![]() |
Nisha |
Thursday, 27 February 2014
FILAMU YA GUMZO TAYARI IPO MADUKANI JIPATIE NAKALA YAKO HALISI.
Monday, 24 February 2014
NISHA KUTOA OFFER YA KWENDA ZANZIBAR KWA TEAM NISHA.
Habari za uhakika ni kuwa star mkubwa wa filamu nchini Salma Jabu Nisha ameamua kutoa offer ya kwenda Zanzibar kwa Team Nisha mara baada ya filamu yake mpya ya GUMZO kuingia sokoni tarehe 27 mwezi huu wa February. Team nisha imekuwa ikizikubalia kazi za Nisha na Nisha mwenyewe na kumsapoti kwenye kazi zake. Mtu yeyote yule huweza kujiunga na Team Nisha WhatsApp kama unazikubali filamu za Nisha na kazi za Nisha. Nisha na Team Nisha pia hutembelea na kutoa misaada kwa wasiojiweza kama vile watoto yatima.
Nisha
Sunday, 23 February 2014
FILAMU YA "GUMZO" KUTOKA KWA NISHA YAWA GUMZO NCHI MBALIMBALI.
![]() |
Nisha akiwa kwenye interview ya Tv |
Vituo mbalimbali vya Tv kwasasa vinamhoji Nisha kuhusiana na filamu hiyo vikwemo TBC na Channel Ten. Interview ya Nisha na Channel Ten kupitia kipindi cha Action and Cut itaonyeshwa kesho Jumatatu saa tatu usiku. Zinazoonekana ni baadhi ya picha wakati Nisha akifanyiwa interview. Vile vile habari nyingine ni kuwa nchi mbalimbali tayari zinaisumbia kwa hamu filamu hiyo kutoka kwa Nisha.
Nisha na Tausi aliyecheza kama mke wa Hemedy katika filamu ya Gumzo.
Team GUMZOOOOOO
Friday, 21 February 2014
UZURI WA BATULI WAWADATISHA WAHESHIMIWA HUKO DODOMA.
![]() |
Batuli |
Chanzo hicho kiliendelea kwa kusema kuwa kilikutana na waheshimiwa hao wawili kwa nyakati tofauti katika hoteli moja iliyopo Dodoma na kumuomba awasaidie namba ya Batuli kwa madai urembo wake unawanyima usingizi "me nipo Dom kwa issue zangu binafsi nimekutana na waheshimiwa wawili(hakuwataja majina) wame-data na uzuri wa Batuli wakataka niwape namba yake nikawaambia sina, mie sipo karibu na Batuli"
Baada ya kuzipata habari hizo Swahiliworldplanet ilimtafuta Batuli na kumueleza kuhusu habari za uzuri na urembo wake kuwachanganya baadhi ya waheshimiwa huko Dodoma, star huyo wa filamu za Bad Luck na 5 Days Family alijibu huku akionyesha kushangazwa na habari hizo kwa kusema "sikwenda Dodoma kufanya uhuni kama baadhi ya mastaa wenzangu wafanyavyo wanapokuwa Dodoma, sina uhakika kuwa namba yangu ya simu ilikuwa inatafutwa na wabunge/mawaziri kwasababu kila kiongozi tuliyekutana nae hakutoka nje ya topic kabisa vile vile sikuwa peke yangu tulikuwa wengi zaidi ya 12 na kila kikao tulikaa wote kwa pamoja"
Batuli ambaye ni mmoja wa mastaa wa filamu nchini waliojipatia umaarufu kwa kazi zao na sio skendo kama baadhi ya mastaa wenzake alimalizia kwa kusema "watu huzusha maneno kutokana na mitazamo yao ila ni vyema mtu kuongea lenye ukweli, binafsi sijaona kiongozi aliyekuwa na muda wa kupoteza kwa ufupi waheshimiwa wote wapo busy sana, sisi wenyewe tulikuwa hoi kwa vikao kuna wakati tulikuwa tunamaliza vikao saa 6 usiku, kwa ufupi naweza kusema aliyefikisha taarifa hakufanya research kutosha, vile vile tuliochaguliwa kwenda Dodoma hasa hasa kwa upande wa wasichana ni mimi na Monalisa hivyo unaweza kupata picha halisi ya tuliochaguliwa na muonekano wetu mbele ya jamii"
OMARY CLAYTON NA MWENZAKE WAMALIZA MGOGORO WAO KUHUSU FILAMU YA MDUNDIKO.
