Wednesday, 28 May 2014

ZENA NA BETINA Kutoka Tarehe 12 June Na Sio Tarehe 29 May.

Nisha
"Habari mashabiki zangu,nyumbani kwetu akifa baba au dada au mwanafamilia yyte,basi km kuna aliyetaka kuolewa harusi inaghairishwa,maisha yangu ni filamu,na filamu ni nyumba yangu ya pili,sisi km NISHA'S FILM PRODUCTION NA STEPS INTERTAINMENT tumeamua kughairisha kuitoa filamu yetu mlokuwa mkiisubiri kwa hamu "ZENA NA BETINA" ilikuwa itoke tar.29/05/2014 sasa basi tutaisogeza mbele hadi tar.12/06/14 kwa ajili ya kuomboleza misiba hii,samahani kwa usumbufu uliojitokeza,munisamehe sana,tumeguswa sana,kwangu mm km Nisha kutoa filamu ni furaha,siwezi kufurahi siku tunayomzika msanii mwenzetu kipenzi RACHEL yaani kesho ambayo ndio ilikuwa siku ya kutoka ZENA NA BETINA ,nina imani kubwa kama ingekuwa mimi  filamu isingetoka kesho na hii ni zawadi yenu Rachel na Adam kuambiana kutoka NISHA'S FILM PRODUCTION. .. naomba mnisamehe sana mashabiki wangu, ila nimetazama UTU KWANZA halafu pesa baadae. wanaoendelea kufanya promo wafanye na naomba mnisaidie kusambaza ujumbe huu. . Nawapenda sana. ZENA NA BETINA itatoka tar.12/06/2014 Inshaallah siyo tar.29 tena. Cc @nishasfilmproduction" ameandika Nisha kupitia mtandao mmoja wa kijamii

Muigizaji Sabby Angel Ajichia Kwa Mapozi Sexy, Jionee Mwenyewe.


Muigizaji wa filamu nchini Salma Tamim maarufu kama Sabby Angel ametoa picha mpya akiwa katika mapozi ya ukweli na kuonyesha miguu yake ya bia.

Irene Uwoya Atoka Kimapenzi Na Dancer Wa THT.

Uwoya na Msami
Habari mpya ni kuwa star wa filamu nchini Irene Uwoya yupo kwenye penzi zito na mwalimu wa kucheza toka Tanzania House Of Talent(THT) anayeitwa Msami. Kwa mujibu wa mpenzi wa Msami anayeitwa Rehema akihojiwa katika U Heard na Soudy Brown alisema kuwa Uwoya ndiye aliyemtongoza Msami licha ya kufahamu kuwa tayari ana mpenzi mwingine(yeye Rehema). Rehema amesema kuwa Uwoya licha ya kumtongoza Msami pia anamhonga sana pesa ndiyo maana Msami akajawa na tamaa na kumkubali kwakuwa bado yeye ana-hustle kimaisha. Rehema alisema "ni tamaa tu za vijana, si unajua tena ukiwa bado hujatoka, wanashawishika na tamaa ya hela ili apate kutoka na ajulikane

Tuesday, 20 May 2014

Nisha Atinga Ofisi Za Sani Kisa Filamu Ya Zena Na Betina.

Nisha
Habari ni kuwa star wa filamu nchini Salma Jabu Nisha juzi Jumatano ya wiki iliyopita aliitwa kwenye ofisi za gazeti la Sani kuhusu issue ya Filamu ya ZENA NA BETINA ambayo imepangwa kuingia sokoni tarehe 29 mwezi huu. Sani walimuita Nisha baada ya jina la filamu yake hiyo kufanana na majina ya katuni za Zena na Betina zinazochorwa kwenye gazeti hilo kwa muda mrefu sasa. Hata hivyo mtoa habari amesema kuwa licha ya gazeti hilo kumtishia kumburuza kotini Nisha au kumtaka atoe fidia ya mil.100 lakini mazungumzo yao yanaelekea vizuri kwa hiyo filamu hiyo itaingia sokoni tarehe 29 kama ilivyopangwa kwasababu story ya filamu ya ZENA NA BETINA ni tofauti kabisa na ya katuni hizo. Story ya filamu ya ZENA NA BETINA inadaiwa kuwa nzuri sana kiasi cha wapenzi wa filamu za kitanzania kuwaisubiria kwa hamu kubwa kuinunua.

Adam Kuambiana Aagwa Katika Viwanja Vya Leaders.

