar  SALMA JABU NISHA ambayo tumekuwa tukiiona sana matangazo yake hivi karibuni katika filamu zinazotoka za Steps Entertainment iitwayo HAKUNA MATATA imetabiriwa kuchukua Tuzo za OSCAR na GOLDEN GLOBE AWARDS

Wednesday, 5 November 2014

Sitti Mtemvu Kuvuliwa Taji La Miss Tanzania Muda Wowote Kuanzia Sasa !

Wakati serikali kupita Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ikisema itakifuta cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu,  taarifa zinasema kwamba hawezi tena kuendelea na taji hilo. Imethibitisha kwamba uamuzi umekwisha kufanyika wa kumvua Sitti taji hilo alilovikwa katika mazingira tata, uamuzi unaotarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Photos: Nisha Akishuti Filamu Mpya Na Wasanii Wa Zanzibar House Of Talent.

Star mkubwa wa filamu Tanzania Nisha Salma Jabu hivi juzi kati alikuwa Zanzibar kwa ajili ya kufanya kazi ya filamu na Zanzibar House Of Talent katika kuinua vipaji vipya ukifikiria mwenyewe anatokea visiwani humo. Nisha alisema bado hajaridhika na mafanikio aliyopata kupitia filamu kwani shida yake sio umaarufu bali kuwa mwanamke mwenyewe mafanikio.......

Friday, 31 October 2014

Wema Na Diamond Wamwagana !

Diamond Platnumz na Wema Sepetu wanadaiwa kumwagana kimtindo kwa mujibu wa gossip mpya. wawili hao inasemekana hawapo kwenye mahusiano mazuri na inaelekea wamemwagana

Mashabiki Hupenda Kazi Zetu Na Sio Skendo Zisizo Na Kichwa Wala Miguu: Nisha

Nisha ameandika 

Saturday, 11 October 2014

Sina Uhusiano Wa Kimapenzi Na Msami Kama Inavyozushwa: Irene Uwoya

Star wa filamu mwenye jina kubwa nchini Tanzania Irene Uwoya amesema kuwa hana uhusiano wa kimapenzi naMsami ambaye ni moja wa wakufunzi wa Tanzania House Of Talents(THT) kwa upande wa dancers.

Photos: Nisha, Wastara, Mtunisy, Kabuti, P-Funk Wakiwa Mkoani Dodoma

Juzi wasanii mbalimbali wa filamu na muziki walikuwa mkoani Dodoma wakati wa Rais Kikwete alipokabidhiwab rasmu ya katiba mpya.

Tuesday, 30 September 2014

Rose Ndauka Na Malick Bandawe Wamwagana.

Wachumba wa muda mrefu, star wa sinema za Tanzania, Rose Ndauka na Malick Bandawe ambao maisha yao ya kimapenzi yamekuwa yakitawaliwa na msuguano wa chini kwa chini, hatimaye wameachana Globalpublishers imeripoti

Sipendi Beef Zisozona Kichwa Wala Miguu: Davina

Davina
"Kuna kitu kinanishangaza sana nimechunguza baadhi ya watu wangu wa karibu wana tasnia wenzangu wanacho sana mfano NASEMA MFANO jamani labda nipo karibu na Cathy(Cathy Rupia) halafu Cathy agombane na Maya(Mayasa Mrisho) kwa mambo yao ambayo hayanihusu eti me nikiongea au kukaa karibu na Maya, Cathy akasirike inaingia akilini jamani.

Kazi Zangu Ni Bora Ndiyo Maana Mashabiki Wakanipigia Kura Kupata Tuzo: Nisha

Nisha na Haji Adam(Baba Haji)
Star mkubwa wa filamu nchini Tanzania Salma Jabu Nisha juzi alionyesha furaha kubwa baada ya kupata tuzo ya muigizaji bora wa kike mchekeshaji(best comedienne) katika tuzo za Action And Cut Viewers Choice Awards zilizotolewa Sunrise resort Kigamboni, Dar es salaam.

Wednesday, 24 September 2014

Wanawake Kunyanyaswa Kunanikera Sana: Nisha

Nisha akiwa na watoto yatima kituo cha Vingunguti
"Takribani week 2 au 3 nimesoma wanawake wachache walopigwa na waume zao,wapo waliokatwa viungo,kuchomwa moto n.k,

Sunday, 21 September 2014

Nisha Adaiwa Ni Mfano wa Kuwa Balozi Wa Jamii.

