Friday, 31 January 2014

BEHIND THE SCENES: AMANDA POSHY NDANI YA FILAMU YA JANI CHANGA.

Muigizaji wa filamu maarufu nchini Amanda Poshy ataonekana katika filamu mpya ya Jani Changa ambayo alikuwa anashuti mwezi January mwaka huu(2014). Angalia behind the scenes ya filamu hiyo ambayo imehusisha mazingira ya kijijini pia.



Thursday, 30 January 2014

SHILOLE APATA MCHUMBA WA KIZUNGU.

Shilole ambaye ni star wa filamu na muziki nchini Tanzania amenasa kwenye penzi la jamaa wa kizungu raia wa Uingereza anayejulikana kwa jina la Ankar. Jamaa huyo kwa mara ya kwanza alidatishwa na shilole katika show aliyoifanya nchini Uingereza. Chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers kilisema "Ukweli ni kwamba Shilole ana mchumba wa Kizungu na walikutana kwenye shoo ya mara ya kwanza aliyoenda kufanya nchini Uingereza na hivi karibuni ataenda tena na amealikwa na huyo mchumba wake"

Naye Shilole alipoulizwa na mtandao huo alisema " Kweli nina mchumba Mzungu ambaye ni raia wa Uingereza, nilipokuwa napataka nimefika, sipindui tena. Unajua muziki wangu na mauno yangu yanawavutia sana watu, siku ya kwanza aliniona kwenye shoo akanipenda ndipo tukaanzisha urafiki, Hivi karibuni nina safari ya kwenda nchini humo kwa mwaliko maalum alionipa, nitaenda peke yangu kwani safari nyingine zote zilizopita nilikuwa naenda na watu,” alisema Shilole"

                             Shilole na mpenzi wake huyo

MAMA WEMA AINGIA MTAANI KUWASAKA DIAMOND NA WEMA SEPETU ILI AWAPE KIBANO.

Mama wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, Mariam Sepetu anadaiwa kuingia rasmi mitaani akiwasaka wapenzi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Wema.

Wema na Diamond wakiwa katika pozi la kimahaba.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers, mama Wema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kusikia taarifa kutoka kwa watu kwamba, Diamond amekuwa akisambaza maneno mitaani kuwa haogopi vitisho vya mwanamke huyo kufuatia hatua yake ya kumrudia binti yake.

ILIKUWAJE KWANI?

Hivi karibuni, mama Wema alisema kitendo cha Diamond kumrudia bintiye hakubaliani nacho.
Aliongeza kuwa, kufuatia hatua hiyo iko siku ataingia mtaani kumsaka Diamond na popote pale atakapomnasa, atamkata na panga.

Mama Wema, Mariam Sepetu anayewasaka wapenzi hao.
TURUDI KWA CHANZO
“Jamani si mnakumbuka juzikati mama Wema alisema atamsaka Diamond? Sasa amesikia Diamond anatangaza mitaani kwamba, hatishiki na tamko la mama mkwe wake huyo na watakapokutana watajua nani zaidi.
“Hivi ninavyosema, mama Wema ameingia mtaani kuwasaka. Lengo lake awakute wote wawili ili awaanzishie timbwili la kufa mtu.
“Tangu Ijumaa iliyopita, kila siku anatoka kwenda mitaani kuwasaka, naamini siku akiwakuta pamoja kweli itakuwa vita kubwa,” kilisema chanzohicho.

Gari la Wema na la Diamond yakiwa yameegeshwa nyumbani kwa Wema.
KWA NINI ASIENDE NYUMBANI?

Chanzo kilipoulizwa kama kweli mama Wema amepania kuwanasa wawili hao, kwa nini asiwafuate nyumbani kwa binti yake, Kijitonyama, Dar ambako wanapika na kupakua, kilijibu:
“Ameweka mtego wake pale, bahati mbaya sana Diamond naye anaishi kwa machale. Kuna siku anakwenda kulala kuna siku haendi. Huenda na yeye (Diamond) ameweka watu wake ndani kwa Wema wa kumpelelezea kama mama Wema atakwenda au ana dalili za kwenda.”
Chanzo kikaendelea: “Siku hizi Diamond anaweza kwenda kwa Wema, akaacha gari lake na kutoka na la Wema na kurudi kwake usiku sana.”

