Tuesday, 31 December 2013

BEHIND THE SCENES: NISHA, AGNES MASOGANGE, JENIFER NA SENGA NDANI YA MOVIE MPYA.

Star maarufu wa filamu Swahiliwood Salma Jabu Nisha yupo location maeneo ya Dar es salaam akishuti filamu yake mpya huku akiwa amemshirikisha Agnes Masogange ambaye ni video queen maarufu nchini. Katika filamu hiyo mpya pia yupo Jenifer aliyetamba na marehemu Kanumba katika filamu za Uncle JJ na This Is It. Pia yupo mchekeshaji maarufu Senga ambaye anaonekana kudatishwa na wowowo la Agnes Masogange kama anavyoonekana pichani hapo chini..................






Friday, 27 December 2013

SNURA AKUMBUKA FADHILA ZA WEMA SEPETU.



Snura na Wema Sepetu

YUSTER NYAKACHAKA MUIGIZAJI ANAYEKUJA JUU KWA KASI NA KAMPUNI YAKE YA EAGLE ENTERTAINMENT.

Yuster
Yuster Nyakachara ni msanii wa filamu anayekuja kwa kasi nchini kiasi cha kuwa tishio kwa mastaa wengine wakubwa kwasasa. Ukiachilia uigizaji Yuster ni mmiliki wa kampuni ya utengenezaji wa filamu iitwayo Eagle Entertainment ambayo tayari imeshatoa filamu nyingi na kwasasa inakuja na filamu mpya inaitwa Majuto Si Hasara itakayoingia sokoni hivi karibuni huku wastaa wengine wakiwa Jackline Wolper na Slim Omar

                                                                           Yuster

Thursday, 26 December 2013

JACKIE CLIFF ADAIWA KUKAMATWA NA UNGA NCHINI CHINA.

Jackie Cliff
Jackie Cliff ambaye ni socialite na video queen wa Bongo anadaiwa kukamatwa na dawa za kulevya  nchini China. Star mmoja nchini aliyekataa kutajwa jina lake aliutonya mtandao huu bila kufafanua zaidi kwa kusema kuwa Jackie amekamatwa na madawa ya kulevya China "Jackie Cliff amekamatwa na unga China". alisema star huyo huku akitutumia na picha za mwanamke aliyefungwa kitambaa usoni baada ya kukamatwa na dawa hizo na mwanamke huyo anadaiwa ni Jackie Cliff. Angalia picha hizo hapo chini..........

Hata hivyo baadhi ya mitandao leo  iliweka habari za mwanamke mmoja wa kitanzania kukamatwa na dawa za kulevya huko china lakini bado habari hizo hazikubainisha mwanamke huyo ni nani na usiku huu ndiyo ikasemekana ni Jackie Cliff. Habari hiyo inasomeka  ..........

"Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.

Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.

Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013."


Tunaendelea kuzifuatilia habari hizi tutakuletea updates zaidi...........



DIAMOND NA WEMA SEPETU WAJIACHIA LIVE.

Diamond na Wema Sepetu hakuna ubishi ni wapenzi rasmi kama zamani na Peniel Mungilwa hana chake kutokana na ishara za wawili hao kuwa penzini waziwazi. Habari mpya ni kuwa show ya Diamond jana ilipambwa na Wema Sepetu jukwaani kwa kuimba pamoja huku watu wakifurahia wawili hao kuwa jukwaani wote. Angalia picha hapo chini ilivyokuwa kwa Wema na Diamond jana...........


Tuesday, 24 December 2013

MERRY X-MAS FROM JOKATE.



KAJALA AKANA MADAI YA KUTEMBEA NA MUME WA SHAMIM MWASHA.

Shamim na Kajala
Jana gazeti la SANI lilikuwa na habari ukurasa wa mbele ikidai star wa Swahiliwood Kajala Masanja anatembea na mume wa Shamim Mwasha ambaye ni blogger maarufu wa 8020fashions. Baada ya habari hiyo kutoka leo Kajala amejibu mapigo ya habri hiyo akionekana kuchukizwa na habri hiyo. Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Kajala ameandika "nadhani namjua huyu dada siku nyingi sana hata kabla ya wengine wenu kumjua, tunaheshimiana sana na hatujawahi kukoseana sasa sijui nanai aliyeanzisha habari ya mimi kutembea na mume wake na sijui alifanya hivyo kwa makusudi gani, naumia kila siku kwa ajili ya ujinga wa watu na hayo magazeti nikiwaambia nipeni ushahidi wa kuwa natembea na mume wa Shamim sijui kama mtafanya daah sijui niseme nini @ 8020fashions mpenzi enjoy ndoa yako achana na wapumbavu, nimevumilia nimeona bora leo niandike unajua sipendagi kuongea lakini gazeti la jana limenikwaza sana"





credit: swahiliworldplanet

Gazeti lenyewe liliandika hivi

SHAMSA FORD AJIACHIA NA MTOTO WAKE.

