Wednesday, 30 April 2014

PHOTOS: NISHA AWA BALOZI WA STEPS SOLAR PAMOJA NA JB, IRENE UWOYA NA KING MAJUTO.

King Majuto, Nisha na JB
Star mkubwa wa filamu nchi Salma Jabu "Nisha" amekuwa balozi wa kampuni ya Steps Solar ambayo hujishughulisha na uuzaji wa umeme wa jua wa bei nafuu na pia vifaa vinavyotumia umeme huo. Hii ina maana kuwa ukinunua vifaa vya umeme vya steps na huduma zao nyingine za umeme wa jua basi una uwezo wa kutumia kifaa chenye umeme seheme yoyote ile hata porini bila kuhitaji umeme wa Tanesco. Nisha ameungana na mastaa wenzake King Majuto, Jacob Stephen(JB) na Irene Uwoya ambao tayari walikuwa mabalozi wa kampuni hiyo. Uzinduzi na kutambulishwa kwa wasanii hao kama mabalozi ulifanyika leo ingawa Irene Uwoya hakuwepo leo.

SWALI: Kwa hiyo wewe King Majuto na Jacob Stephen "JB" nyote ni mabalozi au ?

NISHA: Mwanzo walikuwa JB, Uwoya na Majuto sasa hivi nimeongezeka mimi kama balozi wa Steps Solar umeme bora na rahisi kutumia usio na gharama kubwa na hauna mgao.
baadhi ya vifaa na bidhaa za Steps Solar


SWALI: .Steps Solar inajihusisha na nini na kazi zenu kama mabalozi zitakuwa zipi?

NISHA: Hizo ni baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na kampuni ya steps solar kama unavyoziona hapo kuna mafriji,maji yanayotumia nishati nuru ukame sasa kushinehi,kama mabalozi kazi yetu Kubwa ni kuwakomboa wananchi wa hali ya chini hususan na hizi adha za umeme na maji,kama tujuavyo ndio vitu vya msingi katika jamii,binafsi napenda sana kufanya kazi za kijamii naamini hapa ndipo nakamilisha msemo wa kioo cha jamii
Baadhi ya bidhaa za Steps

Kwa kiasi fulani ndio hiyo moja na pili pia tutatembelea mikoa na vijiji mbalimbali kusaidia wananchi haswa wale wenye shida hasa, ila pia hata wa mjini au mtu yyte anatakiwa atumie Steps Solar hasa hasa kulinda uchumi na matumizi yasiyo ya lazima ili tuzidi kuijenga nchi yetu Kwa kutumia chanzo asilia cha nishati nuru
SWALI: Mkataba wenu ni wa muda gani na vipi kuhusu malipo ya mkataba wenu unayaonaje?

NISHA: Malipo ni mazuri sanaaaaaa ha ha ha na mkataba kwa sasa siwezi zungumzia ni wa muda gani ila kwangu mimi nahisi hadi watanzania watakapomaliza hii adha ya umeme na maji na vifaa vya bei rahisi vinavyouzwa na steps solar ambayo utazipata maduka yote yanayouza Bongo movies au ulizia maduka yaliyo karibu yako.
Mbunge wa Kigamboni pia alikuwepo
SWALI: Una chochote ungependa kuongeza kuzungumzia?

NISHA: Sina, cha zaidi, ila nina suprise kubwa tarehe1 watege macho na masikio mashabiki zangu wapenzi

Angalia picha zaidi....................




JACKLINE WOLPER NA MTUNISY WAJA TOFAUTI.

Jackline Wolper
Mastaa wakubwa wa filamu nchini Jackline Wolper na Nice Mohamed "Mtunisy" wanaonekana kusubiriwa kwa hamu kubwa na filamu yao mpya ya TOM BOY(Jike Dume) inayotoka tarehe 1 May mwaka huu. Katika filamu hiyo kali Wolper na Mtunisy wanadaiwa kuja kivingine kabisa huku story ikiwa na fundisho kwa jamii. 

Mtunisy


NITAWACHUKULIA HATUA WASANII WASIOVAA NGUO ZA NDANI: STEVE NYERERE.

Steve Nyerere
Haya ni makubwa ! Mwenyekiti wa kundi la Bongo Movie Unity Steve Nyerere amesema kuwa atawachukulia hatua na kuwatenga baadhi ya wasanii wa kundi hilo wenye tabia ya kutovaa nguo za ndani na kupenda kukaa mikao ya kihasara wanapokuwa kwenye mizunguko yao na shughuli za kijamii na kupelekea kupigwa picha na kusambaa kwenye media na mitandaoni kwa madi wanaichafua tasnia.

 "tumechoka kunyooshewa vidole na watanzania, ni kweli kuna baadhi ya wasanii wana tabia ya kutovaa nguo za ndani na kukaa mikao ya ajabu na wakati mwingine hupigwa picha na kuwekwa mitandaoni, hiyo huwa inaidhalilisha fani hii na sasa tutakuwa wakali kupita maelezo" alisema Steve Nyerere ambaye mwenyewe anatafunwa na skendo ya kudaiwa kuwa mstari wa mbele kuwakuwadia baadhi ya wasanii wa kike kwa vigogo wa serikali na wafanyabiashara wakubwa.

