Saturday, 17 May 2014

ADAM KUAMBIANA AFARIKI DUNIA GHAFLA.

Adam Kuambiana
Habari zilizoifikia muda huu ni kuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini ambaye pia ni director Adam Kuambiana Amefariki dunia muda mchache uliopita baada ya kuanguka ghafla akiwa location. Chanzo makini ambacho pia ni star mkubwa wa filamu nchini kimesema kuwa "msanii Adam Kuambiana amefariki dunia sasa hivi, alikuwa location kaanguka ghafla, maiti ipo hospital ya Marie Stopas, Mwenge, Dar es salaam. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Ameen.
Enzi za uhai wake Kuambiana alianza kujipatia umaarufu baada ya kuigiza filamu ya Fake Pastors na baada ya hapo kucheza filamu nyingi zilizompa umaarufu kabala ya kuanza kuwa director.

                                                      Adam Kuambiana

No comments:

Post a Comment