Thursday, 19 December 2013

WEMA SEPETU ADAIWA KUFILISIKA NA KUANZA KUUZA MALI ZAKE.

Wema Sepetu
NI kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha? Kama ni kweli, basi ile jeuri ya fedha ya Miss Tanzania mwaka 2006 ambaye pia hufanya vyema kwenye gemu la sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu inadaiwa imefikia nchani, Risasi Mchanganyiko limepashwa ‘ei tu zedi’.

Baadhi ya magari anayomiliki Wema.
Kwa mujibu wa chanzo makini, hali ya kifedha ya staa huyo si nzuri kiasi kwamba kwa sasa amekuwa mtu wa kushinda ndani kwa kuwa hana mpunga unaomuwezesha kwenda kujirusha kama zamani.

SABABU NI NINI HASA?
Chanzo kilidai kwamba, binadamu aliyekuwa akimmwagia manoti staa huyo aliyetajwa kwa jina moja la Clement ambaye ni mwajiriwa wa Ikulu jijini Dar, yu hoi kwa kipato baada ya kunyofolewa kwenye kitengo kilichokuwa na uwezeshaji mwingi wa fedha.
Wema akiwa ofisini kwake.
Inadaiwa kuwa, baada ya Clement ambaye ni mume wa mtu, kuondolewa kwenye kitengo hicho amepelekwa sehemu nyingine ambayo mchana kutwa ni kupiga miayo mpaka muda wa kutoka kazini.

MKONO WA MKEWE WATAJWA
Katika madai hayo, inasemekana mke wa Clement (jina tunalo) ana mkono wa kile kilichompata mumewe, kuondolewa kwenye kitengo chenye ulaji na pia amekuwa akiwawinda wawili hao ili awafanyie fumanizi kwa sababu Clement ni mumewe wa ndoa.

KILICHOTOKEA SASA
Chanzo kikaendelea: “Baada ya kuondolewa kwenye sehemu yenye fedha na kutupwa kwenye ukame, jamaa akaanza kupata tabu kwani fedha alizokuwa akimpa Wema zamani zikawa hazipo.
“Hilo likamwathiri na Wema mwenyewe kwani ile jeuri mliyokuwa mnamuona nayo akiifanya kwa rungu la fedha, mara sherehe, mara kumlipia Kajala (Masanja) makahamani (Kisutu), mara kwenda baa na wapambe imekatika ghafla.
“Siku hizi Wema ndani na yeye, yeye na ndani. Naamini hata mkienda kwake muda huu (juzi Jumatatu saa 5 asubuhi) mtamkuta.”

INADAIWA AMEUZA MAGARI MAWILI
Habari zaidi kutoka chanzo hicho, hali ilipozidi kubana sana, Wema aliamua kuuza magari mawili kati ya matatu anayomiliki ili apate fedha za kuendelea kujikimu katika maisha ya kila siku.
Magari hayo mawili yanasemekana ni Toyota Mark II GX 110 na Toyota Harrier na kubakiwa na Audi Q7.

YALIYOMPATA CLEMENT
Habari zinazidi kudai kwamba hali ikazidi kuwa mbaya kwa Clement kiasi kwamba alijikuta akikabwa koo na benki moja ya jijini Dar es Salaam ambayo aliiomba mkopo wa Shilingi mil. 120 akitumia hati ya nyumba ambayo pia si yake.
Benki hiyo ilipozidi kumbana, mkewe (sasa wametengana) ambaye naye anadaiwa kuwa ‘mzuri’ kwenye fedha alikwenda kulipa fedha hizo benki ili nyumba ya watu isinadiwe na benki hiyo iliyokuwa haitaki mambo ya utani kwenye marejesho.
Madai mengine ambayo hayajathibitishwa yanasema kuwa, mtikisiko huo wa kifedha kwa Clement umesababisha awe ‘choka mbaya’ kiasi cha sasa kuanza kupiga mizinga kwa rafiki zake.