Baada ya filamu zake nyingi kufanya vizuri sokoni na kusapoti jamii isiyojiweza mara kwa mara mashabiki wa muigzaji Nisha Salma Jabu wanataka muigizaji huyo awe balozi wa mambo ya kijamii kupitia kazi zake za sanaa .

Saturday, 13 September 2014

Nisha Ndani Ya Clouds Fm Kuzungumzia Kazi Zake Za Filamu Na Changamoto.

MALKIA WA FILAMU TANZANIA SALMA JABU NISHA JANA AKIHOJIWA KATIKA KIPINDI CHA LEO TENA NDANI YA CLOUDS FM ALIIELEZEA FILAMU YA KIDUME PAMOJA NA CHANGAMOTO ZINAZOMKABILI KATIKA KAZI ZAKE VILEVILE ALIELEZEA UTARATIBU ALIOJIWEKEA KWA KILA MWISHO WA MWEZI KWENDA KUWA TEMBELEA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU NAKUWAPATIA KILE ALICHOJAALIWA.

Tuesday, 9 September 2014

Neema Wa 20% Aja Kivingine Na Filamu Ya Mbwamwitu.

Actress wa Tanzania aliyejaaliwa kipaji cha kuigiza Neema wa 20% anatarajiwa kuonekana katika filamu mpya inayoitwa "Mbwamwitu" katika filamu hiyo Neema kama kawaida yake amesfanya makamuzi ya kufa mtu huku akiwa na wasanii kama Hemedy PHD.
Mbwamwitu ni short film inayosubiriwa kwa hamu.

Saturday, 6 September 2014

Nisha Atoa Misaada Ya Magodoro, Vyandarua Na Mashuka Kwa Yatima.

Muigizaji maarufu wa filamu nchini Salma Jabu Nisha ametoa misaada ya magodoro, mashuka na vyandarua katika kituo cha watoto yatima kilichopo maeneo ya Kigamboni ,

Friday, 5 September 2014

Dokii Amzawadia Lucy Komba Kiwanja Katika Kitchen Party Yake.

Muigizaji maarufu wa filamu nchini Dokii amemzawadia kiwanja star mwenzake wa filamu nchini Lucy Komba katika Kitchen yake iliyofanyika juzi katika ukumbi wa makumbusho ya taifa. Kitchen party ya Lucy Komba ilifunika kwa kutawaliwa na utamaduni wa kitanzania.

Thursday, 21 August 2014

Justin Bieber Kuhusu Kupendwa Hilo Niachie Mimi: Lulu

Star wa filamu Swahiliwood Lulu Elizabeth Michael amesisitiza kuwa yupo serious kuhusu kumpenda Justin Bieber mwanamuziki maarufu wa Marekani. Lulu aliwafungukia pia wale wanaomwambia anaota kwa kusema hajali wayasemayo ila yeye anampenda Bieber kwa dhati kuliko kina Selena Gomez. Kuitia Instagram Lulu aliweka picha ya Bieber leo na kuandika..........

Esha Buheti Alazwa Hospitalini.

Muigizaji wa filamu nchini Esha Buheti amelazwa hospitalini kutokana na kusumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Thursday, 14 August 2014

Jackie Cliff Ahukumiwa Kwenda Jela Miaka 6 Nchini China Baada Ya Kupatikana Na Hati

Jackie Cliff
Baada ya kushikiliwa kwa takriban miezi tisa kwa kesi ya madawa ya kulevya ‘unga’, hatimaye model maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Cliff’ amehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela huku kukiwa na uwezekano wa kupunguziwa adhabu ikawa ndogo zaidi.

Wednesday, 13 August 2014

Nisha Aingia Location Kushuti Filamu Mpya.

Star wa filamu nchini Salma Jabu Nisha kwasasa anashui filamu mpya katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na wasanii wenzake kadhaa akiwemo King Majuto na Hemedy. picha zaidi zitakujia....

Jackline Wolper Shares New Hot Photos.

Actress Jackline Wolper looking dashing wish her new colorful hair. Her choices of outfits always make her stunning............

Thursday, 31 July 2014

Frank Kuja Kufanya Filamu Na Chris Tucker Wa Hollywood Na Rose Ndauka.

Frank
Star mkubwa wa filamu nchini ambaye hana skendo za hovyo hovyo Frank Mohamed Mwikongi amesema kuwa ana ndoto ya kuja kufanya filamu na star wa Hollywood Chris Tucker kwa kuwa anamkubakli sana, na kwa upande wa hapa nchini anataka kufanya kazi na Rose Ndauka kwasababu anaukubali uwezo wake licha ya kuwa tayari wamefanya pamoja filamu ya Waiting Soul lakini yupo mbioni kucheza nae tena filamu mpya.

