Tuesday, 20 May 2014

Nisha Atinga Ofisi Za Sani Kisa Filamu Ya Zena Na Betina.

Nisha
Habari ni kuwa star wa filamu nchini Salma Jabu Nisha juzi Jumatano ya wiki iliyopita aliitwa kwenye ofisi za gazeti la Sani kuhusu issue ya Filamu ya ZENA NA BETINA ambayo imepangwa kuingia sokoni tarehe 29 mwezi huu. Sani walimuita Nisha baada ya jina la filamu yake hiyo kufanana na majina ya katuni za Zena na Betina zinazochorwa kwenye gazeti hilo kwa muda mrefu sasa. Hata hivyo mtoa habari amesema kuwa licha ya gazeti hilo kumtishia kumburuza kotini Nisha au kumtaka atoe fidia ya mil.100 lakini mazungumzo yao yanaelekea vizuri kwa hiyo filamu hiyo itaingia sokoni tarehe 29 kama ilivyopangwa kwasababu story ya filamu ya ZENA NA BETINA ni tofauti kabisa na ya katuni hizo. Story ya filamu ya ZENA NA BETINA inadaiwa kuwa nzuri sana kiasi cha wapenzi wa filamu za kitanzania kuwaisubiria kwa hamu kubwa kuinunua.

No comments:

Post a Comment