WEMA ASAKWA ASEME UKWELI WAKE
Baada ya kupokea ishu hiyo, Risasi Mchanganyiko liliamua kumsaka Wema ili aseme lolote kuhusiana na tuhuma hizo.
Saa 4:32 Wema alipigiwa simu yake ya mkononi ambayo iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa hata pale iliporudiwa tena na tena.
Baada ya jitihada hizo kugonga mwamba, gazeti hili liliamua kumwendea hewani meneja wake Martin Kadinda ambaye naye hakupokea simu licha ya kupigiwa zaidi ya mara tatu.
Risasi Mchanganyiko halikukata tamaa, kwani ni haki ya msingi kwa Wema kuongelea suala hilo. Likampigia msaidizi wake wa karibu anayeitwa Pat Man, yeye alipokea, akaulizwa kuhusu bosi wake huyo, akasema:
“Wema anaumwa (hakutaja ugonjwa), ametoka hospitali sasa hivi  (hakusema hospitali gani) yuko nyumbani.”
Mapaparazi wetu wakafunga safari kutoka Bamaga – Mwenge, Dar yalipo Makao Makuu ya Nyumba ya Magazeti Pendwa Bongo, Global Publishers hadi nyumbani kwa Wema - Makumbusho (lakini ni Kijitonyama).
Getini alikutwa mlinzi mahiri kwa mwonekano ambapo alipoombwa kumwita Wema au kumwambia kuna waandishi wa Global wapo nje, alisema:
“Mh! Kwa kweli si rahisi kutoka, amelala anaumwa... alikwenda hospitali amerudi muda si mrefu.”
Alipochombezwa kwa maneno ya ‘kisiasa’ kwamba awaambie wasaidizi wake wa ndani wakamwamshe, alikataa akisema litazuka timbwili ambalo yeye hakuwa tayari kuliona.
“Bosi akilala huwa hapendi kuamshwa, hasa kama hayuko sawa. Watu wanaomwamsha ni wale wenye ahadi naye,” alisema mlinzi huyo.

WEMA ATUMIWA MESEJI
Baada ya kuondoka nyumbani kwa Wema, Risasi Mchanganyiko lilimtumia ujumbe mfupi (SMS) ‘mreeefu’ wenye madai yote na ikaonesha ‘delivered’ kwenye simu ya Wema, lakini pia haikujibiwa.

TUNARUDI KWA CLEMENT  
Simu yake haikuwa ikipatikana hewani alipopigiwa ili na yeye apewe nafasi ya kusema lolote kuhusu sakata hilo.

MKE WA CLEMENT AVUNJA UKIMYA
Risasi Mchanganyiko liliamua kumsaka kwa simu ya mkononi mke wa Clement ambapo alipopokea na kusomewa mashitaka ya mumewe na nafasi yake kama shahidi muhimu alikiri hali ya jamaa kuwa tete kimfuko.
“Kuhusu hilo la nyumba ni kweli ilikuwa inadaiwa na benki (aliitaja jina) na walitaka kuinadi ili wapate fedha zao, lakini nikaingilia kati ili kulinda heshima ya familia.
“Unajua ile nyumba kuna mtu alituuzia, kwa hiyo Clement alitoa kiasi cha fedha lakini hakumalizia na akatumia hati ya nyumba kwenda kuombea huo mkopo. Kwa sababu benki walikuja juu nilitafuta mtu akainunua, kiasi cha fedha nikammalizia aliyetuuzia na kulipa benki,” alisema mwanamke huyo.

KUHUSU KUMFANYIA FITINA MUME AKAHAMISHWA KITENGO
Huyu hapa mke wa Clement: “Hilo si kweli bwana. Kwanza mimi ndiyo nilimfikisha pale alipofika. Sasa mtu nimuinue mwenyewe nitamfanyiaje fitina?
“Kwanza mimi siko naye siku hizi. Nilipoona anachukua magari ya nyumbani na kuyapeleka huko kwa nani sijui (Wema) nikaamua kukaa pembeni na kunyamaza kimya.
“Kama ni mabalaa anayapata hukohuko aliko, nisisingiziwe mimi kwa lolote lile.”
KUHUSU KUMWANDALIA FUMANIZI WEMA
“Aaa wapi! Nimwandalie fumanizi la nini? Yeye ana maisha yake mengine mimi niko na mambo yangu, muda huo sina kabisa, yaani niko bize sana,” alisema mwanamke huyo huku akidai muda huo alikuwa akidraivu.