Actress Faiza Ally Aonyesha Tattoo Yake Mpya.

Actress Faiza Ally mara nyingi hajali maneno ya watu watasema nini yeye hufanya anachopenda na kinachompa furaha in her life. Faiza has new tattoo and aliamua kuiweka wazi, tattoo hiyo ipo eneo la shingoni kwa nyuma kama inavyoonekana pichani.

Friday, 25 July 2014

Lulu Amfungukia Ali Kiba Na Kutoa Makavu Kwa Wanaoendekeza Ushabiki.

Ujio mpya wa Ali Kiba ulikuwa jana usiku alipoachia nyimbo zake mbili mpya ambazo response ya mashabiki ni nzuri. Sasa kupitia Instagram star wa filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu" amefunguka haya.....

Thursday, 24 July 2014

Naitumia Vizuri Fursa Kuwekeza Katika Ardhi Na Ujenzi Na Sio Kushindana Kuvaa Na Kwenda Club: Nisha

Star mkubwa wa filamu Tanzania Salma Jabu Nisha amesema kuwa anaitumia vizuri fursa anayoipata sasa katika kazi zake za sanaa kwa kuwekeza kwa ajili ya maisha yake ya baadae hususani katika ardhi na ujenzi na sio kushindana kuvaa, kwenda club na starehe nyinginezo zisizo na maana kama baadhi ya wasanii wengine halafu baadaye wanaishia kulalamikia maisha wakati wao wanaigiza maisha kwa kuendekeza starehe.

Sina Mpango Wa Kuwa Mwanasiasa kama Baadhi Ya Wasanii Wenzangu: Frank Mohamed Mwikongi

Muigizaji maarufu wa filamu Tanzania Frank Mohamed Mwikongi amesema kuwa hana mpango wa kuingia katika siasa kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii wenzake ambao siku za hivi karibuni wameamua kutumbukia huko. Frank alisema kuwa hana ndoto ya kuwa mwanasiasa ingawa anaweza kuwa mfuasi wa chama chochote kile cha siasa.

Wednesday, 16 July 2014

Odama Amuanika Mwanae Miezi Kadhaa Baada Ya Kujifungua.

Baada ya watu na mashabiki wa star wa filamu nchini Odama Jennifer Kyaka kusubiri kwa hamu kubwa kumuona mtoto wa star huyo aliyejifungua hivi karibuni bila mafanikio. Hatimaye star huyo kupitia Instagram leo hii amemuweka wazi mwanae huyo alijifungua takribani miezi miwili na nusu iliyopita.

Sexy Kajala Masanja Covers Vibe Magazine New Issue

Sexy.....sexy.... Kajala on the Vibe magazine Tz for the July issue. Her styling was on point and the photographer did a great job..

Photos: Kajala Amfanyia Mwanae Party Ya Nguvu Na Kusaidia Walemavu.

Odama, Chuchu na Kajala
Star wa filamu nchini Kajala Masanja juzi alimfanyia mwanae Paula birthday party ya nguvu huku akiwasaidia watoto wenye ulemavu wa akili vitu mbalimbali. jionee picha............

Saturday, 5 July 2014

King Majuto, Sabby Angel, Tino, Dude And Leo Shoot New Film In Kenya.

Sabby Angel
Tanzanian Swahiliwood actors Sabby Angel, King Majuto, Tino Hisan Muya and Dude Kulwa Kikumba are shooting new film with Kenyan actors including Leo. The film is being shot in Mombasa, Kenya, it is called  Riziki. Sabby Angel is the producer of the film while the director is Tanzania's Timoth Conrad with close assistance by well-known Kenyan film maker and director Hassan Feisal Mufti of Coastal Films. Look some photos of behind the scenes...........

Jokate Akana Kuvunja Ndoa Ya Dida Na Ezden.

Model, actress na designer maarufu nchini Jokate Mwegelo amepangua madai ya kuwa inawezekana anahusikia na kuvunjika kwa ndoa ya Dida na Ezden. Jokate na Ezden wapo karibu wakiwa watangazaji wa kipindi cha The One Show kupitia TV1, hata hivyo akizungumza na GPL Jokate aliwawakia watu wanaopenda kuungaunga mambo kwa kusema

Sipendi Kufanya Mambo Ya Ajabu Yatakayopelekea Kunichafua: Nisha

Nisha
Star wa filamu ya Zena Na Betina, Salma Jabu Nisha amesema kuwa katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan hapendi kabisa kufanya mambo yasiyompendeza Mungu bali anafanya yote yaliyo mema. Nisha amesema kuwa katika maisha yake ya kila siku pia huwa hapendi kunywa vileo wala kwenda Club sana. Nisha  amesema kuwa hafikirii kutengeneza skendo kama baadhi ya wasanii wenzake ili tu wazidi kuwa maarufu kwa madai ni kujichafua na kujishushia heshima mbele ya jamii.