Mama Wema alipotafutwa na kutumiwa ujumbe wa simu alijibu kwa kusema ....
: Nipo msibani tuma sms. Pia akatuma sms kwenye simu yake nyingine akisema: Nipo msibani, ulikuwa unasemaje?
Alipotumiwa madai yote kuhusu yeye kuanza kuwatafuta Wema na Diamond, pia likamjulisha kwamba kama anawatafuta kweli, muda huo, wawili hao walikuwa wapo chumbani kwa Wema hawajaamka.
Hata hivyo, mama Wema hakujibu meseji yoyote kati ya hizo mbili hali iliyotafsiriwa kuwa, uchungu wa msiba ulimuondolea uwezo wa mawasiliano.

NYUMBANI KWA DIAMOND

Mapaparazi walitia timu nyumbani kwa Diamond, Sinza-Mori na kukutana na mtu mmoja aliyedai ni mjomba wa staa huyo ambaye alidai Diamond Platnumz alitoka asubuhi na mama yake, Sanura Kassim kwenda Tegeta, Dar.

NYUMBANI KWA WEMA
Baada ya kutoka nyumbani kwa Diamond huku wakiamini Mbongo Fleva huyo kaenda Tegeta kama alivyosema mjomba mtu, mapaparazi walikwenda nyumbani kwa Wema.
Baada ya kugonga geti kwa dakika moja, alitokea mlinzi na mambo yalikuwa kama ifuatavyo;

Paparazi: Mambo?
Mlinzi: Poa, karibu.
Paparazi: Asante, nina shida na Wema, sijui nimemkuta?
Mlinzi: Wamelala, hawawezi kuamka muda huu.
Paparazi: Wamelala? Nani na nani?
Mlinzi: Madam (Wema) na Diamond.
Diamond.
Paparazi: Ina maana Diamond yumo ndani?
Mlinzi: Si nimekwambia wamelala?
Paparazi alifanikiwa kupenyeza macho kwenye nafasi ya uzio na kuyaona magari ya wote wawili, la Diamond aina ya Toyota Land Cruiser V8 na la Wema, Toyota Lexus Harrier.

KAJALA AJIACHIA NA BIKINI.

Muigizaji wa filamu Swahiliwood Kajala Masanja amejimwaga katika vazi la bikini a.k. swimsuit kama anavyoonekana pichani chini


Monday, 27 January 2014

WEMA SEPETU ASALITIWA NA RAFIKI YAKE WA KARIBU KWA KUMCHUKUA KIGOGO WA IKULU.

Wema Sepetu
Baada ya kuachana na Wema Sepetu huku akimnyang’anya vitu vyote vya ofisini, yule kigogo wa ikulu, Clement a.k.a CK, hivi sasa anadaiwa kutoka na shosti wa staa huyo, Naima Shaa.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers, Naima anatamba na kuwapiga vijembe wasichana wa mjini kuwa anatoka na CK mwenye mkwanja mrefu (bado fedha hazijaisha).
“Nakwambia hatunywi maji, mtoto kadata kabisa hadi ameamua kujichora ‘tatuu’ ya jina la Clement  kwenye bega lake la kulia. Inahusu?” kilihoji chanzo hicho

NI MTOTO WA MBUNGE
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Naima ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM) hivi sasa anaonekana na mdogo wa CK huku wakiitana shemeji wa ukweli.
“Sasa hivi jamaa anajilia vyake mdogomdogo kwa mtoto Naima pale kati, naona ameamua kumalizia machungu ya Wema kwa Naima.
“Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki.
“Unajua kama mtu akikuumiza kimapenzi, ukitembea na rafiki yake naye anaumia vibaya mno. Kwani hukumbuki ilivyokuwa kwa Penny (Penniel Mungilwa) alipochukuliwa na Diamond (Nasibu Abdul)? Ilikuwa ni ili kumuumiza Wema na kweli walifanikiwa. Ndicho anachokifanya CK,” kilitiririka chanzo hicho.

