Muigizaji mwenye jina kubwa katika tasnia ya filamu nchini Salma Jabu Nisha amepongezwa na watu mbalimbali kutokana na moyo wake wa kujitoa kila mara kwa jamii ya watu wasiojiweza. Nisha amekuwa akitoa misaada kwa vituo vya watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu kama alivyofanya juzi Jumapili katika kituo cha yatima huko Vingunguti, Dar es salaam kwa kutoa misaada mbalimbali kama vile unga, mafuta ya kupikia, sabuni na misaada mingine.
Wiki iliyopita pia Nisha alichaguliwa kuwa balozi wa Steps Solar
.
Tungependa kumpongeza Nisha kwa kitendo hicho cha kuisaidia jamii na kuwa mfano wa kuigwa. Kwa upande mwingine filamu mpya ya Nisha inayoitwa ZENA NA BETINA itaingia sokoni tarehe 29 mwezi May 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
No comments:
Post a Comment