Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekumbwa na masaibu mapya ya kuvamiwa na vibaka nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar na kumuibia simu zake mbili aina ya Iphone.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo wezi hao wanadaiwa kuruka ukuta na kufanikiwa kuvunja dirisha la chumba anacholala mrembo huyo na kumliza simu hizo huku yeye akiwa amelala fofofo.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wezi hao walitumia mbinu za ‘kisayansi’ kutekeleza zoezi lao kwani siku hiyo Lulu alirudi nyumbani mapema na akawa anachati kwa kutumia moja ya simu hizo, ghafla akapitiwa ambapo alikuja kushtuka na kukuta dirisha limevunjwa na simu zimetoweka.