Naima Shaa
WATU WAMEDATA
Chanzo hicho kiliweka wazi kuwa Naima ambaye mara nyingi haoni soni kuonesha tatuu ya jina la Clement, amekuwa akijinadi kuwa yeye ndiye mrithi halali wa Wema na kwa sasa kigogo huyo haoni wala hasikii kwake.
 
Tatoo ya Clement mgongoni mwa Naima.
“Naima naye amedata kabisa na sidhani kama anaogopa Wema kujua kama yeye ndiye hasa anatembea na kigogo huyo kwa kipindi hiki,” kilisema chanzo hicho.

UNATAKA KUMSIKIA NAIMA?
  Naima alitafutwa ili kuthibitisha madai hayo ambapo alikiri kumfahamu CK lakini akadai watu wanamsingizia.
Alipoulizwa kuhusu  tatuu aliyochora yenye jina la Clement, Naima alisema ameandika ‘Element’ na siyo ‘Clement’ (tazama picha, akili ya kuambiwa changanya na yako).
“Yeleuuuwi...jamani watu wananisingizia. Hii tatuu niliyochora nimeandika jina Element na siyo Clement (angalia maneno yanafafa! Moja alikuwa anamaanisha Clement),” alisema Naima na kukata simu.

WEMA ANAJUA CHOCHOTE?

  Wema Sepetu alipoulizwa kuhusiana na madai ya zilipendwa wake kulipiza kisasi kwa rafiki yake, Naima, alisema kuwa habari hizo ameshazisikia lakini anasikitika kwa kuwa kigogo huyo karuka majivu na kwenda kukanyaga moto.
Alisema kuwa ishu hiyo haimuumizi na zaidi sana anawaombea wawili hao maisha mema ya kimapenzi ilimradi moyo wake umeshatua kwa umpendaye.
“Moyo wangu ulishatulia kwa nimpendaye, nawatakia maisha mema,” alisema Wema.

PETER PHINIAS KUCHEZA FILAMU YA MAISHA HALISI YA KANUMBA !

Peter Phinias
Hivi karibuni mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba alisema kuwa ana lengo la kutengeneza filamu itakayohusu maisha halisi ya mwanae marehemu Steven Kanumba ambaye alikuwa star mkubwa wa filamu nchini aliyekuwa tayari ameanza kukubalika katika nchi kadhaa za kiafrika ikiwemo Nigeria kwa juhudi zake alizozifanya kupitia filamu na kufanikiwa kuanza kuitangaza Tanzania vizuri. mama Kanumba ambaye jina lake halisi ni Flora Mtegoa alisema kuwa atafanya usaili wa kutafuta muigizaji wa kiume anayefanana na Kanumba ili acheze nafasi ya maisha ya Kanumba, na hataangalia umaarufu wa mtu bali kipaji na kufanana na Kanumba.

Steven Kanumba

Kama hiyo ikitokea basi Peter Phinias ambaye ni muigizaji chipukizi nchini anayedaiwa kufanana na Kanumba anaweza kupata nafasi ya kuigiza filamu hiyo, Peter Phinias tayari ameigiza kwenye filamu ya Mahaba Niue akiwa na Jackline Wolper na Simon Mwapagata(Rado) na Mistake Vision akiwa na Deogratiaus Shija. Ukiachilia mbali Phinias muigizaji mwingine wa filamu anayedaiwa kufanana na Kanumba ni Philimon Lutwaza ambaye tayari ameshaigiza filamu kadhaa na mastaa wengi nchini ikiwemo After Death amabyo ilikuwa maalum kwa ajili ya kumuenzi marehemu Kanumba.

Wiki mbili zilizopita baadhi ya mitandao kadhaa nchini na hata page ya East Africa Television iliweka picha ya Peter Phinias kuwa anafanana na Kanumba na kuwataka watu wampe asilimia za ufanano wake na Kanumba. Je wewe unadhani Peter anafanana na marehemu Kanumba kwa asilimia ngapi?

