Msanii nyota wa filamu Swahiliwood Irene Paul ameponda staili ya filamu za
kitanzania kutoka sehemu ya kwanza na ya pili na kubatizwa jina la part
1 na Part 2 amesema kuwa zimekuwa ni kikwazo kwa filamu hizo
kushiriki katika matamasha na tuzo zinazoandaliwa nje ya Tanzania,
anasema nashangaa kwani hakuna sehemu nyingine ya mfumo huo ispokuwa Tanzania pekee.
"Hakuna sababu ya filamu moja kukatwa na kuwa na sehemu mbili yaani
Part 1 na Part 2 ukituma katika matamasha ya tuzo nje unapata usumbufu
inabidi inakuchukua muda kwa marekebisho wakati ilikuwa jambo rahisi
kuwa na Dvd moja tu unajaza fomu na kutuma sehemu husika" alisema Irene Paul akizungumza na mtandao wa
Filamucental
Msanii huyo anasema kuwa hivi karibuni alikuwa anafuatilia filamu
yake kuipeleka katika tamasha fulani kubwa la filamu alikutana na
usumbufu ambao anaamini ni mfumo uliowekwa na wafanyabiashara wachache
ambao wananufaika na mfumo huo wa kutoa Dvd sehemu mbili kwa filamu moja
na kubatiza jina la part 1 na Part 2.
Irene anasema kajifunza mengi kwa wenzetu waliosonga mbele katika
masuala ya filamu huku sisi Tanzania tukipigania hatua kwa taratibu
kuelekea katika medani za kimataifa.
Irene Paul
No comments:
Post a Comment