Wema Sepetu Na Najma Datan Walinifilisi: Mr.Blue

Mwanamuziki maarufu wa Bongofleva Mr. Blue amesema kuwa wasanii wa filamu nchini Wema Sepetu na Najma Datan ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongofleva akiwa pia ameishi UK kwa muda mrefu walimfilisi wakati alipokuwa nao kimapenzi kwa nyakati tofauti kutokana na kuendekeza matumizi ya pesa nyingi na starehe
Akizungumza na Globalpublishers Mr. Blue ambaye aliyeanza kupata umaarufu akiwa bado kijana mdogo, alisema alilazimika kutumia fedha nyingi akiwa nao, kwani vinginevyo wangemuona hana pesa, kitu ambacho hakuwa tayari kuona kinatokea.
Mr.Blue na Najma Datan
"Mademu wengi walikuwa wanapenda sana starehe, kila day (siku) wanataka twende kiwanja, ndiyo maana kama unakumbuka niliyumba kimuziki"
"Wanawake wengi niliotoka nao hawajulikani, ila kuna Wema na Najma, ilikuwa ukizama nao dukani lazima ufanye shopping (manunuzi) ya nguvu, kuanzia laki saba, nane na kuendelea ili wakuone unazo na mademu wengi wakisikia tu umepiga shoo, sms hazikauki kuomba uwatumie mawe (pesa),” alisema.
Kuhusu maisha yake ya sasa, Mr. Blue alisema yamebadilika sana, kwani hivi sasa ameoa mwanamke mwenye asili ya Kiarabu na amejaliwa kupata mtoto mmoja, hivyo ni baba wa familia ambaye pia anakaribia kumaliza mjengo wake siku si nyingi.
Hata hivyo alisema mkewe siyo maarufu, ana malengo na upendo kwani amekuwa akimuaga kila safari anayofanya na kwamba hata yeye anaporejea nyumbani, hupokelewa vizuri.



Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao bado wanafanya muziki na wenye mashabiki wengi ndani na nje ya Tanzania.

                                                                          Wema

Friday, 18 April 2014

Irene Uwoya Kuolewa Upya Kwa Ndoa Ya Kifahari.

Irene Uwoya
Baada ya kudaiwa kutengana na aliyekuwa mumewe yaani Ndikumana Katauti toka nchini Rwanda, Star mkubwa wa filamu Swahiliwood Irene Uwoya anadaiwa kuwa katika mishe mishe za kufunga ndoa na jamaa mmoja mfanyabiashara wa Madini mwenye pesa zake ambaye anaishi Sinza, Dar es salaam. Habari zaidi zinadadavua kuwa jamaa huyo ameoza kwenye penzi la Uwoya ambaye alifunga ndoa ya kifahari na Ndikumana miaka michache nyuma na kuishia kuwa katika gogoro la mara kwa mara. Jamaa ndiye anataka kumuoa Uwoya haraka iwezekanavyo huku mashosti wa Uwoya wakimshangaa star huyo kama ataiweza ndoa hiyo baada ya kushindwa kwa Ndiku. "Inashangaza sana kwasababu hata Uwoya mwenyewe anaridhia hicho kitu, sasa sisi mashosti zake tunajiuliza alishindwa nini kwa Ndiku mpaka leo hii atake kuingia kwenye ndoa mpya?" Chanzo kililiambia gazeti la Visa

Chanzo hicho kilizidi kumwaga habari kwa kusema "huyo kijana kadata na Uwoya kwa kweli, hasikii la bibi yake wala la shangazi zake, kaamua na yeye ndiye kiherehere kutaka kumuoa Uwoya, na hizo pesa zake ndizo zinazomzuzua hata Uwoya mwenyewe"

Mashosti hao wa Uwoya walimalizia kwa kusema kuwa hata hivyo Uwoya atakuwa na wakati mgumu kwani mpaka sasa wazazi wake hawajui kuhusu issue hiyo ya ndoa mpya kwasababu wao ni waaminifu kwa dini yao ya kikiristu na pia bado wanamtambua Ndikumana kama mkwe wao kwasababu ndoa za kikiristu huwa hazivunjiki.

Mainda Aangua Kilio Kanisani kwa Madai Ya Kuharibiwa Sifa Yake Katika Jamii Na Waandishi Wa Habari.

Star mkubwa wa filamu nchini Mainda anadaiwa kuangua kilio ‘laivu’ kanisani kisa kubanwa na waandishi wa Global Publishers juu ya madai ya kupora waume za watu na ishu ya kutaka kuolewa na mchungaji hivyo kuzua ‘kitimbwili’ kwenye nyumba hiyo ya Mungu.

Mainda akilia
                                                 ENEO LA TUKIO
Timbwili hilo la aina yake lilijiri kwenye Kanisa la Kiroho la Huduma ya Inuka Uangaze lililopo maeneo ya Sinza-Lion jijini Dar hivi karibuni baada ya waandishi wetu kutinga kanisani hapo kwa lengo la kuzungumza na mchungaji wake aliyetajwa kwa jina la Mwamposa.
Ishu kubwa ilikuwa ni kujua undani wa skendo iliyoenea mjini kuwa, Mainda anadaiwa kukwapua baadhi ya waume wa waumini wa kanisa hilo na kwamba yupo kwenye maandalizi kabambe ya kufunga ndoa na mchungaji.

ANAJIPENDEKEZA KWA WAUME ZA WATU?
Ilisemekana kwamba madai hayo yalirushwa na baadhi ya waumini ikidaiwa kuwa Mainda amekuwa na tabia ya kujipendekeza kwa baadhi ya waume za watu huku wengine wakidai anataka kuolewa na mchungaji.