Shughuli ya kuuaga mwili wa aliyekuwa muigizaji na muongozaji wa filamu hapa nchini, Marehemu Adam Kuambiana inaendelea hivi sasa kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Marehemu kuambiana anatarajiwa kuzikwa leo hii kwenye Makaburi ya Kinondoni hapa hapa jijini Dar.

Sunday, 18 May 2014

Anayoyafanaya Nisha Mastaa Wenzake Wengi Yanawashinda.

Muigizaji wa filamu mwenye jina kubwa nchini Salma Jabu Nisha hajulikani tu kwa kazi zake za filamu bali anajulikana pia kwa kujitoa katika matukio mbalimbali ya kijamii ikiwemo kusaidia wasiojiweza na watoto yatima mara kwa mara kitu ambacho hufanywa na wasanii wachache sana. Jana katika msiba wa msanii mwenzake Adam Kuambiana, muigizaji huyo aliweka u-star wake pembeni na kujitosa kupika maandazi kama anavyoonekana pichani.

Gazeti La Sani Lamshitaki Nisha Na Kumtaka Atoe Fidia Ya Mil.100 Kisa ZENA NA BETINA.

Nisha
Habari mpya ni kuwa gazeti la Sani limemshitaki star mkubwa wa filamu nchini Salma Jabu Nisha baada ya star huyo kutumia jina la katuni maarufu za Zena na Betina katika filamu yake mpya. Nisha alitumia jina la ZENA NA BETINA katika filamu yake mpya ambayo ina mastaa kibao kama vile Hanifa Daudi(Jeniifer wa Kanumba) aliyecheza kama Betina na Nisha kama Zena. Sani limemshitaki Nisha au atoe faini ya million 100 kwa kuwa Zena na Betina ni katuni maarufu toka gazeti la Sani.
Filamu ya ZENA NA BETINA ipengwa kutoka tarehe 29 mwezi huu. huku mastaa wengine ndani ya filamu hiyo wakiwa ni Senga, Manaiki Sanga, Farida Sabu, Lumolwe Matovolwa na wengineo.

Saturday, 17 May 2014

ADAM KUAMBIANA AFARIKI DUNIA GHAFLA.

Adam Kuambiana
Habari zilizoifikia muda huu ni kuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini ambaye pia ni director Adam Kuambiana Amefariki dunia muda mchache uliopita baada ya kuanguka ghafla akiwa location. Chanzo makini ambacho pia ni star mkubwa wa filamu nchini kimesema kuwa "msanii Adam Kuambiana amefariki dunia sasa hivi, alikuwa location kaanguka ghafla, maiti ipo hospital ya Marie Stopas, Mwenge, Dar es salaam. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Ameen.

Wednesday, 14 May 2014

ZENA NA BETINA Yaongelewa Kila Kona Ya Nchi Hata Kabla Ya Kuingia Sokoni

Nisha
Star wa filamu Swahiliwood Salma Jabu Nisha amewaambia mashabiki wake kuwa filamu yake mpya ya ZENA NA BETINA inayotarajiwa kutoka tarehe 29 mwezi huu sio ya kukosa kwani amefanya makubwa humo ndani akiwa na mastaa wenzake kama vile Hanifa Daudi(Jennifer wa Kanumba), Farida Sabu, Manaiki Sanga, Lumolwe Matovolwa "Biggie", Happy Nyatawe na wengineo. Yaani wasanii hao wametoana jasho katika movie hii kila mmoja kutaka kumfunika mwenzake. Filamu hiyo tayari imekuwa habari ya mjini katika maeneo mbalimbali hata kabla ya kutoka. Hakikisha unapata nakala yako halisi tarehe 29 ikiingia sokoni.

Friday, 9 May 2014

Mzuka Wa ZENA NA BETINA Wasambaa Kwa Kasi Mikoani.

Filamu mpya ya ZENA NA BETINA kutoka Nisha's Films Production chini ya mkurugenzi wake Salma Jabu Nisha imeanza kuuliziwa na mashabiki wake wengi hasa wa mikoani huku ikiwa bado kuingia sokoni. Nisha mwenyewe ambaye ni star mkubwa wa filamu kwasasa amesema kuwa anawaomba mashabiki wake watulize mzuka wa ZENA NA BETINA kwani filamu hiyo itaingia sokoni tarehe 29 mwezi huu wa tano 2014 na ndipo mashabiki wa filamu za Tanzania watakaposhuhudia humo ndani mambo yaliyofanywa na Nisha, Hanifa Daudi "Jennifer wa Kanumba", Senga, Lumolwe Matovolwa "Biggie", Farida Sabu "Mama Sonia", Manaiki Sanga na wasanii wengine machachari. Filamu hiyo imeongozwa na Leah Richard Mwendamseke "Lamata".

