Thursday, 8 May 2014

NISHA ASEMA HANYWI POMBE NA HATAKI HATA KUISIKIA.

Salma Jabu Nisha ambaye ni star wa filamu aliyekubalika kwa muda mfupi ndani ya tasnia hiyo amesema kuwa moja ya vitu ambavyo havipendi na hatakuja kuvigusa ni unywaji wa pombe. Nisha amesema kuwa hapendi pombe na pia huwa hahudhurii events zinazodhamniwa na pombe kwakuwa dini yake hairuhusu unywaji wa pombe. "mimi huwa siendi kwenye event zinazodhaminiwa na pombe, pia sinywi pombe kabisa, unajua katika sanaa huwa naigiza tu ili kufikisha ujumbe kwa jamii lakini mimi binafsi sinywi kwakuwa dini yangu ya kiislam hairuhusu" Alisema Nisha ambaye anatajwa kama mmoja wa mastaa wachache wanaojitoa kuisaidia jamii mara kwa mara.

Filamu mpya ya Nisha inayoitwa ZENA NA BETINA inatarajiwa kuingia sokoni tarehe 29 mwezi huu wa May usikose kununua nakala yako halisi.

No comments:

Post a Comment