MCHUNGAJI AFUNGUKA
Waandishi wetu walipozinyaka habari hizo ambazo zilizua gumzo kwa baadhi ya watu hasa kwenye mitandao ya kijamii, walifunga safari hadi kanisani hapo ili kuzungumza na mchungaji huyo baada ya Mainda kukataa kupokea simu ya mapaparazi ambapo alipopatikana mchungaji huyo alifunguka anachokijua juu ya skendo hiyo.

“Mainda ni binti kama mabinti wengine ninaowalea kiroho hapa kanisani na amekuwa akijituma sana.
“Mainda ni tofauti na waumini wasanii wengine labda ndiyo sababu ya watu kumchafua.
“Kuhusiana na ukaribu na waume za watu ni uongo, hao wanaoeneza habari hizo wana nia ya kumchafua kabisa kwa sababu wameona ametoka eneo lile na kumfuata Mungu,” alisema baba mchungaji huyo.
Mchungaji huyo aliendelea kufunguka kwamba, Mainda amekuwa akikutana naye na viongozi wengine siku ya Jumatatu kwenye kamati yao ya utendaji kazi, si kwa mengine na amekuwa mstari wa mbele kwenye kazi za kujitolea huduma za kanisani.

ANAJITUMA SANA KANISANI
“Unaweza kuamini kutokana na ufanisi wake wa kazi na kujituma, ndiye muumini ambaye tumempa nafasi ya kuwa mbele watu wanapotoa ushuhuda kwa sababu ana uwezo kwa sasa na amekuwa akifanya kila analoweza kuweka safi mazingira ya kanisa,” alisema mchunga kondoo huyo wa Mungu.

KUHUSU KUMUOA
Kuhusu suala la kumuoa Mainda, mchungaji alisema kwamba yeye hana wazo la kumuoa Mainda na wala staa huyo hajawahi kuingia kwenye gari lake.
“Ni binti mwenye heshima sana na kila kukicha anakuwa muumini mwenye uwezo wa kutoa huduma kwa waumini wenzake,” aligongea msumari.

MAINDA AOMBWA AFUNGUE MOYO
Baada ya mazungumzo hayo mchungaji alimuomba msaidizi wake kumwita Mainda ili aufungue moyo wake kwa kuzungumza na waandishi wa habari ambao walikwenda pale kwa lengo la kupata ufafanuzi.

Hata hivyo, Mainda alipotoka tu na kuwaona waandishi wetu alikataa kuzungumza na kuanza kuangua kilio cha kufa mtu.
Kufuatia tukio hilo, waumini waliokuwa wakiendelea na shughuli zao kanisani hapo walimshangaa Mainda huku wakimbeba msobemsobe kumpeleka pembeni na kumbembeleza.
“Maweee…Sitakiii…Nasema sitakii…nyiii…waandishi wameniharibia sifa yangu, sitaki kuongea nao jambo lolote,” alisikika Mainda wakati akiangua kilio.

Kwa muda mrefu sasa, Mainda amekuwa akitumia muda wake mwingi kanisani akisali na kufanya usafi hivyo kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.

source: Globalpublishers

Sunday, 13 April 2014

TANZANIA YAAMBULIA NOMINATION 1 TUZO ZA AMAA 2014, WASAMBAZAJI WA FILAMU WALAUMIWA.

Nominees wa tuzo za African Movie Academy Awards 2014 wametajwa huku S.Africa na Ghana zikitamba kwenye tuzo hizo. Hata hivyo cha kusikitisha ni kwa Tanzania kupata nomination moja tu ya Best Short Film kupitia Siri Ya Mtungi. Sio kuwa Tanzania haina filamu zenye sifa za kuingia kwenye tuzo hizo, filamu zenye vigezo vya kupenya kwenye categories mbalimbali zipo sana tatizo kubwa ambalo nilijaribu kuwauliza baadhi ya wasanii na watayarishaji wa filamu siku za nyuma walisema kuwa tatizo ni wasambazaji wanaosambaza kazi zao kwani wao ndiyo wanaomiliki kazi hizo badala ya wao wasanii kutokana na mikataba kandamizi na ya kinyonyaji. Huku wasambazaji wakiwa hawaoni umuhimu wa kupeleka filamu kwenye tuzo za nje ya nchi kwa ajili ya kuitangaza Tanzania na kuzidi kuikuza tasnia ya filamu Swahiliwood.

 Tatizo linaloonekana ni kutokuwa na mfumo imara na sera ya filamu Tanzania ambayo kwasasa juhudi zinafanywa na Shirikisho La Filamu Tanzania(TAFF) kwa kushirikiana na wasanii na wadau wengine ili tasnia ya filamu iwe sekta rasmi inayotambulika serikalini. Wito wetu ni kuwa badala ya kufikiria pesa pekee wasambazaji wa filamu nchini mnatakiwa kutoa kipaumbele katika kutuma kazi za wasanii katika tuzo mbalimbali kwasababu licha ya kuitangaza na kuzidi kuikuza tasnia ya filamu Swahiliwood lakini pia itaongeza idadi ya mashabiki na wanunuzi wa filamu za kitanzania hivyo wasambazaji kufanya biashara zaidi. BASATA pi haiwezi kukwepa lawama kwa kushindwa kuruhusu na kuweka mazingira mazuri ya wadau wa filamu kuandaa tuzo za ndani ya nchi tena zaidi ya moja ambazo mara nyingi kwa nchi yoyote ile iliyopiga hatua katika tasnia ya filamu huwa ndiyo kipaumbele cha kwanza na huchochea mwamko wasanii kufanya kazi nzuri zaidi na pia kupata hamasa ya kutuma kazi zao nje ya nchi kwenye matamasha na tuzo mbalimbali.

