Sunday, 21 June 2015

Hii Ndioo Maana Ya Msemo Wa Msanii Ni Kioo Cha Jamii

Namshukuru M/MUNGU kwa kuweza kutusaidia kufanikisha jambo nililolipanga kuwa iwe kawaida yangu kuwasaidia wale wenye matatizo na waishio katika mazingira magumu napenda kuwashukuru watoto wangu TEAM NISHA kwa kujumuika nami jana bila kujali umbali tuliokwenda pia natoa shukrani zangu za dhati kwa vyombo vya habari.
Napenda kuongea jambo moja kuna watu wanasema nikitoa mkono wa kushoto wakulia usijue wakiwa namaana unapotoa sadaka hutakiwi kutangaza huku wakiwa wamesahau kuwa mimi ni msanii na msanii ni kioo cha jamii natakiwa nifanye mambo mazuri na kuionyesha jamii ili nawao waige yale mazuri niyafanyayo.
Hawa watoto wanaishi mbali sana nasehemu wanayoishi hakuna huduma za muhimu zilizopo karibu mfano Maduka,Hospital,Shule n.k hawana usafiri kusema mtoto akiumwa usiku wamuwahishe hospital je tusipo tangaza nani atajua kuna watu wanahitaji msaada?
                              HIVYO NI BAADHI YA VITANDA VYA WATOTO HAO

                                 WANAMAHITAJI MENGI WANAYO HITAJI
                                KAMA VITANDA,MAGODORO,MASHUKA,VYANDARUA




No comments:

Post a Comment