Mgogoro wa chini chini uliokuwepo kati ya Omary Clayton na Timothy
Conrod kuhusu uandishi wa story ya filamu ya Mdundiko umeisha baada ya
wawili hao kukaa chini na kuyamaliza. Akizungumza na swahiliworldplanet Clayton ambaye tayari ameshaandika filamu nyingi alisema "movie ya Mdundiko ambayo
ilichukuwa tuzo nchini marekani jana ndiyo imezinduliwa rasmi. mimi ndio
mtunzi wa story ile huku screenplay ikifanywa na Timothy Conrad.. huku
kulikuwa na mgogoro wa credit nani mtunzi wa story but nashukuru now
limeisha na kukubali kuwa mimi ndio mtunzi yeye akiwa ni screenplay"
Filamu hiyo imeongozwa na Jackson Kabirigi na excutive producer akiwa ni MFDI Tanzania. Mastaa humo ndani ni pamoja na Dokii, Tino, Lumolwe Motovolwa na wengineo.
Timothy Conrod
Filamu hiyo imeongozwa na Jackson Kabirigi na excutive producer akiwa ni MFDI Tanzania. Mastaa humo ndani ni pamoja na Dokii, Tino, Lumolwe Motovolwa na wengineo.
Timothy Conrod
SWAHILIWOOD YAZINDUA FILAMU TATU KWA MPIGO.
Mkurugenzi
wa Media For Development International (MFDI) – Tanzania Bw. John Riber
akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa
Filamu tatu chini ya mradi wa Swahiliwood. MFDI inatambua umuhimu wa
tasnia ya filamu nchini, na sio
tu kwamba ni daraja linaloelezea habari za kijamii, lakini pia kama
tasnia ambayo inaweza kuleta maendeleo na ajira kwa vijana wa
Kitanzania.
Baadhi
ya wageni waalikwa waliohudhuria katika usiku wa kipekee kushuhudia
uzinduzi wa filamu za Swahiliwood wakimsikiliza Mkurugenzi wa Media For
Development International (MFDI) – Tanzania Bw. John Riber. Filamu tatu
zilizozinduliwa katika usiku wa jana ni Network, Sunshine na Mdundiko.
Wakongwe
katika tasnia ya filamu hapa nchini Tanzania Bw. Jacob Steven (JB)
kushoto na Bw. Muhsin Awadh (Dk. Cheni) wakiwa ukumbini tayari kushudia
uzinduzi wa Filamu za Swahiliwood katika Ukumbi wa Century Cinemax –
Oysterbay.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakiwa katika moja ya kumbi za Century Cinemax –
Oysterbay wakitazama filamu ya Mdundiko mara baada ya uzinduzi. Filamu
zote zinahusu mapambano ya UKIMWI ambapo watazamaji watapata elimu na
watengenezaji watapambana na kufanikiwa katika maswala ya kibiashara kwa
kuiga muundo wa Swahiliwood.
Wadau
wa Proin Promotion ambao ni wasambazaji wakuu wa Filamu zote tatu nchi
nzima wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Red Carpet ya uzinduzi wa
filamu za Swahiliwood.
credit: lukaza blog
Wednesday, 19 February 2014
TUZO ZA WATU TANZANIA ZAANZISHWA(TANZANIA PEOPLE'S CHOICE AWARDS).
Mwaka 2009, wazo jipya lilizaliwa. Wazo la kuwa na tuzo zitakazopatikana
kwa mchakato wa wazi utakaotokana na mapendekezo ya watu wenyewe ya
kuchagua mastaa wa michezo, muziki, filamu au vipindi na watangazaji
wanaopendwa zaidi. Wazo hilo liliendelea kuboreshwa na mwaka huu (2014),
limeiva na liko tayari kutoka kwenye hatua ya wazo la kichwani, na kuwa
tukio lenyewe.
“Nilizisajili na kuanzisha mwaka 2009 ila kutokana na mipango na malengo
ya kampuni niliamua kuziweka kwanza hadi sasa,” anasema Mwenyekiti wa
Bongo5 Media Group, Luca Neghesti. “Sasa hivi tumeshuhudia ukuaji katika
tasnia mbalimbali na tumeona ni wakati muafaka wa kuwatunuku wale
wanaopendwa na wananchi, kuwapatia tuzo pamoja na zawadi ya fedha taslimu
milioni 1″ ameongeza.
Tofauti na tuzo zingine, tuzo za watu hazitafuti ubora bali zinalenga
wanaopendwa zaidi na tuzo hizi hazitajikita katika tasnia moja peke yake.
Kwa kuanzia, tuzo hizi zitatolewa katika tasnia ya burudani inayojumuisha
filamu na muziki. Pia zitaiangazia sekta ya utangazaji kwa kuwatunuku
watangazaji na vipindi vinavyopendwa zaidi na watu nchini huku pia
mwanamichezo bora (soka, basketball, ndondi na michezo mingine) naye
akipewa nafasi.
Tuzo za watu si tuzo za vijana peke yake, zipo kuwakilisha watu wa rika zote.
