Tuesday, 17 February 2015

Sitaki Kuwa Na Mume Ambaye Ni Maarufu: Johari

Mrembo na mwigizaji  wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa kamwe hatarajii kuolewa na staa kama Vicent Kigosi ‘Ray’ bali anahitaji mume wa kawaida asiye maarufu. Akizungumza na Uwazi, Johari alisema kuwa kwa upande wake hachagui mwanaume gani wa kumuoa bali tu ajue kumthamini na kumuheshimu kama mwanamke.

Nisha Kutoa Funzo Kubwa.

MWIGIZAJI wa filamu nchini, Salma Jabu ‘Nisha’, amesema anatarajia kuachia kazi yake mpya aliyoipa jina la ‘Shida’, ambayo itatoa mafunzo kwa mashabiki kukabiliana na hali yoyote ya maisha.
Akizungumzia filamu hiyo hapo jana, Nisha alisema filamu hiyo inatarajia kuingia sokoni mwishoni mwa mwezi huu, ambapo ameweza kumshirikisha nguli mwingine, Gabo.

Saturday, 14 February 2015

VICHWA VIWILI ADIMU VYAKUTANA PAMOJA NDANI YA ''SHIDA''

Anaitwa Salma Jabu wengi wanamfahamu kama ''NISHA'' ndiye msanii aliyechukua tunzo ya mchekeshaji bora wakike wakutana na msanii mwenzie aliyechukua tunzo ya muigizaji bora wakiume Salim Ahmed anajulikana kama ''GABO ZIGAMBA''.  ''SHIDA'' ndio movie iliyowakutanisha mastar hawa. Unataka kujua wamefanya nini humo Tarehe 23 mwezi huu itakuwa sokoni usikose nakala yako ama neneeeeeeeeeeeeeeee!!!!!

Nataka Nizae Mtoto Mwingine Sasa: Kajala

Mrembo na muigizaji wa  filamu za Kibongo, Kajala Masanja amefunguka kuwa ni muda muafaka wa kufanya mishemishe za kumtafuta mtoto mwingine kwani yule wa kwanza, Paula ameshakua.

Selembe Toko Kuja na Mambo Makubwa Mwaka Huu.

Msanii wa filamu za kiswahili mwenye makazi yake nchini Denmark Selembe toko amesema kuwa nagependa kuwatakia heri ya Valentine Day mashabiki wake hsa wale walio katika mapenzi halisi ya kweli. Selembe amesema pia kuwa kuna kazi kubwa ya filamu inakuja muda si mrefu hivyo mashabiki wake watarajie kitu kikubwa mwaka huu.

Monday, 9 February 2015

NISHA NA GABO NDANI YA FILAMU IITWAYO SHIDA,MWISHO WA MWEZI HUU

''Zanzibar ndipo lilipo chimbuko langu,nlikuja dar baada ya baba yangu kufariki
nikiwa darasa la nne,kipaji na maisha ya sanaa nnayafanya dar kwa %95,siku nliyopata simu ya wazanzibar kutaka nicheze filamu ya SHIDA hakika sikurudi nyuma nliwaambia leteni story niipitie kwanza,nna mwiko wa kucheza filamu za nje ya kampuni yng ya NISHA"S FILM PRODUCTION,Ila nilijishangaa kuipenda SHIDA kabla sijaiona  script na story iliponiridhisha niliwaambia YES bila ya tatizo lolote .. kuanzia crew nzima ya Zanzibar house of talent chini ya mwanamke anayejituma na kujali wasanii wake na vipaji  bi ZUBEDA,, SHIDA iliisha salama huku vipaji vipya vikionesha uwezo wa hali ya juu,, SHIDAAAA tar.23 mtaani utapata kuniona mimi Nisha na Gabo,Ndambwe,Zainabu(Tunu) na Bi Zubeda mwenyewe.

Davina Akiri Kumuonea Wivu Lulu Kwa Mafaniko Yake Kisanaa Baada Ya Kuwa Chini Ya Management Nzuri.

Akipiga stori na paparazi wa GPL kuhusiana na ishu ya msanii huyo ambaye ni mdogo zaidi yake, kufikia hatua ya kulipwa shilingi milioni kumi na tano kwa filamu moja, ni mafanikio makubwa ambaye anayatamani sana.

Kwasasa Nataka Kuolewa Na Kuanzisha Familia: Wema Sepetu

Wema Sepetu anaonekana kuchoka kuwa katika mahusiano pasipo ndoa baada ya kusema kuwa sasa anataka kuolewa. Kupitia reality show yake ya In My Shoes Ijumaa usiku alisema kuwa sasa anataka kutulia kuna mambo anaweka sawa ikiwemo kutaka kuolewa.

Friday, 6 February 2015

Photos: Kuna Kitu Kinakuja Toka Kwa Wema Sepetu Na Ommy Dimpoz?

Wema Sepetu ame-share hizo picha akiwa na Ommy Dimpoz na mashabiki kujiuliza nini kinakuja baina ya wawili hao...

Van Vicker Amkumbuka Lulu

Muigizaji maarufu wa Ghana Van Vicker ameonekana kukumbuka good time aliyokutana na kupiga picha na star wa filamu Tanzanina Lulu Elizabeth Michael baada ya jana kuweka picha waliyopiga mwaka 2013 kama inavyyonekna hapo chini

Sunday, 1 February 2015

SHIDA COMING SOON

HAYA KWA WALE WAPENZI WA GABO PAMOJA NA NISHA MLIOKUWA MKITAKA WAFANYE KAZI PAMOJA KILIO CHENU KIMESIKIKA SOON MZIGO UTAKUWA MTAANI TEGA SIKIO NA MACHO KUJUA LINI INATOKA