Friday, 21 August 2015

Gabo: Sijaona Msanii Wa Kushindana Nae Katika Filamu Nchini.

Msanii wa filamu aliyejizolea umaarufu miaka ya hivi karibuni, Salim Ahmed maarufu kwa jina la Gabo amesema haoni msanii anayempa changamato.
Akizungumza kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, Gabo alisema wengi wamekuwa wakimwambia anaringa kutokana na kuwaambia ukweli.
“Kwa hapa Tanzania sijui ndio maana wanasema mimi naringa,” alisema Gabo alipoulizwa ni msanii gani anayempa changamoto.

“Nyuma alikuwa Single Mtambalike, sasa hivi sijaona wa kumtazama na kunipa changamoto tuweze kushirikiana kupeana nguvu. Kwa single sijui nisene vitu vinakwenda vinaisha! Lakini simuoni tena yule, sasa hivi amekuwa akifanya kazi anakuwa ni yule yule, hakuna mabadiliko. Lakini nikimwangalia yule single wa filamu za nyuma nasemaga yule jamaa, amebadilika kabisa na kuwa wa kawaida,” aliongeza.
Gabo amesema kuwa pamoja na filamu za Tanzania kuwa na changamoto, amefanikiwa kupata mafanikio mengi.
“Mimi kama ningekuwa nchi nyingine ningekuwa mtu mkubwa sana,” alisema.
“Ukiangalia uwezo wangu mimi na jinsi ninavyoishi havilingani. Nimekuwa nikitembelea nchi kama Afrika Kusini na Jumatatu kama Mungu akipenda naenda Botswana, watu wanakuona huyooo kumbe maandazi tu hamna chochote! Kitu kikubwa ambacho nilikuwa nakihitaji kwa sasa ni kampuni yangu ya Sarafu Media, nilitamani iwe strong mtu akija anaogopa, lakini sasa ipo kampuni jina, mtu akija anaona huyu naye anaanza.
Kingine mimi nimejenga nje ya sanaa, hata kwangu pale nikilala najiona bado. Ndioa maana nikapangisha kule nikaja kukaa Kinondoni ili nitafute kwa jasho la filamu. Mimi ninachojivunia kwa sasa kilichopatikana kutokana na filamu ni gari (Passo), ndio maana sasa hivi naboresha zaidi kazi zangu hata mtu akinihitaji kufanya filamu yake aandae milioni 8,” alisisitiza.

No comments:

Post a Comment