Tofauti nyingine kubwa ni kuwa tuzo za watu zitalenga kuwatunuku watu
kutokana na umaarufu ama kupendwa kwao na si ubora. “Tuzo hizi hazileti
ushindani na tuzo zingine kwasababu hazilengi tasnia moja tu,” anafafanua
Neghesti.
“Tanzania imesifiwa kwa uhuru wa vyombo vya habari na tuzo hizi zinalenga
kujumuika na tuzo zingine kuhakikisha watanzania wanaopendwa na kufanya
vizuri wanatambuliwa.”
Upigaji kura unaanza wiki hii katika vipengele 11 ambapo wananchi wenyewe
watachagua majina ya washiriki watakaoshindana kwenye vipengele hivyo.
Awamu ya kwanza ya upigaji kura itafungwa baada ya wiki mbili kutoka siku
ya kwanza ya upigaji kura na majina ya watu watano waliotajwa zaidi kutoka
kwenye kila kipengele watachaguliwa kama watajwa wa mwisho.
Kuanzia hapo, upigaji kura wa wananchi utajikita tu katika orodha ya
majina hayo matano kwenye kila kipengele kinachoshindaniwa. Wiki moja
baada ya majina ya washiriki kutangazwa, mchujo wa kwanza utafanyika
katika kila kipengele na mtu mmoja ataondolewa.
Wiki moja baadaye, mchujo wa pili utafanyika na kuwabakiza washiriki
watatu kwenye ila kipengele.
Washiriki wote 33 (watatu katika kila kipengele) waliosalia baada ya
kufanyika mchujo wa mwisho, watakuwa wageni wa heshima kwenye utoaji wa
tuzo hizo, utakaofanyika wiki moja baada ya mchujo huo wa mwisho. Katika
hafla hiyo, washindi watatangazwa na kila mshindi atapokea zawadi ya fedha
taslimu, shilingi 1,000,000 za Kitanzania pamoja na tuzo ya thamani
iliyotengenezwa kwa mkono kutoka kwenye mali ghafi asili za Kitanzania.
Tuzo za watu mwaka 2014 zitajumuisha vipengele 11 ambavyo ni pamoja na:
1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW1 na jina’ kwenda
15678)
2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW2 na jina’ kwenda
15678)
3. MTANGAZAJI WA TV ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW3 na jina’ kwenda 15678)
4. KIPINDI CHA TV KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW4 na jina’ kwenda 15678)
5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW5 na jina’ kwenda 15678)
6. MWANAMUZIKI WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW6 na jina’ kwenda
15678)
7. MWANAMUZIKI WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW7 na jina’ kwenda
15678)
8. WIMBO UNAOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye ‘TZW8 na jina’ kwenda 15678)
9. MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW9 na jina’
kwenda 15678)
10. MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye ‘TZW10 na
jina’ kwenda 15678)
11. FILAMU INAYOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye ‘TZW11 na jina’ kwenda 15678)
JINSI YA YA KUPIGA KURA
Mchakato wa kupendekeza majina ya washiriki katika tuzo hizi utafanyika
kwa njia kuu mbili. Ya kwanza ni kwa kutumia tovuti ya tuzo hizi ambayo
ni www.tuzozetu.com ambapo utakutana na hatua rahisi ya kupendekeza na
kutaja majina katika vipengele vyote 11. Jinsi ya kupiga kura, bofya
palipoandikwa Piga Kura na ufuate hatua rahisi kabisa ambayo haikuhitaji
kujiandikisha jina wala email yako.
Njia ya pili ni kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ambapo utaandika neno
‘Tuzo’ kwenda namba 15678. Ukishafanya hivyo utaletewa Menu yenye
vipengele vyote 11 vikiwa na code number zake. Kutaja ama kupendekeza
jina, tuma code husika na jina kwenye namba hiyo hiyo; kwa mfano Justin
Bieber. Gharama ya sms ni ile ile inayotozwa sms ya kawaida.

NANI ZAIDI: MTUNISY OR RAMSEY NOUAH ?
Mtunisy na Ramsey Nouah
Nice Mohamed(Mtunisy) na Ramsey Nouah wote ni wasanii maarufu wa filamu barani Afrika. Ramsey Nouah ni muigizaji kutoka Nigeria huku Mtunisy akiwa muigizaji wa Tanzania. Hata hivyo baadhi ya watu wanadai kuwa mastaa hawa wawili wanafanana kimuonekano, utanashati na hata kiugizaji ikidaiwa kuwa wanacheza vizuri hasa nafasi za kimapenzi katika filamu. Ukiachilia mbali kiwango cha umaarufu wao na idadi ya filamu walizocheza, unadhani nani mkali zaidi katika uigizaji na suala zima la utanashati?
Subscribe to:
Posts (Atom)