Friday, 9 May 2014

Mzuka Wa ZENA NA BETINA Wasambaa Kwa Kasi Mikoani.

Filamu mpya ya ZENA NA BETINA kutoka Nisha's Films Production chini ya mkurugenzi wake Salma Jabu Nisha imeanza kuuliziwa na mashabiki wake wengi hasa wa mikoani huku ikiwa bado kuingia sokoni. Nisha mwenyewe ambaye ni star mkubwa wa filamu kwasasa amesema kuwa anawaomba mashabiki wake watulize mzuka wa ZENA NA BETINA kwani filamu hiyo itaingia sokoni tarehe 29 mwezi huu wa tano 2014 na ndipo mashabiki wa filamu za Tanzania watakaposhuhudia humo ndani mambo yaliyofanywa na Nisha, Hanifa Daudi "Jennifer wa Kanumba", Senga, Lumolwe Matovolwa "Biggie", Farida Sabu "Mama Sonia", Manaiki Sanga na wasanii wengine machachari. Filamu hiyo imeongozwa na Leah Richard Mwendamseke "Lamata".

No comments:

Post a Comment