A. 100%

B. 85%

C. 70%

D. 50%

E. 0%
                                                              Peter Phinias

Thursday, 23 January 2014

LULU NA STEVE NYERERE KUONEKANA THE MBONI SHOW LEO ALHAMISI.

 Msanii wa Maigizo Tanzania Steve Mongere aka Steve Nyerere akisalimiana na Mwendesha Kipindi cha The Mboni Show , Mboni Masimba (Wa Kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili ndani ya mjengo ambapo kipindi hiko hurekodiwa Pembeni ni Msanii nguli wa Filamu Tanzania Elizabeth Michael "Lulu" akifuatiwa na Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ni watengenezaji, wauzaji na wasambazaji wa Filamu za Kitanzania Nchini.

Msanii Nguli na mahiri aliye chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited Elizabeth Michael "Lulu" akisikiliza kwa makini wakati msanii mwenzie Steve Nyerere alipokuwa akiongea katika kipindi cha The Mboni Show
 Mwendeshaji wa Kipindi cha The Mboni Show Mboni Masimba (Wa Kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Muigiza Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu aliye chini ya kampuni ya Proin Promotions Limited mara baada ya kipindi kumalizika
 Meneja masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Limited Evance Steven akiwa tayari kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na Mwendesha Kipindi Cha The Mboni Show, Mboni Masimba wakati wa kurekodi kipindi hiko kitakachorushwa leo Alhamisi
 Muigiza wa filamu za vichekesho Steve Mogere "Nyerere" akieleza mikakati yake na filamu zake mpya alizotoa akiwa chini ya Kampuni ya Utengenezaji, Usambazaji na Uuzaji wa Filamu za Kitanzania ya Proin Promotions Limited wakati wa kipindi cha the Mboni Show kitakachorushwa hewani leo
 Mboni Masimba, mwendeshaji wa Kipindi cha the Mboni Show akimsikiliza Steve Nyerere kwa umakini wakati msanii huyo wa vichekesho alipokuwa akielezea Mikakati yake katika Mwaka huu na juu ya filamu zake alizozitoa akiwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions Limited 
 Mwendeshaji wa kipindi cha the Mboni Show, Mboni Masimba (wa kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni aliowaalika katika kipindi chake cha The Mboni Show kitakachorushwa leo usiku. Kutoka Kulia Ni Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited Evance Stephen, Msanii Nguli na Mahiri Elizabeth Michael aka Lulu na Steve Mongere aka Steve Nyerere.

JOHARI ADAIWA KUWA MGONJWA NA KULAZWA HOSPITALINI.

Muigizaji maarufu wa filamu nchini Blandina Chagula(Johari) anadaiwa kuwa amelazwa katika hospitali moja jijini Dar es salaam kutokana na kuumwa ingawa bado haijajulikana nini kinamsumbua star huyo mkongwe wa filamu Swahiliwood. kwa mujibu wa mtandao mmoja ndugu mmoja wa Johari alisema kuwa Johari anaumwa sana na amelazwa hospitali moja jijini Dar es salaam lakini alikataa kuitaja hospitali hiyo kwa kuhofia waandishi wa habari akidai watamsumbua star huyo "kwa kweli Johari anaumwa sana na tunaomba dua zenu tu" alisema ndugu huyo.

 Ugua pole Johari


LULU APATA MCHUMBA, KUOLEWA MUDA SI MREFU !

Elizabeth Michael(Lulu) ambaye ni star mkubwa wa filamu Swahiliwood anadaiwa kuwa na mchumba ambaye anajulikana kwao tayari. Mchumba wa Lulu anadaiwa kuwa kigogo mwenye pesa zake na pia mmiliki wa kampuni moja kubwa ya usambazaji wa filamu na anajulikana kwa jina la Johnson au Jr. Chanzo kimoja kikizungumza na Globalpublishers kilisema .......



