Saturday, 8 March 2014

MASTAA 25 WA KIKE TANZANIA WENYE NGUVU KATIKA FILAMU, MUZIKI, UREMBO NA MITINDO.

Leo ni siku ya wanawake duniani ambapo kila pembe ya dunia mwanamke anadhimishwa kwa kutambua mchango wake katika kada mbalimbali. Sekta ya burudani nchini kuanzia filamu muziki, utangazaji, mitindo, urembo na hata blogging imezungukwa na wanawake ambao kwa namna moja au nyingine wametoa power flani katika kazi zao kiasi cha kuzidi kupata mafanikio au kujijengea heshima kwa namna moja au nyingine licha ya kukutana na changamoto kadhaa. Power ni mvuto, power ni ushawishi, power ni hazina ambayo kwa namna moja au nyingine humfanya mtu mwenye nayo kutambulika, kubadilisha au kushawishi vitu au watu flani kubadilika. Swahiliworldplanet imekuletea wanawake 25 kutoka kwenye entertainment industry ya Tanzania wenye power iliyopelekea mabadiliko ya vitu flani au kwa namna yoyote ile. Hawa wanatoka katika filamu, muziki, mitindo, urembo, utangazaji na uandishi wa blogging unaogusa tasnia ya burudani moja kwa moja. kumbuka majina hayajawekwa katika mpangilio maalum kuwa huyu ni wa kwanza na yule ni wa mwisho


1.WEMA SEPETU
 Ni Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu nchini, Wema hakauki katika vyombo vya habari nchini kutokana na skendo za mara kwa mara au maisha yake binafsi na ya kimapenzi.


Power quotient: Filamu anayoigiza iwe mbaya au nzuri ni lazima iuze sokoni kutokana na kuwa na nyota ya kupendwa na watu wengi licha ya kuwa kipaji chake cha uigizaji kinatia shaka na wasiwasi.



2. LADY JAYDEE
Ni mwanamuziki wa muda mrefu ambaye nyimbo zake nyingi zimekuwa hits, ana mashabiki wengi na nyimbo zake nyingi hata za zamani hazichuji.


Power quotient: Queen of Bongofleva, Wakati industry ya muziki wa Bongofleva ikionekana kushikiliwa zaidi na wanaume, Jaydee amedhihirisha kuwa kipaji anacho na ni jasiri kuliko mwanaume. Jaydee haogopi mtu yeyote yule anayemuwekea kauzibe mbele yake na kuzuia mafanikio yake. Mpaka sasa hana mpinzani wa kike katika muziki wa Bongofleva licha ya kuwa na zaidi ya miaka kumi kwenye game. She is the most successful "Anaconda" diva in the music industry.


3: FLAVIANA MATATA
Ni mwanamitindo wa kimataifa kutoka Tanzania akiwa na makazi yake nchini marekani, ameshatokea kwenye shows za designers wakubwa duniani na fashion weeks kubwa kama vile London na New York Fashion Weeks. Kupitia foundation yake ya Flaviana Matata anawasaidia wanafunzi mbalimbali wa msingi na secondary hasa wasichana mahitaji mbalimbali ya shule.


Power quotient: Role model wa wanamitindo wengi chipukizi nchini Tanzania na Africa kwa ujumla.


4. YVONNE CHERRYL "MONALISA"
Ni muigizaji wa filamu wa muda mrefu nchini Tanzania, tayari ameigiza filamu nyingi na anakubalika. Filamu yake ya Girlfriend ndiyo inadaiwa kuleta ushawishi na mapinduzi ya kutengeneza filamu za kibiashara nchini.


Power quotient: Endless Fame and talent, ni zaidi ya miaka 12 tangu Monalisa aanze kuigiza na kupata umaarufu na hawajawahi kuchuja tofauti na waigizaji wenzake wengi wa kike aliowika nao miaka hiyo ambao hawajulikani walipo huku wengine wakijikongoja kwenye tasnia. Monalisa pia anachukuliwa kama atress wa Tanzania mwenye sifa za kuwika kimataifa.


5.SALAMA JABIRI
Ni mtangazaji wa muda mrefu sasa alipijipatia umaarufu na na kipindi cha Planet Bongo na sasa Mkasi show vyote vikirushwa EATV.


Power quotient: Game changer...ingawa kwa sasa Salama hatangazi tena kipindi cha Planet Bongo lakini aliweza kuleta mapinduzi kwa wanamuziki wengi wa Bongofleva kufanya video nzuri kutokana na kuzikosoa video mbovumbovu bila kumuonea aibu mtu so wanamuziki wengi wakawa na hofu ya kufanya video zisizo na viwango kwa kuogopa kulipuliwa na salama. mapaka leo watu wanakumbuka mchango na nguvu ya bidada huyu.


6.RITA PAUSLEN(MADAM RITA)
Ni mwanzilishi wa shindando maarufu la kusaka vipaji nchini liitwalo Bongo Star Search aliyeibua vijana wengi kupitia shindano hilo.


Power quotient: Madam Rita ni kimbilio la vijana wengi wanaotaka kutoka kupitia muziki na kiuchumi lakini hawajui waanzie wapi so wanajitosa Bongo Star Search. Akiwa kama mwanamke ameweza kilisimamia shindano hilo na kusimama vizuri tangu lianzishwe mpaka leo licha ya washindi wengi kushindwa kufurukuta baada ya kushinda.


7.MARIA SARUNGI -TSEHAI
Ni mwandaaji wa mashindano ya Miss universe, Miss Eath Tanzania ambaye ameibua vipaji vingi vya urembo kupitia mashindano anayoandaa.


Power quotient: Ameweza kuondoa kasumba kuwa warembo wa Tanzania hawafurukuti katika mashindano ya kimataifa kutokana na warembo wengi wanaoshinda katika mashindano anayoyaandaa kufanya vizuri kimataifa kuliko mwandaaji mwingine yeyote wa mashindano ya urembo nchini. Mfano. mzuri ni Flaviana Matata, Miriam Odemba na Tetemaria Mallya ambao waliingia final za mashindano ya kimataifa na kushika nafasi za juu.
Soma list nzima katika link hii hapa 25 Powerful Women In the Tanzanian entertainment industry.

No comments:

Post a Comment