Sunday, 18 May 2014

Gazeti La Sani Lamshitaki Nisha Na Kumtaka Atoe Fidia Ya Mil.100 Kisa ZENA NA BETINA.

Nisha
Habari mpya ni kuwa gazeti la Sani limemshitaki star mkubwa wa filamu nchini Salma Jabu Nisha baada ya star huyo kutumia jina la katuni maarufu za Zena na Betina katika filamu yake mpya. Nisha alitumia jina la ZENA NA BETINA katika filamu yake mpya ambayo ina mastaa kibao kama vile Hanifa Daudi(Jeniifer wa Kanumba) aliyecheza kama Betina na Nisha kama Zena. Sani limemshitaki Nisha au atoe faini ya million 100 kwa kuwa Zena na Betina ni katuni maarufu toka gazeti la Sani.
Filamu ya ZENA NA BETINA ipengwa kutoka tarehe 29 mwezi huu. huku mastaa wengine ndani ya filamu hiyo wakiwa ni Senga, Manaiki Sanga, Farida Sabu, Lumolwe Matovolwa na wengineo.
Nisha alipotafutwa kuzungumzia sakata hilo number yake ilionekana kutokuwa hewani kwa wakati. Filamu hiyo hata kabla ya kutoka tayari imeonekana kuwa gumzo kwa wafuatiliaji mbalimbali wa filamu za kitanzania kutaka wajue kilichomo ndani ya filamu hiyo.

No comments:

Post a Comment