"Kwa taarifa yenu, tayari JR anafahamika vizuri kwa akina Lulu kwani alishakwenda kujitambulisha na kuna maneno kwamba ndiye aliyempangia nyumba kubwa, Tegeta jijini Dar. Unajua yule jamaa aliona fursa akaitumia baada ya Lulu kutoka mahabusu kwa matatizo ya kifo cha mwandani wake, Steven Kanumba ndipo JR akafanya juu chini hadi akafanikiwa"

Chanzo hicho kiliendelea kwa kusema "Muda si mrefu zitasikika cherekochereko za Lulu kuolewa. ukweli nin kwamba hata mama Lulu(Lucresia Karugila) amemkubali yule mchumba kwani ndiye anayemfanya Lulu aonekane kama alivyo sasa, sasa hivi Lulu anaishi kwenye bonge la nyumba kule Tegeta(Dar es salaam) na suala la usafiri si ishu, Anabadili tu magari, kusema kweli kwa sasa bidada mambo yamemwendea vizuri, Anachoogopa tu yasitokee kama yale ya Clement wa Wema Sepetu"

Naye mama Lulu alipoulizwa na mtandao huo kuhusu issue hiyo alisema kuwa yeye hana kipingamizi kwakuwa hayo ni maelewano ya Lulu na mchumba wake na anamkubali mchumba huyo na alipoulizwa kuwa mwanaume huyo ni kigogo mwenye fedha zake alisema "mimi sina sababu ya kumkataa mwanaume ambaye wamekubaliana na mwanangu, kikubwa ni makubaliano, namkubali"

Lulu alipotafutwa mazungumzo yake na mtandao huo kupitia gazeti lake la Amani yalikuwa hivi.........

Amani: Mambo vipi Lulu?
Lulu: Poa, naongea na nani?
Amani: (akatajiwa jina la mwandishi) kwanza hongera kwa kupata mchumba.
Lulu: Nani kawaambia?
Amani: Kwa kazi yetu hii hatushindwi kujua. Je, ni kweli umepata mchumba?
Lulu: Ndiyo lakini nisingependa sana kulizungumzia hilo.
Amani: Anaitwa nani?
Lulu: Siwezi kumtaja leo (Jumanne iliyopita). Nitawatajia tu ninyi subirini. Itakuwa surprise (mshangao), siku si nyingi nitamuanika.
Amani: Je, ni kweli ni maarufu kwa jina la JR? Au wewe tutajie hata jina la mwanzo tu.
Lulu: Nimeshasema jamani nitawatajia kwani ninyi mna haraka gani?
Amani: Je, ni kweli ni mmiliki wa kampuni ya burudani? (anatajiwa kampuni).
Lulu: Hayo yote yatafahamika kwenye utambulisho. Naomba niishie hapo ‘coz’ sina cha zaidi kuhusu ishu hiyo jamani subirini siku si nyingi.


Naye Flora Mtegoa ambaye ni mama wa Kanumba alipogusiwa kuhusu Lulu kupata mchumba alionyesha kuchekelea na kusema hana tatizo kabisa kwani Lulu tayari ni mtu mzima.
"Mimi sina tatizo kabisa, namjua. Lulu anaweza kuolewa na nimempa baraka zote" alisema mama Kanumba ambaye kwa sasa ni shosti mkubwa wa mama Lulu.

Kwa upande  wa JR alipotafutwa na mtandao huo ilikuwa hivi..

Amani: Habari yako mkuu JR?
JR: Safi, nikusaidie nini?
Amani: Mimi…(akatajiwa jina la mwandishi na kampuni) wewe ndiye JR mmiliki wa kampuni ya…(anatajiwa jina la kampuni).
JR: Kwanza mimi siyo JR ni GR. Huyo JR ni mdogo wangu.
Amani: Mbona sisi tumetajiwa JR ambaye anamiliki kampuni ya...(anatajiwa tena jina la kampuni).
JR: Oke, ndiyo mimi nikusaidie nini?
Amani: Taarifa tulizonazo ni kwamba una uhusiano na Lulu? Yaani wewe ndiye mchumba wake?
JR: Ndiyo, sitaki maswali (tusi na kukata simu).
Tangu kitokee kifo cha Kanumba ambaye alikuwa na uhusiano wa siri na Lulu, bidada huyo hajawahi kuwa na mwanaume hadi huyo mchumba aliyejitokeza.