Hiyo hapo chini ndiyo list nzima ya nominees wa tuzo za AMAA 2014.

The full nomination list
EFERE OZAKO AMAA 2014 AWARD FOR BEST SHORT FILM
Haunted Soul – Kenya
Siriya Mtungi – Tanzania
Dialemi – Gabon
New Horizon – Nigeria
Nandy l’orpheline – Mali
Living Funeral – Nigeria
Phindile’s Heart – South Africa

AMAA 2014 AWARD FOR BEST ANIMATION
The Hare and the Lion – Burkina Faso
Thank God its Friday – Morocco
Leila – Nigeria
Khumba – South Africa
The Brats and Toy Thief – Mozambique

AMAA 2014 AWARD FOR BEST DOCUMENTARY
Hamu Beya- The Sand Fishers – Mali
Potraits of a Lone Farmer – Nigeria/Denmark
Kushaya Ingagasi – South Africa
Daughters of the Niger Delta – Nigeria
Sincerely Ethiopia – Ethiopia

Ousmane Sembene AMAA 2014 AWARD FOR BEST FILM IN AN AFRICAN LANGUAGE
The forgotten Kingdom – South Africa
B for Boy – Nigeria
Omo Elemosho – Nigeria
Onye Ozi – Nigeria
Ni Sisi – Kenya

AMAA 2014 AWARD FOR BEST FILM BY AN AFRICAN LIVING ABROAD: THE JURY DECIDED THAT THERE WILL BE NO NOMINATION THIS YEAR FOR THIS CATEGORY.
AMAA 2014 AWARD FOR BEST DIASPORA SHORT
Passage – Bahamas
Heaven – USA
Tickle Me Rich – Trinidad and Tobago
Red – USA

AMAA 2014 AWARD FOR BEST DIASPORA DOCUMENTARY
Finding Samuel Lowe: From Harlem to China – USA/CANADA
Freedom Summer – USA
No Bois Man, No Frad – Trinidad and Tobago
Through the Lens Darkly : Black Photographers and the Emergence of a People – USA

AMAA 2014 AWARD FOR BEST DIASPORA FEATURE
Tula The Revolt – Curacao
AZU – Venezuela
Kingston Paradise – Jamaica
Retrieval – USA

AMAA 2014 AWARD FOR ACHIEVEMENT IN PRODUCTION DESIGN
Northern Affair – Ghana
Of Good Report – South Africa
Ni Sisi – Kenya
Good Old Days: Love of AA – Ghana
Apaye – Nigeria

AMAA 2014 ACHIEVEMENT IN COSTUME DESIGN
Good Old Days: Love of AA – Ghana
Apaye – Nigeria
Omo Elemosho – Nigeria
Ni Sisi – Kenya
The Forgotten Kingdom – South Africa

AMAA 2014 AWARD FOR ACHIEVEMENT IN MAKE-UP
A Mile From Home – Nigeria
Apaye – Nigeria
Once Upon A Road Trip – South Africa
Felista Fable – Uganda
Potomanto -Ghana

AMAA 2014 AWARD FOR ACHIEVEMENT IN SOUNDTRACK
Once Upon A Road Trip
Onye Ozi- Nigeria
Felix
Of Good Report- South Africa
Potomanto- Ghana

AMAA 2014 AWARD FOR ACHIEVEMENT IN VISUAL EFFECT
A Mile From Home
Omo Elemosho- Nigeria
Secret Room -
Ni Sisi- Kenya
Of Good Report- South Africa

AMAA 2014 AWARD FOR ACHIEVEMENT IN SOUND
Felix-
Northern Affair -
Nothing For Mahala-
Of Good Report- South Africa
The Forgotten Kingdom -

AMAA 2014 AWARD FOR ACHIEVEMENT IN CINEMATOGRAPHY
Once Upon A Road Trip
Good Old Days: Love of AA
Of Good Report
The Forgotten Kingdom
The Children of Troumaron

AMAA 2014 AWARD FOR ACHIEVEMENT IN EDITING
Of Good Report
Accident
Once Upon A Road Trip
Potomanto
Felix

AMAA 2014 AWARD FOR ACHIEVEMENT IN SCREEN PLAY
B For Boy
Of Good Report
Accident
Potomanto
Felix

AMAA 2014- BAYELSA STATE GOVERNMENT ENDOWED AWARD FOR BEST NIGERIAN FILM
Apaye
B For Boy
Accident
Murder at Prime Suites
Omo Elemosho

AMAA 2014 AWARD FOR BEST CHILD ACTOR
Tobe Oboli – Brothers Keeper
Lebohang Ntsane – Forgotten Kingdom
Hlayani Junior Mabasa – Felix

1. AMAA 2014 AWARD FOR BEST YOUNG/ PROMISING ACTOR
Evelyn Galle Ansah – Good Old Days: For the Love of AA
Petronella Tshuma – Of Good Report
Tope Tedela – A Mile From Home
Kitty Phillips – The Children of Troumatron
Shawn Faqua – Lagos Cougar

AMAA 2014 AWARD FOR BEST ACTOR IN A SUPPORTING ROLE
Desmond Elliot – Finding Mercy
Thapelo Mofekeng – Felix
Yomi Fash-Lanso – Omo Elemosho
Aniekan Iyoho – Potomanto
Tshamano Sebe – Of Good Report

MONALISA, RICHIE NA KUPA NDANI YA DODOMA.

