Thursday, 12 June 2014

Zena Na Betina Yaingia Sokoni Kwa Kishindo Kikubwa.

Filamu ya Zena Na Betina imeingia kwa kishindo sokoni leo hii, Hakikisha unanunua nakala yako halisi

Wednesday, 11 June 2014

Zena Na Betina Kuwasha Kivumbi Sokoni Kesho Tarehe 12 June.

Nisha
Filamu ya ZENA NA BETINA ambayo imekuwa masikioni mwa watu kwa muda sasa kutokana na kupata promo ya kutosha kutoka kwenye media zikiwemo tv, magazeti, blogs na mitandao mingine ya kijamii inatarajiwa kuingia sokoni kesho tarehe 12 June kwa kishindo kikubwa. Filamu hiyo imetengenezwa na Nisha's Film Production huku wasanii wenye majina kama vile Salma Jabu Nisha, Manaiki Sanga, Hanifer Daudi "Jennifer wa Kanumba", Farida Sabu, Senga, Happy Nyatawe na Lumolwe Matovolwa akionyesha uwezo wao kisanaa. Usikose kununua nakala yako halisi

Sunday, 8 June 2014

Filamu Ya ZENA NA BETINA Kutikisa Soko La Filamu Nchini !

Zimebaki siku chache kwa filamu ya ZENA NA BETINA kuingia sokoni huku ikisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa filamu za kitanzania. Filamu hiyo itaingia sokoni tarehe 12 mwezi huu wa June. Mastaa ndani ya movie hiyo ni Nisha, Manaiki Sanga, Jennifer wa Kanumba, Senga, Farida Sabu na wengineo. usikose kununua nakala yako halisi.

Shamsa Ford Afunguka Kufuatia Picha Chafu Zinazodaiwa Kuwa Zake Akiwa Na Mbunge Kusambaa.

Shamsa Ford
Picha chafu zinazodaiwa kuwa za star wa filamu nchini Shamsa Ford na mbunge wa Chadema, Salvatory Machemli zimeanza kusambaa kwa kasi mitandaoni tangu jana,. Picha hizo zinawaonyesha wawili hao wakiwa kitandani kwenye mahaba mazito. Hata hivyo picha hizo zinatia shaka kuwa sio halisi ni za kutengenezwa ingawa hatuna uhakika kwa asilimia zote kwasababu msichana anayedaiwa kuwa Shamsa Ford ana umbo tofauti na la star huyo, Shamsa ana umbo la kawaida ki-shape lakini msichana huyo anaonekana kuwa na umbo namba nane.

Wema Sepetu, Diamond Na Aunty Ezekiel Katika Red Carpet MTV Africa Music Awards 2014

Wema na Diamond
Jana ilikuwa kilele cha tuzo za MTV Africa Music Awards ambapo Diamond Platnumz alikuwa amependekezwa katika vipengele viwili na kukosa kuibuka mshindi. Katika red carpet mastaa wa Tanzania akiwemo Diamond mwenyewe, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel walikuwepo kutuwakilisha Tanzania angalia picha zilivyokuwa na unadhani nani alipendeza zaidi?

Thursday, 5 June 2014

Nisha Ndani Ya TBC1 Katika Interview Kuhusu Zena Na Betina.

Nisha
Star wa filamu nchini Salma Jabu Nisha leo atakuwa na interview na kituo cha tv cha TBC1 kwa ajili ya kuizungumzia filamu yake mpya ya ZENA NA BETINA ambayo tayari inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa filamu za kitanzania. Interview hiyo itarushwa hewani Jumamosi hii. Zena Na Betina inaingia sokoni tarehe 12 June huku mastaa wengine wakiwa ni Khanifa Daudi "Jennifer wa Kanumba", Farida Sabu, Manaiki Sanga, Happy Nyatawe, Senga na Lumolwe Matovolwa

Monday, 2 June 2014

ZENA NA BETINA Yasubiriwa Kwa Hamu Kubwa.

Filamu ya ZENA NA BETINA ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa filamu za kitanzania inatarajiwa kuingia sokoni kwa kishindo tarehe 12 June. Hakikisha unanunua nakala yako halisi