Wema na Kajala |
Kajala alipoulizwa kuhusu madai kuwa alianza kumdharau Wema baada ya kuanza kuyumba katika suala la pesa Kajala alipangua madai hayo kwa kusema kuwa walikuwa marafiki muda mrefu hata kabla Wema hajawa na pesa hivyo asingeweza kufanya kitendo hicho " alikuwa rafiki yangu kabla hana kitu, kwa hiyo madai kwamba nilianzisha urafiki na Wema kwasababu alikuwa na hela lakini sasa hivi hana hela tena mimi sio rafiki yangu tena sio kweli" alisema star huyo wa filamu za Devil Kingdom, Kigodoro na Kijiji Cha Tambua Haki.
Kajala aliongeza kwa kusema kuwa kutofautiana kwao kumemuathiri "inaniathiri sana kwasababu ni mtu ambaye nimemzoea, mtu ambaye tumefanya vitu vingi kwahiyo sometimes nikikaa nam-miss"
No comments:
Post a Comment