 Bango lililopo kwenye ofisi za redio ya Rasi Fm zilizopo Mkoani Dodoma
 Muigizaji Maarufu wa Filamu za Kitanzania, Single Mtambalike aka Richie akiwa ndani ya studio za Rasi FM zilizopo Mjini Dodoma wakati wasanii hao walipotembelea redio hiyo hapo jana kwaajili ya kujionea kazi zinazofanywa na kituoo hiko cha Redio cha Rasi Fm ambacho kinapatikana kwenye masafa ya 103.7 FM katika kanda ya Kati.
 Yvonne Cherry Almaarufu Kama Monalisa akiwa ndani ya Studio za Rasi Fm wakati alipotembelea studio za Rasi FM zilizopo Mjini Dodoma
 Kalala Junior akiwa katika picha ya pamoja na Mmoja wa wafanyakazi wa Kituo hicho cha Redio cha Rasi FM kinachopatikana katika masafa ya 103.7 Fm na redio hiyo inapatikana kanda ya kati
 Kupa akiwa katika studio hiyo ya Rasi FM wakati walipotembelea kituo hiko hapo jana
Wakiwa katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya wafanyakazi wa kituo hiko cha RASI FM 103.7 FM mara baada ya kumaliza mahojiano wakati walipotembelea kituo hiko cha redio hapo jana
 

Saturday, 12 April 2014

JOHARI NA OSTAZ JUMA KATIKA VITA NZITO, JOHARI ASEMA HAWEZI KUOLEWA NA MPUUZI KAMA OSTAZ JUMA.

Johari
Staa mkubwa wa filamu Swahiliwood, Blandina Chagula ‘Johari’ ameingia kwenye vita ya maneno na bosi wa Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma Namusoma ikiwa ni siku chache tangu jamaa huyo alipotangaza kumuoa mwanadada huyo.
Wakizungumza na Globalpublishers kupitia gazeti la Risasi Jumamosi kwa nyakati tofauti, kila mmoja alitoa la moyoni huku Johari akionekana kukasirishwa mno na ishu hiyo.
KILICHOMPONZA JOHARI
Ilidaiwa kuwa baada ya Ostaz kutangaza kwamba atafunga ndoa na Johari, vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii vililichukulia jambo hilo kwa ukubwa wake kwani mwanadada huyo hakufunguka sawasawa.

WENGINE WADAI KULIPA KISASI
Habari zinasema baada ya ishu hiyo kugeuka habari ya mjini ilidaiwa kwamba labda Johari aliamua kufanya hivyo kwa kuwa mkurugenzi mwenzake wa RJ Film Production ‘RJ’, Vincent Kigosi "Ray" naye alidaiwa ‘kuchepuka’ na Chuchu Hans.
Bosi wa Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma.
Kuenea kwa habari za Johari kuolewa na Ostaz kulimsababishia usumbufu mkubwa mwanadada huyo kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki wakihoji ukweli wa ishu hiyo ili kujiandaa na cherekochereko.

MADAI YA AWALI YA OSTAZ
Ostaz alidai kuwa Johari anajua kila kitu kwani walifahamiana kitambo hata kabla ya mrembo huyo kujuana na Ray.
Hakuishia hapo, Ostaz alidai kuwa tayari amemfungulia Johari kampuni ya kutengeneza sinema pamoja na vifaa vyote hivyo yupo kwenye mishemishe za kumuoa.

JOHARI SASA
Ili kuondoa utata huo, gazeti hili lilimtafuta Johari kwa udi na uvumba na kutaka kujua undani wa ishu hiyo ambayo imezua maswali mengi hasa kwa mashabiki wake.Johari: Sijawahi, sina na wala siwezi kuwa na uhusiano na mtu mpuuzi kama yule (Ostaz Juma). Mwanzoni nilidhani utani, nashangaa imekuwa ishu kubwa.

Risasi Jumamosi: Kwani hufahamiani na Ostaz? Mbona anasema anakujua tangu unaishi Mburahati, Dar na enzi ukiwa Kaole?

Johari: Ni kweli Ostaz alikuwaga anakuja pale Kaole tulipokuwa tunafanya mazoezi lakini si yeye waliokuwa wanakuja ni wengi.

Risasi Jumamosi: Je, hajawahi kuleta maombi ya kukuoa?

Johari: Hakuwahi kunitongoza ila kila nilipokutana naye nilikuwa najua kwa kumwangalia tu machoni. Alikuwa anaonesha kabisa ananitaka lakini hakuwahi kunitamkia.

“Hajawahi kuniambia anataka kunioa. Kwanza mimi ni Mkristo. Sina ndoa mbili. Siwezi kuolewa mke wa pili na mpuuzi kama yeye.

Risasi Jumamosi: Je, zile picha zilizosambaa ukiwa umepozi kimahaba na Ostaz zilitoka wapi?