                                                  Lulu

Monday, 20 January 2014

DIAMOND ANAMROGA MWANANGU ILI AHARIBIKIWE KIMAISHA: MAMA WEMA SEPETU

Sijui ni hasira au nini! Mama mzazi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Mariam Sepetu ‘Mama Wema’ amemshika uchawi mpenzi wa bintiye, Diamond Platinumz huku akilaani vikali kitendo cha kumrudia mwanaye akidai lengo lake ni kumharibia maisha, Globalpublishers  kupitia gazeti lake la Ijumaa Wikienda limeweka kila kitu kweupe.

Wema na Diamond.
Mama Wema alitoa hisia zake hizo juzi jijini Dar es Salaam alipoongea kwa simu na paparazi wetu huku maneno yake yakiwekwa kwenye kumbukumbu ya kinasa sauti cha Global Publishers.


ALIANZAJE?
Mwanamke huyo mwenye msimamo uliopitiliza kuhusu bintiye Wema, aliwasiliana na paparazi wetu akisema siku hiyo anataka kutoa dukuduku lake kuhusu Diamond ambaye pia ni staa wa Bongo Fleva.
Mama Wema alisema taarifa alizonazo kuhusu staa huyo ni kwamba, juzikati alikwenda kwa mganga f’lani na kuzika  kondoo watatu ili Wema aharibikiwe maisha.
Mama mzazi wa Wema Sepetu, Mariam Sepetu.
“Mimi nimekerwa sana na huyo Diamond wenu. Najua hajamrudia Wema kwa mapenzi, amemrudia ili apate nafasi ya kumharibia maisha. Ni kijana hatari sana.
“Nina taarifa kutoka kwa watu wa karibu naye kwamba alikwenda kwa mganga akazika kondoo watatu ili mwanangu aharibikiwe.
“Simpendi na sitaki hata kumwona. Hana nia nzuri na mwanangu, najua. Kwanza mama Diamond (Sanura Kasim) hampendi Wema, anampenda Penny, nampongeza sana kwa uamuzi huo,” alisema mwanamke huyo.

AMSHANGAA DIAMOND KULALIA KITANDA CHA KIGOGO WA IKULU
Mama Wema ambaye anasifika kwa ubabe, alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa amesikia Diamond sasa analala na kula kwa Wema. Akatolea tamko kitendo hicho.
“Kama angekuwa mwanaume kweli ana pesa zake angekubali vipi kulala kwenye kitanda alichonunua mwanaume mwenzake (Clement)?

Wema.
“Hiyo ni akili kweli? Vitu anunue mwanaume mwenzako halafu wewe uje kutumia bila haya. Halafu nimesoma kwenye gazeti moja (Amani) eti atamnunulia Wema vitu vyote alivyonyang’anywa na Clement, mimi nasema hawezi kumnunulia kamwe, anamdanganya tu,” alisema mama Wema.

ANACHOTAMANI
Mama Wema hakuacha kutoa donge lililokaa juu ya moyo wake, alisema:
“Nimeshamaliza arobaini ya mume wangu (Mzee Isaac Sepetu). Natamani siku moja nimfuate Diamond popote alipo nikamtandike makofi mpaka ashike adabu yake mwana…(tusi).”

AMPA TAHADHARI YA KUMKATA NA PANGA
Paparazi wetu alimpomuuliza mama Wema kama yupo tayari kumkaribisha Diamond nyumbani kwake ili wayaongee na kuwekana sawa na abariki uhusiano wao wa kimapenzi, alikuja juu.
“Aje wapi? Aje aongee na nani? Asije akajaribu kuja nyumbani kwangu, haki ya Mungu tena nitamkata na panga, hivi yule…(tusi) ananijua hanijui?”

ASEMA HAKUNA MZAZI YEYOTE ANAYEKUBALI UHUSIANO WA DIAMOND NA MTOTO WAKE WA KIKE

Mama huyo alizidi kuweka wazi kuwa hakuna mzazi yeyote Tanzania mwenye uchungu na mwanaye anayeweza kuruhusu uhusiano wa Diamond na mtoto wake wa kike.
“Nataka kukwambia kwamba hakuna mzazi yeyote hapa Tanzania anayeweza kukubali ujinga anaoufanya Diamond kwa mwanaye wa kike. Ni mtu gani ambaye hapendi kabisa kuwa mtulivu zaidi ya kuwachafua wasichana? Mimi naumizwa sana na yeye,” alisema mama huyo huku akisisitiza maneno yake yaandikwe gazetini.