PRODYUZA WA WEMA ALIJUA HILI?
Wiki mbili zilizopita, gazeti damu moja na hili, Ijumaa Wikienda liliandika katika ukurasa wake wa mbele habari yenye kichwa; MAGARI YA WEMA YAGEUZWA GESTI.
Katika habari hiyo, Wema alidaiwa kumtimua kazi prodyuza wake katika Kampuni ya Endless Fame, Rashid Mohammed ‘Chid Classic’ kwa sababu ya kumtuhumu kufanya ufuska kwenye magari yake maeneo ya Ufukwe wa Coco, Dar.
Siku chache mbele, prodyuza huyo alifunguka katika gazeti lingine pendwa ndani ya mjengo, Amani kuwa, Wema ‘amechoka’ siku hizi, halipi mishahara wafanyakazi wake na alitaka yeye awe kuwadi ndiyo wangeendana jambo ambalo yeye hakuwa tayari.


HABARI NYINGINE YA MJINI
Yapo madai kuwa, kutokana na maswahibu hayo ya kuwa kwenye wakati mgumu kifedha, kampuni yake imeanza kudoda na mbaya zaidi, marafiki zake anaokuwa nao kwenye raha, wamemkacha na kumwacha akihangaika mwenyewe.
“Msiniandike gazetini lakini ukweli ni kuwa, huu ndiyo wakati wake wa kujifunza kuchagua marafiki. Ona sasa, wale wote aliokuwa akila nao raha, wamekaa pembeni. Ni tatizo sawa, lakini pia ni funzo kwa upande mwingine,” alisema mpambe mmoja anayefanya naye kazi kwa karibu sana.

source: Globalpublishers

MR.NICE APATA SHAVU LA KUCHEZA FILAMU NCHINI DENMARK.

Mr. Nice kutoka Tanzania ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya aliyewahi kujipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi akiwa na style yake ya Takeu kupitia nyimbo kama Kidali Po na Kikulacho amepata nafasi ya kucheza filamu huko Denmark kupitia wasanii wa VAD productions wenye asili ya kiafrika hasa kutoka nchini Congo ambao hufanya kazi na wasanii wa nchi za Afrika hususani Afrika mashariki.

Mr. Nice amepata nafasi hiyo huku akiwa hajawahi hata siku moja kucheza filamu nchini Tanzania na dalili za kucheza filamu Swahiliwood zikiwa bado hakuna. Wasanii wa VAD kwa ujumla wamefurahi kuwa na MR. Nice nchini humo.

Angalia picha za uchukuaji wa filamu hiyo na nyingine ambazo sio za uchukuaji wa filamu hiyo.....


                                          credit: Swahiliworldplanet

IRENE PAUL AKERWA NA PART 1 NA PART 2 KATIKA FILAMU ZA KITANZANIA.

Msanii nyota wa filamu Swahiliwood Irene Paul ameponda staili ya filamu za kitanzania kutoka sehemu ya kwanza na ya pili na kubatizwa jina la part 1 na Part 2 amesema kuwa zimekuwa ni kikwazo kwa filamu hizo kushiriki katika matamasha na tuzo zinazoandaliwa nje ya Tanzania, anasema nashangaa kwani hakuna sehemu nyingine ya mfumo huo ispokuwa Tanzania pekee.


"Hakuna sababu ya filamu moja kukatwa na kuwa na sehemu mbili yaani Part 1 na Part 2 ukituma katika matamasha ya tuzo nje unapata usumbufu inabidi inakuchukua muda kwa marekebisho wakati ilikuwa jambo rahisi kuwa na Dvd moja tu unajaza fomu na kutuma sehemu husika" alisema Irene Paul akizungumza na mtandao wa Filamucental
 
Msanii huyo anasema kuwa hivi karibuni alikuwa anafuatilia filamu yake kuipeleka katika tamasha fulani kubwa la filamu alikutana na usumbufu ambao anaamini ni mfumo uliowekwa na wafanyabiashara wachache ambao wananufaika na mfumo huo wa kutoa Dvd sehemu mbili kwa filamu moja na kubatiza jina la part 1 na Part 2.
Irene anasema kajifunza mengi kwa wenzetu waliosonga mbele katika masuala ya filamu huku sisi Tanzania tukipigania hatua kwa taratibu kuelekea katika medani za kimataifa.

                                                               Irene Paul
 

Monday, 16 December 2013

HEMEDY PHD STARS IN A NEW MOVIE WITH ZAMBIAN STARS.

anzanian Swahiliwood star Hemedy Suleiman landed Lusaka,Zambia on Friday 6 December to shoot new movie called "Tangled Mess" starring Hemedy, Zambian Love Games Star Cassie kabwita, Big Brother Africa 8 "the chase" male representative the ruby master Sulu Banda, Zambian music legendary Moureen Lilanda and Zambia's best DJ Yahya Kiba KB. The movie is a tribute to the late Steven Kanumba.






                                                      images by Majoy