Johari: Ilikuwa nje ya RJ, nilipiga picha na watu wengi kama Dogo Janja akiwemo na huyo Ostaz. Nilipigwa na butwaa nilipoziona mitandaoni eti nina uhusiano na Ostaz huku naye akiulizwa na kudai ni kweli.
“Kwani kupiga picha na mtu ndiyo tayari mmekuwa wapenzi au wachumba? Labda yeye anachukulia hivyo kwamba ukishapiga picha na mwanamke tayari anakuwa mpenzi wako.”

Risasi Jumamosi: Kuhusu dini, Ostaz alisema atakubali uwe Mwislamu na jina lako litakuwa Rahma. Je, alishakuambia juu ya hilo?
Johari: Hajaniambia, hata  hivyo, sina mpango wa kubadili dini ili niolewe na yeye.

Risasi Jumamosi: Vipi kuhusu Ostaz kukufungulia kampuni na vifaa vya kutengenezea sinema?

Johari: Mh! Achana na kampuni au vifaa, hata simu tu hajawahi kuninunulia, kwanza hana fedha. Halafu ajue kabisa kwamba mimi ni tofauti na hao wasanii wengine wanaoishi kwa kutegemea kuhongwa. Mimi ni super woman, siku hizi huwa fedha kwangu ni makaratasi. Huyo Ostaz ana fedha gani?

“Haniwezi, mimi siyo kama hao watoto anaowadhalilisha kwa kuwapigisha magoti na akome kabisa kutumia jina langu kama daraja. Hakuna kitu ninachochukia kama mtu kutaka kutumia jina langu kujitafutia umaarufu, ana hadhi gani ya kuwa na mimi, akome kabisa, mimi nimesota, ninyi Global mnajua.”

Risasi Jumamosi: Umekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ostaz, je, una mchumba au mpenzi?

Johari: Mimi ni mwanamke niliyekamilika. Nina mchumba na ‘soon’ nitamtambulisha kwa mashabiki wangu. Lakini ijulikane kuwa siyo Ostaz kwani hawezi kuwa mchumba wangu.

Risasi Jumamosi: Au unataka kurudi kwa Ray?

Johari: (mshtuko) hivi ni nani aliwahi kutamka kwamba mimi na Ray ni wapenzi. Hapana, siyo Ray.

Risasi Jumamosi: Kwani Ray ni nani kwako?

Johari: Ray ni mkurugenzi mwenzangu wa RJ. Nje ya kazi tuna maisha yetu mengine.

Risasi Jumamosi: Je, ni mtu maarufu?

Johari: Nimeshasema nitawatambulisha subirini. Unajua mimi siyo mtu wa matangazo. 

Baada ya kumsikia Johari, Globalpublishers ilimgeukia Ostaz ambaye hakupatikana, lakini rafiki yake wa karibu alidai kuwa Johari amechanganyikiwa kwani Ostaz alikuwa amuoe kweli lakini hamuelewi mwenendo wake wa sasa.
“Johari amechanganyikiwa,” alisema rafiki huyo.




source: Globalpublishers

JINI MAHABA LAMTESA LULU NA KUSABABISHA ATONGOZWE SANA NA WANAUME.

Lulu
Vile vituko vya rejareja kutoka kwa Lulu haviishi na wala havielekei kuisha leo au kesho !. Sasa Lulu anadaiwa kukiri kuwa ana jini mahaba ambalo linamsumbua sana katika mapenzi na ndiyo sababu ya kupendwa sana na wanaume.

Akizungumza na TZA1961 Lulu alisema "Hakuna anayeweza kukubali kufanya ngono kama kuku, mara nyingi nimekuwa nikiota ninafanya mapenzi na wanaume nisio wajua na baada ya kuuliza nikaambiwa ni jini mahaba na hili limekuwa likinitesa na limepelekea niwe na mvuto wa kupendwa zaidi na wanaume ambao  baadhi yao huwa nashindwa kujizuia kuwapa uroda"

Monday, 7 April 2014

KAJALA AFUNGUKA KWA UCHUNGU KUHUSU BEEF LAKE NA WEMA NA KUTUKANWA NA TEAM WEMA.

Kajala Masanja ambaye ni star wa filamu Swahiliwood amefunguka kuwa hana tatizo na Wema ila anashangzwa sana kutukanwa matusi ya nguoni na "Team Wema" katika mitandao ya kijamii hasa Instagram kiasi cha mwanae aitwaye Paula kuona matusi hayo na kujisikia fedheha. Inadaiwa kuwa Kajala na Wema kwasasa hawapo katika urafiki mzuri kama zamani na zile millioni 13 alizowahi kulipiwa kama faini na Wema ili asifungwe gerezani zimekuwa kama wimbo wa taifa kwa team Wema kwenda kwa Kajala wakimtaka azirudishe.


Kajala akitoa maelezo kwa uchungu kudhihirisha urafiki wao wa sasa na Wema sio kama ule wa zamani

Vile vile inadaiwa kuwa wiki ilopita Wema na Kajala walikutana katika ukumbi wa Maisha Club uliopo Masaki na kushindana kumtunza Snura aliyekuwa na show lakini team Wema walipomuona Kajala wakaanza kutaka kuanzisha vurugu huku team Kajala nao wakijibu mapigo na kumlinda Kajala aliyetaka kuondoka eneo hilo kuepusha shari.