Diamond.
WEMA YAKIMSHINDA ARUDI NYUMBANI
Bi. Mariam alizidi kutoa ya moyoni mwake na kusema kuwa inawezekana Diamond anafanya hivyo akijua kuwa  Wema hana pa kwenda akishamuacha mweupe baada ya kumharibia uhusiano wake na Clement.
“Najua Diamond anaamini akishamchezea Wema na kumwacha atakuwa akitangatanga, lakini akumbuke ana kwao na hakuna shida yoyote, Wema atarudi nyumbani hapa na kuendelea na maisha yake kama kawaida,” alisema mama Wema.

NDOA YAO WATAFUNGIA CHUMBANI
Akizidi kutiririka, mama wa staa huyo alisema kama Diamond atamuoa Wema (kitu ambacho hakiamini kabisa) basi ndoa hiyo itafungiwa chumbani na upande wa Diamond tu ndiyo watakaoshiriki lakini upande wake hakuna atakayehudhuria.
“Ndoa yao watafungia chumbani, si hadharani tena wakiwa ndugu wa upande mmoja tu wa Diamond, sisi hatuwezi kushiriki ng’oo, ndugu zangu wakijitokeza tu nitakuwa na panga  mkononi, watakiona cha moto,” alisema mama huyo.

DIAMOND, WEMA
Juzi, Diamond alipigiwa simu zake zote za mkononi lakini hakuna iliyopokelewa, akatumiwa meseji yenye madai yote, hakujibu.
Kwa upande wake, Wema alisema mama yake ametoa maoni yake kama ambavyo angeweza kutoa mzazi yeyote katika mtazamo wake.

source: Globalpublishers

Sunday, 19 January 2014

RADO ANUNUA MKOKO MPYA.

Muigizaji wa filamu Swahiliwood Simon Mwapagata(Rado) amenunua gari jipya a.k.a mkoko mpya. Angalia picha hizooooo....................


DIVA KUGOMBEA UBUNGE UCHAGUZI MKUU 2015.

Diva
Loveness Malinzi a.k.a Diva ambaye ni mtangazaji maarufu wa kipindi cha Ala Za Roho kinachorushwa na Clouds fm ametangaza nia ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Diva ameandika maneno hayo hapo chini katika mtandao mmoja wa kijamii.

 Hata hivyo inadaiwa kama Diva atagombea ubunge anaweza kupata support ndogo kutoka kwa wanawake wenzake ambao ni moja ya kundi linalodaiwa kuwa mstari wa mbele kupiga kura kipindi cha uchaguzi kwani inadaiwa ni mtu wa kujishaua na kujikomba sana hivyo anaweza asifanikishe azma yake hiyo kama asipojipanga vizuri kama mwanasiasa kwani siasa si lelemama. Star mmoja wa filamu nchini baada ya kuona alichoandika Diva aliuambia mtandao huu kwa kusema  "Diva ni mtu wa kujishaua na kujikomba sana atakuwa na wakati mgumu kupata sapoti kutoka kwa sisi wanawake wenzake kwani namjua vizuri sana, anatakiwa ajue kuwa siasa sio sehemu ya mashauzi kama utangazaji, siasa ni kuwatumikia wananchi ndio tutamuunga mkono akija kupata huo ubunge mjini hapatalalika nakwambia" alisema star huyo wa filamu ambaye amedai kujuana vizuri na Diva.


 Hivi majuzi imedaiwa Diva na watangazaji wenzake B12, Adam Mchomvu, na Dj Fetty wamesimamishwa kazi Clouds fm kwa utovu wa nidhamu.

 Mtangazaji huyo mwenye sauti tamu ameandika hivi..........

kila la kheri Diva................

Tuesday, 14 January 2014

WASANII WA TANZANIA WASHINDANA KUPIGA PICHA ZA NUSU UCHI NCHINI KENYA.

