Leo ni siku ya wanawake duniani ambapo kila pembe ya dunia mwanamke
anadhimishwa kwa kutambua mchango wake katika kada mbalimbali. Sekta ya
burudani nchini kuanzia filamu muziki, utangazaji, mitindo, urembo na
hata blogging imezungukwa na wanawake ambao kwa namna moja au nyingine
wametoa power flani katika kazi zao kiasi cha kuzidi kupata mafanikio au
kujijengea heshima kwa namna moja au nyingine licha ya kukutana na
changamoto kadhaa. Power ni mvuto, power ni ushawishi, power ni hazina
ambayo kwa namna moja au nyingine humfanya mtu mwenye nayo kutambulika,
kubadilisha au kushawishi vitu au watu flani kubadilika.
Swahiliworldplanet
imekuletea wanawake 25 kutoka kwenye entertainment industry ya Tanzania
wenye power iliyopelekea mabadiliko ya vitu flani au kwa namna yoyote
ile. Hawa wanatoka katika filamu, muziki, mitindo, urembo, utangazaji na
uandishi wa blogging unaogusa tasnia ya burudani moja kwa moja. kumbuka
majina hayajawekwa katika mpangilio maalum kuwa huyu ni wa kwanza na
yule ni wa mwisho
1.WEMA SEPETU
Ni Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu
nchini, Wema hakauki katika vyombo vya habari nchini kutokana na skendo
za mara kwa mara au maisha yake binafsi na ya kimapenzi.
Power quotient: Filamu anayoigiza iwe mbaya au nzuri ni
lazima iuze sokoni kutokana na kuwa na nyota ya kupendwa na watu wengi
licha ya kuwa kipaji chake cha uigizaji kinatia shaka na wasiwasi.
2. LADY JAYDEE
Ni mwanamuziki wa muda mrefu ambaye nyimbo
zake nyingi zimekuwa hits, ana mashabiki wengi na nyimbo zake nyingi
hata za zamani hazichuji.
Power quotient: Queen of Bongofleva, Wakati industry ya muziki wa Bongofleva
ikionekana kushikiliwa zaidi na wanaume, Jaydee amedhihirisha kuwa
kipaji anacho na ni jasiri kuliko mwanaume. Jaydee haogopi mtu yeyote
yule anayemuwekea kauzibe mbele yake na kuzuia mafanikio yake. Mpaka
sasa hana mpinzani wa kike katika muziki wa Bongofleva licha ya kuwa na
zaidi ya miaka kumi kwenye game. She is the most successful "Anaconda"
diva in the music industry.
3: FLAVIANA MATATA
Ni mwanamitindo wa kimataifa kutoka
Tanzania akiwa na makazi yake nchini marekani, ameshatokea kwenye shows
za designers wakubwa duniani na fashion weeks kubwa kama vile London na
New York Fashion Weeks. Kupitia foundation yake ya Flaviana Matata
anawasaidia wanafunzi mbalimbali wa msingi na secondary hasa wasichana
mahitaji mbalimbali ya shule.
Power quotient: Role model wa wanamitindo wengi chipukizi nchini Tanzania na Africa kwa ujumla.
4. YVONNE CHERRYL "MONALISA"
Ni muigizaji wa filamu wa muda
mrefu nchini Tanzania, tayari ameigiza filamu nyingi na anakubalika.
Filamu yake ya Girlfriend ndiyo inadaiwa kuleta ushawishi na mapinduzi
ya kutengeneza filamu za kibiashara nchini.
Power quotient: Endless Fame and talent, ni zaidi ya miaka 12
tangu Monalisa aanze kuigiza na kupata umaarufu na hawajawahi kuchuja
tofauti na waigizaji wenzake wengi wa kike aliowika nao miaka hiyo ambao
hawajulikani walipo huku wengine wakijikongoja kwenye tasnia. Monalisa
pia anachukuliwa kama atress wa Tanzania mwenye sifa za kuwika
kimataifa.
5.SALAMA JABIRI
Ni mtangazaji wa muda mrefu sasa alipijipatia umaarufu na na kipindi cha Planet Bongo na sasa Mkasi show vyote vikirushwa EATV.
Power quotient: Game changer...ingawa kwa sasa Salama hatangazi
tena kipindi cha Planet Bongo lakini aliweza kuleta mapinduzi kwa
wanamuziki wengi wa Bongofleva kufanya video nzuri kutokana na kuzikosoa
video mbovumbovu bila kumuonea aibu mtu so wanamuziki wengi wakawa na
hofu ya kufanya video zisizo na viwango kwa kuogopa kulipuliwa na
salama. mapaka leo watu wanakumbuka mchango na nguvu ya bidada huyu.
6.RITA PAUSLEN(MADAM RITA)
Ni mwanzilishi wa shindando
maarufu la kusaka vipaji nchini liitwalo Bongo Star Search aliyeibua
vijana wengi kupitia shindano hilo.
Power quotient: Madam Rita ni kimbilio la vijana wengi wanaotaka
kutoka kupitia muziki na kiuchumi lakini hawajui waanzie wapi so
wanajitosa Bongo Star Search. Akiwa kama mwanamke ameweza kilisimamia
shindano hilo na kusimama vizuri tangu lianzishwe mpaka leo licha ya
washindi wengi kushindwa kufurukuta baada ya kushinda.
7.MARIA SARUNGI -TSEHAI
Ni mwandaaji wa mashindano ya Miss
universe, Miss Eath Tanzania ambaye ameibua vipaji vingi vya urembo
kupitia mashindano anayoandaa.
Power quotient: Ameweza kuondoa kasumba kuwa warembo wa Tanzania
hawafurukuti katika mashindano ya kimataifa kutokana na warembo wengi
wanaoshinda katika mashindano anayoyaandaa kufanya vizuri kimataifa
kuliko mwandaaji mwingine yeyote wa mashindano ya urembo nchini. Mfano.
mzuri ni Flaviana Matata, Miriam Odemba na Tetemaria Mallya ambao
waliingia final za mashindano ya kimataifa na kushika nafasi za juu.
Soma list nzima katika link hii hapa
25 Powerful Women In the Tanzanian entertainment industry.