Friday, 21 August 2015

Lulu Avamiwa Na Vibaka.

Elizabeth Michael ‘Lulu’ amekumbwa na masaibu mapya ya kuvamiwa na vibaka nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar na kumuibia simu zake mbili aina ya Iphone.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo wezi hao wanadaiwa kuruka ukuta na kufanikiwa kuvunja dirisha la chumba anacholala mrembo huyo na kumliza simu hizo huku yeye akiwa amelala fofofo.
Kwa mujibu wa chanzo makini, wezi hao walitumia mbinu za ‘kisayansi’ kutekeleza zoezi lao kwani siku hiyo Lulu alirudi nyumbani mapema na akawa anachati kwa kutumia moja ya simu hizo, ghafla akapitiwa ambapo alikuja kushtuka na kukuta dirisha limevunjwa na simu zimetoweka.

“Nimemhurumia sana Lulu kwa kuwa siku ambayo ameibiwa, simu kesho yake tena akafiwa na bibi yake mzaa mama ambaye ndiye alikuwa kipenzi chake sana. Hapo utagundua alipata majanga kiasi gani maana wakati alikuwa bado anafikiria ishu ya simu huku tena akakumbana na janga la kifo.
“Amelazimika kutafuta simu nyingine anayoitumia sasa tofauti na awali alikuwa nazo mbili,” kilisema chanzo hicho.
Paparazi wetu baada ya kupenyezewa ubuyu huo, alimtafuta Lulu ili aizungumzie ishu hiyo, ambapo alikiri kufikwa na masaibu hayo huku akishindwa kufafanua zaidi juu ya tukio hilo kwa kile alichodai alikuwa sehemu yenye kelele.
“Ni kweli nimepata matatizo sana mwezi huu ikiwa pamoja na hilo la kuibiwa simu, sema kwa hapa nilipo siwezi kuzungumzia lolote maana nipo katikati ya watu wengi na kuna makelele sana. Lakini itakuwa vyema nikikutafuta baadaye,” alisema.
Licha ya Lulu kutotaja kiasi, simu hizo zinakadiriwa kufikia kiasi cha shilingi milioni tatu.

No comments:

Post a Comment