Waigizaji wa filamu nchini ambao pia ni models wameonekana kushindana kupiga picha za kujiachia sana nchini Kenya ingawa ni katika mapozi na photoshoot tofauti. Salma Tamim maarufu kama Sabby Angel filamu zake nyingi akiwa na mastaa wakubwa kama Ray na Dr.Cheni zinatoka mwaka huu huku Hamisa Mobeto yeye akiwa hajacheza filamu nyingi ila akiwa active sana kwenye issue za modelling. Kwasasa inaonekana Kenya ndiyo destination mpya kwa mastaa wa Tanzania kwenda kujiachia na mapozi hatari ya ukweli. Ukiangalia hizo picha hapo chini nani kampiku mwenzake kwa hayo mapozi ya utata a.ka nusu uchi..!!


MUIGIZAJI YUSTER NYAKACHAKA ATOA MSAADA WA VYANDARUA 400 KWA YATIMA.

Muigizaji wa filamu nchini Yuster Nyakachaka ambaye filamu yake mpya akiwa na Jackline Wolper na Slim Omar inatarajiwa kutoka muda si mrefu ametoa msaada wa vitu mbalimbali  katika kituo cha watoto yatima na kina mama wajane wasiojiweza. Yuster muigizaji mwenye muonekano na umbo la kistaa alitembelea kituo hicho kitwaacho Madale Orphanage Centre kilichopo madale kata ya wazo. Muigizaji huyo aliandaa chakula cha mchana katika kituo hicho na pia kutoa vyandarau 400 kwa watoto na kina mama wajane waishio katika kituo hicho kama picha zinavyoonekana hapo chini. Muigizaji huyo pia alitoa vitu vidogo vidogo kama vile sabuni, mafuta ya kujipaka, nguo na viatu kwa watoto wote na pia khanga na vitenge. Angalia picha hapo chini.

Yuster aliyeshika mtoto akiwa na kina mama wa kituo hicho jana

Yuster akitoa msaada wa vitu mbalimbali jana katika kituo hicho

Wasanii wengine mliondekeza starehe bila kurudisha chochote kwa jamii inayosapoti kazi zenu igeni mfano.

Mungu akuzidishie sana Yuster kwa kuonyesha moyo wa kusaidia walio katika mazingira magumu.

MUIGIZAJI WA FILAMU NCHINI SABBY ANGEL AACHIA PICHA MPYA HATARI SANA.

Salma Tamim(Sabby Angel) ambaye ni muigizaji wa filamu nchini akiwa tayari amecheza filamu mpya na wasanii wakubwa kama Ray, Dr.Che ni na wengineo ameachia picha zake mpya ambazo ilikuwa shooting maalum nchini Kenya na kwa mujibu wa mtandao wa Swahiliworldplanet kuna baadhi ya kampuni za filamu kutoka Kenya zimeonysha interest kufanya filamu na muigizaji huyu wa Tanzania. Angalia picha hizo hapo chini Sabby Angel akiwa katika pose hatariiii..

Oooh babyy..................


oohh.......... this is definetly Sabby "Angel"
and we loved the styling....
Does she look hot or not...?

Part 2 of her photoshoot coming soon right here.........

Friday, 10 January 2014

ISABELA MPANDA AMCHANA LIVE SINTAH.

Isabela
Isabela Mpanda ambaye ni mwanamuziki na muigizaji wa filamu nchini ameonekana kuwa katika beef na Sintah kwa kumchana live kupitia mtandao mmoja wa kijamii. Hata hivyo sababu ya Bella kumtolea uvivu Sintah ambaye ni muigizaji wa filamu pia na blogger haijajulikana. Bella aliandika na kuweka picha ya Sintah kama inavyoonekana hapo chini...

"
Wewe sinta kwa nini unapenda kufwatilia maisha ya watu. Jione apo miwan na ilo pua lako na miziwa na viguu kama chelewa na mkorogo wa mia 2 . Nimekuchoka why wewe unapenda kufwatilia mambo ya watu. Nafikir umenielewa nini namaanisha. Na chokoza hao wapole mimi nitakufuraisha