Thursday, 12 June 2014

Zena Na Betina Yaingia Sokoni Kwa Kishindo Kikubwa.

Filamu ya Zena Na Betina imeingia kwa kishindo sokoni leo hii, Hakikisha unanunua nakala yako halisi

Wednesday, 11 June 2014

Zena Na Betina Kuwasha Kivumbi Sokoni Kesho Tarehe 12 June.

Nisha
Filamu ya ZENA NA BETINA ambayo imekuwa masikioni mwa watu kwa muda sasa kutokana na kupata promo ya kutosha kutoka kwenye media zikiwemo tv, magazeti, blogs na mitandao mingine ya kijamii inatarajiwa kuingia sokoni kesho tarehe 12 June kwa kishindo kikubwa. Filamu hiyo imetengenezwa na Nisha's Film Production huku wasanii wenye majina kama vile Salma Jabu Nisha, Manaiki Sanga, Hanifer Daudi "Jennifer wa Kanumba", Farida Sabu, Senga, Happy Nyatawe na Lumolwe Matovolwa akionyesha uwezo wao kisanaa. Usikose kununua nakala yako halisi

Sunday, 8 June 2014

Filamu Ya ZENA NA BETINA Kutikisa Soko La Filamu Nchini !

Zimebaki siku chache kwa filamu ya ZENA NA BETINA kuingia sokoni huku ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa filamu za kitanzania. Filamu hiyo itaingia sokoni tarehe 12 mwezi huu wa June. Mastaa ndani ya movie hiyo ni Nisha, Manaiki Sanga, Jennifer wa Kanumba, Senga, Farida Sabu na wengineo. usikose kununua nakala yako halisi.

Shamsa Ford Afunguka Kufuatia Picha Chafu Zinazodaiwa Kuwa Zake Akiwa Na Mbunge Kusambaa.

Shamsa Ford
Picha chafu zinazodaiwa kuwa za star wa filamu nchini Shamsa Ford na mbunge wa Chadema, Salvatory Machemli zimeanza kusambaa kwa kasi mitandaoni tangu jana,. Picha hizo zinawaonyesha wawili hao wakiwa kitandani kwenye mahaba mazito. Hata hivyo picha hizo zinatia shaka kuwa sio halisi ni za kutengenezwa ingawa hatuna uhakika kwa asilimia zote kwasababu msichana anayedaiwa kuwa Shamsa Ford ana umbo tofauti na la star huyo, Shamsa ana umbo la kawaida ki-shape lakini msichana huyo anaonekana kuwa na umbo namba nane.

Wema Sepetu, Diamond Na Aunty Ezekiel Katika Red Carpet MTV Africa Music Awards 2014

Wema na Diamond
Jana ilikuwa kilele cha tuzo za MTV Africa Music Awards ambapo Diamond Platnumz alikuwa amependekezwa katika vipengele viwili na kukosa kuibuka mshindi. Katika red carpet mastaa wa Tanzania akiwemo Diamond mwenyewe, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel walikuwepo kutuwakilisha Tanzania angalia picha zilivyokuwa na unadhani nani alipendeza zaidi?

Thursday, 5 June 2014

Nisha Ndani Ya TBC1 Katika Interview Kuhusu Zena Na Betina.

Nisha
Star wa filamu nchini Salma Jabu Nisha leo atakuwa na interview na kituo cha tv cha TBC1 kwa ajili ya kuizungumzia filamu yake mpya ya ZENA NA BETINA ambayo tayari inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa filamu za kitanzania. Interview hiyo itarushwa hewani Jumamosi hii. Zena Na Betina inaingia sokoni tarehe 12 June huku mastaa wengine wakiwa ni Khanifa Daudi "Jennifer wa Kanumba", Farida Sabu, Manaiki Sanga, Happy Nyatawe, Senga na Lumolwe Matovolwa

Monday, 2 June 2014

ZENA NA BETINA Yasubiriwa Kwa Hamu Kubwa.