Monalisa, Riyama, Wastara And Cloud Shooting New Movie In London.

Wastara
About three weeks ago Tanzanian well-known movie stars, Yvonne Cherryl "Monalisa", Wastara Juma, Riyama Ally and Issa Musa "Cloud" flew to London for special invitation and shooting new film called Ughaibuni(Abroad). Shooting of the movie has already commenced in London, it is directed by Cloud . Look behind the scenes/making of the film.......

Wema Sepetu Azifuma SMS Za Mazungumzo Ya Kajala Na Clement Yule Kigogo Wa Ikulu !

Unaweza ukaficha siri na ukaamini hakuna atakayejua bila kukumbuka kuwa hakuna siri ya watu wawili ! Hatimaye Wema Sepetu amenasa ushahidi wa aliyekuwa rafikiye kipenzi, Kajala Masanja wa kumwibia aliyekuwa bwana’ke, Clement au CK, yule kigogo wa ikulu

Thursday, 8 May 2014

BASATA NA BODI YA FILAMU MSITUBANIE SANA DUNIA INABADILIKA: LULU

Star machachari kunako tasnia ya filamu nchini Elizabethn Michael "Lulu" ameviomba vyombo vinavyohusika na ukuzaji na utoaji wa vibali katika tasnia ya filamu nchini vikwemo BASATA na Bodi ya Filamu Tanzania visibane sana kuhusu wasanii kuvaa nguo fupi katika filamu kwasababu hawafanyi hivyo muda wote ila hutokea kama story imetaka muigizaji avae mavazi ya aina hiyo. Vile vile Lulu amesema kuwa mabadiliko ya mazingira na wakati yanahusika kwa wasanii kubadilika kimavazi kwasababu jamii za wakati huo ni tofauti na sasa
. "Wanasema hatufuati maadili wakati kuna movies ambazo zipo theatre na watu wanaangalia hazina maadili, wao wanataka tufanye vitu kwa kudanganya wakati sasa hivi tuko dunia ambayo tuna takiwa tuweke vitu wazi, wasibane sana" alisema Lulu wakati akizungumza na GPL

NISHA ASEMA HANYWI POMBE NA HATAKI HATA KUISIKIA.

Salma Jabu Nisha ambaye ni star wa filamu aliyekubalika kwa muda mfupi ndani ya tasnia hiyo amesema kuwa moja ya vitu ambavyo havipendi na hatakuja kuvigusa ni unywaji wa pombe. Nisha amesema kuwa hapendi pombe na pia huwa hahudhurii events zinazodhamniwa na pombe kwakuwa dini yake hairuhusu unywaji wa pombe. "mimi huwa siendi kwenye event zinazodhaminiwa na pombe, pia sinywi pombe kabisa, unajua katika sanaa huwa naigiza tu ili kufikisha ujumbe kwa jamii lakini mimi binafsi sinywi kwakuwa dini yangu ya kiislam hairuhusu" Alisema Nisha ambaye anatajwa kama mmoja wa mastaa wachache wanaojitoa kuisaidia jamii mara kwa mara.

Filamu mpya ya Nisha inayoitwa ZENA NA BETINA inatarajiwa kuingia sokoni tarehe 29 mwezi huu wa May usikose kununua nakala yako halisi.

Wednesday, 7 May 2014

Lucy Komba Amuweka Wazi Mpenzi Wake Mzungu

Star wa filamu Swahiliwood Tanzania, Lucy Komba ameamua kumuweka wazi mpenzi wake ambaye wana muda sasa tangu wawe pamoja. Jamaa huyo ni raia wa Denmark ambaye ni msanii wa muziki na pia akiwa na kazi zake nyingine mbali na muziki. Swahiliworldplanet imefanikiwa kuzipata picha za Lucy na mpenzi wake huyo kama wanavyoonekana pichani.

Nisha Apongezwa Kwa Kuisaidia Jamii Mara Kwa Mara.

Muigizaji mwenye jina kubwa katika tasnia ya filamu nchini Salma Jabu Nisha amepongezwa na watu mbalimbali kutokana na moyo wake wa kujitoa kila mara kwa jamii ya watu wasiojiweza. Nisha amekuwa akitoa misaada kwa vituo vya watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu kama alivyofanya juzi Jumapili katika kituo cha yatima huko Vingunguti, Dar es salaam kwa kutoa misaada mbalimbali kama vile unga, mafuta ya kupikia, sabuni na misaada mingine.