Kajala alipoulizwa na Globalpublishers kuhusu tukio hilo alikana kulishuhudia ila alikiri kutokuwa katika uhusiano mzuri na Wema kwa kusema "Mimi kwa upande wangu sina tatizo na Wema lakini natukanwa sana bila sababu. Sijui nimemfanyia nini kibaya, narudia tena sina tatizo na Wema halafu siyo yeye anayenitukana au kunisakama, ni kundi linalojiita TeamWema, sina uhakika kama yeye ndiye anawatuma, kuhusu milioni 13, sasa nitazirudishaje wakati hakunikopesha, alinilipia bure? Hata sijui kama nikizirudisha nitakuwa sahihi? Sielewi lakini kama ni matusi, kweli natukanwa sana hadi mwanangu anaona ninavyoitwa malaya" alikaririwa Kajala akisema kwa uchungu mkubwa.

Wasanii Walaani Kanumba Kuenziwa Kwa Bonanza La Muziki Kwa kiingilio Wakati Hakuwa Mwanamuziki.

Leo ni siku ya kumuenzi aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini hayati Steven Kanumba ikiwa ni miaka 2 tangu afariki dunia. Leo kuna bonanza la muziki la kumenzi Kanumba huku watu wakiingia kwa kiingilio kitu ambacho baadhi ya wasanii wenyewe wamesema sio sahihi hata kidogo bali watu wachache wanataka kumuenzi Kanumba kwa kujiingizia pesa. Baadhi ya wasanii waliondika kulalamikia hilo ni wasanii wa siku nyingi nchini Michael Sangu "Mike" na Swebe.

"NIJUAVYO MIMI KANUMBA ALIKUWA MWANAKWAYA WA KANISANI AKUWAI KUWA MWANAMUZIKI WA JAHAZI WALA WA TWANGA PEPETA IWEJE TUMUENZI KWA HAYO? JAMANI PESA ZINATAFUTWA KWELI ILA KWA NJIA HIYO YA KANUMBA SIO VIZURI WATANZANIA WENGI WANASIKITIKA SANA JAMANI ? HII NI AIBU KUBWA SANA KWA FAMILIA NA KANISA ALILOKUWA AKIABUDU KANUMBA" ameandika Mike

Nae Swebe ameandika "R.I.P RAFIKI YANGU MPENDWA.. MIAKA 2 SASA.. HAUKO TENA NASI NA HAITOTOKEA... UMEKUA MTAJI KWA WALIO HAI... BADALA YA KUOMBEWA DUWA WATU WANASHEREHEKA KWA MABENDI KUYAALIKA HUKU VIINGILIO VIKITAWALA... AMA KWA HAKIKA UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA YA FIRAUNI.... HUKO ULIKO SALAMU ZANGU NAZITUMA... KWA SASA FILAMU ZINAUZWA KWA MAJINA NA SURA NA SI UWEZO... YOTE KWA YOTE SOKO LA FILAMU LIMEKUFA BONGO.... ZANGU DUA ZITAKUFIKIA NA MUNGU MWENYE SIFA YA KUSAMEHE AKUSAMEHE.. NA WANAOFANYA DHIHAKA JUU YA HILI NAO AWASAMEHE.... HAKIKA.. KWA MUNGU SOTE TUTAREJEA.... NINA MENGI.. LAKINI KWA HAYA MACHACHE WACHA TUU NIJIFUTE CHOZI NA DUA KUKUOMBEA.... R.I.P RAFIKI YANGU MPENDWA STEVEN CHARLES KANUMBA"

Swebe ambaye aliigiza tamthilia na filamu kadhaa na Kanumba aliongeza kwa kuandika " R.I.P.... STEVEN CHARLEZ KANUMBA... ILA NATAMKA KWA HERUFI KUU.. NDG, JAMAA, NA MARAFIKI WAMEKUSALITI... KWA SABABU YA PESA... WACHACHE TUTAKUOMBEA UPUMZIKE KWA AMANI... KWA SABABU TUKO MAPITONI TUNAPITA... WENGI LEO WANATOA PESA ZAO KWENDA KUCHEZA MUZIKI ULIOANDALIWA KWA AJILI YA KUMBUKUMBU YAKO BADALA YA KUKUOMBEA MAPUMZIKO YA MILELE... HAKIKA WATAFANYA YAMCHUKIZAYO MUUMBA.. WATAKUNYWA, WATAPIGANA, NA HATA KUFANYA YASIYOSTAHILI ILIMRADI TUWAONE KWENYE MAGAZETI YAO NA KASHFA WALIZOZIZOEA... MUNGU ATAWALIPA KWA WAYAFANYAYO.... NAMUOMBA MUNGU AKUWEKE MAHALA PA AMANI NA KUKUPA MAPUMZIKO MEMA.. AAMEN.. ........KAMA UNAUNGANA NAMI..LIKE.. AU COMMENT ..AMEN.. PUMZIKA KWA AMANI STEVEN CHARLES KANUMBA."

Saturday, 5 April 2014

ODAMA, GABO NA THADEO ALEXANDER WALITEKA SOKO NA FILAMU YA JICHO LANGU.

Odama ameigiza sokoni filamu yake mpya inayoitwa JICHO LANGU akiwa na Salim Ahmed(Gabo), Thadeo Alexander na Grace Mapunda, Filamu hiyo yenye kisa cha kusisimua kwasasa inagombaniwa sokoni, wahi kununua nakala yako halisi usije ukaikosa.