Filamu ya ZENA NA BETINA ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa filamu za kitanzania inatarajiwa kuingia sokoni kwa kishindo tarehe 12 June. Hakikisha unanunua nakala yako halisi

Wednesday, 28 May 2014

ZENA NA BETINA Kutoka Tarehe 12 June Na Sio Tarehe 29 May.

Nisha
"Habari mashabiki zangu,nyumbani kwetu akifa baba au dada au mwanafamilia yyte,basi km kuna aliyetaka kuolewa harusi inaghairishwa,maisha yangu ni filamu,na filamu ni nyumba yangu ya pili,sisi km NISHA'S FILM PRODUCTION NA STEPS INTERTAINMENT tumeamua kughairisha kuitoa filamu yetu mlokuwa mkiisubiri kwa hamu "ZENA NA BETINA" ilikuwa itoke tar.29/05/2014 sasa basi tutaisogeza mbele hadi tar.12/06/14 kwa ajili ya kuomboleza misiba hii,samahani kwa usumbufu uliojitokeza,munisamehe sana,tumeguswa sana,kwangu mm km Nisha kutoa filamu ni furaha,siwezi kufurahi siku tunayomzika msanii mwenzetu kipenzi RACHEL yaani kesho ambayo ndio ilikuwa siku ya kutoka ZENA NA BETINA ,nina imani kubwa kama ingekuwa mimi  filamu isingetoka kesho na hii ni zawadi yenu Rachel na Adam kuambiana kutoka NISHA'S FILM PRODUCTION. .. naomba mnisamehe sana mashabiki wangu, ila nimetazama UTU KWANZA halafu pesa baadae. wanaoendelea kufanya promo wafanye na naomba mnisaidie kusambaza ujumbe huu. . Nawapenda sana. ZENA NA BETINA itatoka tar.12/06/2014 Inshaallah siyo tar.29 tena. Cc @nishasfilmproduction" ameandika Nisha kupitia mtandao mmoja wa kijamii

Muigizaji Sabby Angel Ajichia Kwa Mapozi Sexy, Jionee Mwenyewe.


Muigizaji wa filamu nchini Salma Tamim maarufu kama Sabby Angel ametoa picha mpya akiwa katika mapozi ya ukweli na kuonyesha miguu yake ya bia.

Irene Uwoya Atoka Kimapenzi Na Dancer Wa THT.

Uwoya na Msami
Habari mpya ni kuwa star wa filamu nchini Irene Uwoya yupo kwenye penzi zito na mwalimu wa kucheza toka Tanzania House Of Talent(THT) anayeitwa Msami. Kwa mujibu wa mpenzi wa Msami anayeitwa Rehema akihojiwa katika U Heard na Soudy Brown alisema kuwa Uwoya ndiye aliyemtongoza Msami licha ya kufahamu kuwa tayari ana mpenzi mwingine(yeye Rehema). Rehema amesema kuwa Uwoya licha ya kumtongoza Msami pia anamhonga sana pesa ndiyo maana Msami akajawa na tamaa na kumkubali kwakuwa bado yeye ana-hustle kimaisha. Rehema alisema "ni tamaa tu za vijana, si unajua tena ukiwa bado hujatoka, wanashawishika na tamaa ya hela ili apate kutoka na ajulikane

Tuesday, 20 May 2014

Nisha Atinga Ofisi Za Sani Kisa Filamu Ya Zena Na Betina.

Nisha
Habari ni kuwa star wa filamu nchini Salma Jabu Nisha juzi Jumatano ya wiki iliyopita aliitwa kwenye ofisi za gazeti la Sani kuhusu issue ya Filamu ya ZENA NA BETINA ambayo imepangwa kuingia sokoni tarehe 29 mwezi huu. Sani walimuita Nisha baada ya jina la filamu yake hiyo kufanana na majina ya katuni za Zena na Betina zinazochorwa kwenye gazeti hilo kwa muda mrefu sasa. Hata hivyo mtoa habari amesema kuwa licha ya gazeti hilo kumtishia kumburuza kotini Nisha au kumtaka atoe fidia ya mil.100 lakini mazungumzo yao yanaelekea vizuri kwa hiyo filamu hiyo itaingia sokoni tarehe 29 kama ilivyopangwa kwasababu story ya filamu ya ZENA NA BETINA ni tofauti kabisa na ya katuni hizo. Story ya filamu ya ZENA NA BETINA inadaiwa kuwa nzuri sana kiasi cha wapenzi wa filamu za kitanzania kuwaisubiria kwa hamu kubwa kuinunua.