Wiki iliyopita pia Nisha alichaguliwa kuwa balozi wa Steps Solar
.
Tungependa kumpongeza Nisha kwa kitendo hicho cha kuisaidia jamii na kuwa mfano wa kuigwa. Kwa upande mwingine filamu mpya ya Nisha inayoitwa ZENA NA BETINA itaingia sokoni tarehe 29 mwezi May 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.

Monday, 5 May 2014

PHOTOS: NISHA ATOA MISAADA KWA WATOTO YATIMA.

Nisha akiwa na watoto hao
Star mkubwa wa filamu nchini Tanzania Salma Jabu Nisha ambaye filamu yake mpya ya ZENA na BETINA inatarajiwa kuingia sokoni tarehe 29 mwezi huu wa tano 2014 jana Jumapili alienda kutoa misaada katika kituo cha watoto yatima kilichopo vingunguti, Dar salaam. Nisha aliongozana na star mwenzake wa filamu ambaye pia ni rafiki yake wa karibu Happy Nyatawe. Nisha alitoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile unga wa kupikia, ndoo za mafuta, sabuni, juice na vitu vingine vingi. Baada ya hapo Nisha, Team Nisha, watoto hao yatima na walezi wao walijumuika kutoa burudani huku watoto hao baadhi wakionyesha vipaji vyao ikiwemo kucheza muziki na kuigiza. Nisha pia alitoa pesa taslim kwa mlezi wa kituo hicho ambaye hakusita kutoa shukrani kwa Nisha na team yake nzima kwa msaada huo. Angalia baadhi ya picha za tukio hilo...........

Friday, 2 May 2014

Muigizaji wa Filamu Sabby Angel Kugombea Ubunge 2015.

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania Sabby Angel ambaye filamu zake mbili zaMoto Wa Radi akiwa na Mohamed Musa na Siri Ya Giningi akiwa na Salim Ahmed "Gabo" muda wowote kuanzia sasa zitaingia sokoni amesema kuwa anapenda siasa na kuna uwezekano siku za usoni akajitosa mzima mzima ili kuwatumikia wananchi. Haikujulikana kama Sabby Angel atagombea ubunge au nafasi gani ingawa elimu yake ni ya chuo. "Nina interest na siasa and siku za usoni naweza kuingia huko rasmi" alisema Sabby akizungumza na Swahiliworldplanet

Monalisa, Wastara, Cloud Na Riyama Ally Waibukia London, Uingereza.

Mastaa wa filamu nchini Monalisa, Riyama Ally, Wastara na Cloud wapo London, Uingereza kufanya filamu mpya inayoandaliwa na kampuni ya Didas Entertainment. Angalia picha.,.

Wastara, Cloud na Monalisa
                                                      Cloud and Wastara
                                                           Cloud and Riyama Ally
                                                       Wastara
                                                                   Riyama Ally
xxxxxxx

Kajala Adai Kuogopa Kushika Simu Yake Sababu Ya Beef Lake Na Wema Sepetu.

Wema na Kajala
Kajala Masanja ambaye ni star wa filamu nchini amesema kuwa imefikia hatua anaogopa kushika simu yake kutokana na ugomvi wake na Wema Sepetu ambao amedai kuwa umekuzwa na watu na media kiasi cha kutokea kweli ugomvi baina yao lakini wao walitofautiana kwa kitu kidogo tu na cha kawaida  sio kama inavyodaiwa kuwa alimchukulia Wema mwanaume(Clement yule kigogo wa ikulu). Akizungumza katika kipindi cha TakeOne kupitia Clouds Tv Kajala alisema kuwa anaumizwa sana na hali hiyo na alishamwambia Wema wamalize tofauti zao lakini ikashindikana.

Kajala alipoulizwa kuhusu madai kuwa alianza kumdharau Wema baada ya kuanza kuyumba katika suala la pesa Kajala alipangua madai hayo kwa kusema kuwa walikuwa marafiki muda mrefu hata kabla Wema hajawa na pesa hivyo asingeweza kufanya kitendo hicho " alikuwa rafiki yangu kabla hana kitu, kwa hiyo madai kwamba nilianzisha urafiki na Wema kwasababu alikuwa na hela lakini sasa hivi hana hela tena mimi sio rafiki yangu tena sio kweli" alisema star huyo wa filamu za Devil Kingdom, Kigodoro na Kijiji Cha Tambua Haki.

Kajala aliongeza kwa kusema kuwa kutofautiana kwao kumemuathiri "inaniathiri sana kwasababu ni mtu ambaye nimemzoea, mtu ambaye tumefanya vitu vingi kwahiyo sometimes nikikaa nam-miss"