RISALA YA KUNDI LA BONGO MOVIE ILIJAA UONGO: DUDE

Star wa filamu Swahiliwood Kulwa Kikumba"Dude" amesema kuwa risala iliyosomwa juzi katika sherehe za kuadhimisha miaka 3 ya kundi la Bongo Movie Unity imepikwa kwani haikuegemea katika ukweli kuhusu waanzilishi wa Kundi hilo. Akizungumza na Globalpublishers Dude ambaye ametamba na filamu nyingi sokoni na pia igizo la Bongo Dar es salaam alisema "Ile risala imepotosha, Bongo Muvi ilianzishwa na wasanii wa muziki na filamu wakiwemo mimi,  William  Mtitu, H.Baba, Simon Mwakifwamba, MwanaFA na Fid Q na wengineo kwa lengo maalum, nimeshangaa kusikia vile"

Maelezo ya Dude yanashabihiana na alichokisema Simon Mwakifwamba ambaye ni msanii pia na Rais wa Shirikisho La Filamu Tanzania kuhusu waanzilishi wa kundi hilo huku Mwakifwamba akisema kuwa Bongo movie sio chama bali ni kampuni inayomilikiwa na watu tisa na pia sio wanachama wa TAFF na kuongeza kuwa wengine katika kundi hilo wanafuata tu mkumbo wa wasichokijua.


LULU, RICHIE, STEVE NYERERE WATUA MWANZA NA TEAM YA TANZANIA MOVIE TALENT.

 Msanii wa Filamu Tanzania Elizabeth Michael (Lulu) akikumbatiana na Mmoja wa Mashabiki wa Filamu zake katika Eneo la Nyegezi Mwanza Jioni ya Leo wakati wasanii wa filamu Tanzania walipotembelea eneo hilo kwa lengo la kutambulisha Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents litakaloanza kesho Mkoani Mwanza, Mahali ni Isamilo Lodge
Baadhi ya Wakazi wa Nyegezi Mwanza wakiwa wamekusanyika kwaajili ya kuwashuhudia wasanii wa filamu Tanzania waliofika katika Viwanja hivyo vya Stendi ya Nyegezi kwaajili ya Kutambulisha Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania litakaloanzia Jijini Mwanza.
 Kijana Mmoja wa Kike ambaye jina lake halikuweza kupatikana haraka akionyesha jinsi ya kushtua Kijoti joti wakati wasanii wa filamu Tanzania Walipofika katika Viwanja vya Stendi ya Nyegezi jioni ya leo
 Msanii wa Vichekesho Joti akimchagua mmoja wa wakazi wa Nyegezi Mwanza kwaajili ya Kupewa zawadi kutoka kwake
 Lulu akiongea na wakazi wa Nyegezi Mwanza wakati walipotembelea Viwanja vya Stendi ya Nyegezi jioni ya Leo
 Baadhi ya wakazi wa Nyegezi wakinyoosha vidole kwaajili ya kuchaguliwa kujibu swali ambapo mshindi alijishindia Zawadi ya Kopi moja wapo ya Filamu ya Msanii Lulu
 Lulu akimkabidhi Zawadi ya Filamu yake ya Foolish Age kijana ambae alipatia kumtaja jina lake halisi wakati wasanii hao walipotembelea viwanja vya Nyegezi Mwanza 
 Picha ya Pamoja na Mshindi wa zawadi ya Filamu
 Msanii Rich Rich akiongea na wakazi wa Nyegezi Jioni ya Leo
 Msanii wa Filamu Tanzania Steve Nyerere ambe pia ni Mwenyekiti wa Bongo Movie akiongea na wakazi wa Nyegezi Jioni ya leo wakati wasanii walipotembelea viwanja vya stendi ya nyegezi kwaajili ya Kutambulisha na kuwahamasisha vijana na wazee kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kuonyesha Vipaji vyao Vya kuigiza katika Shindano la Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambalo linaanza rasmi Kesho jijini Mwanza mahali ni Isamilo Lodge
Wakazi wa Nyegezi Mwanza wakichungulia kwenye gari walilopanda wasanii wa kuigiza Tanzania ambao walifika katika Viwanja vya Stendi ya Nyegezi kwaajili ya kuhamasisha vijana kwa wazee kuweza kujitokeza kwa wingi Hapo Kesho katika Shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents ambalo litafanyika Isamilo Lodge kuanzia Saa Moja asubuhi na Hakuna Kiingilio. 
Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Thursday, 3 April 2014

PICHA ZA IRENE UWOYA NA BABA HAJI ZAZUA MASWALI.

Ulimwengu wa mastaa ni vituko kila siku !..... Latest gossip ni kuhusu picha mpya zinazosambaa kwa kasi mitandaoni za Star mkubwa wa filamu nchini Irene Uwoya akidaiwa kumshika maeneo yaleee a.k.a nyeti star mwenzake wa filamu Haji Adam(Baba Haji). Tukio hilo lilitokea juzi katika kuhitimisha miaka mitatu ya kundi la Bongo Movie Unity, Inaonekana Uwoya alikuwa anataniana na Baba Haji na kamera kuchukua picha iliyotafsiriwa kivingine. Lakini ukiangalia kwa makini hiyo picha ya kwanza hapo chini hakuna ukweli wowote wa tukio hilo kwani wawili hao wanaonekana kucheza muziki na kupeana nafasi ila kamera ikachukua picha kama wameshikana maeneo yaleeeeee.

Penye minong'ono ndiyo hapa............

Heee ! jamani tumeshafumwa hawa mapaparazi hawachezi mbali..!
Nasema mtuacheeeeeeee........futeni hizo picha harakaaaa