|
Irene Uwoya |
Baada ya kudaiwa kutengana na aliyekuwa mumewe yaani Ndikumana Katauti
toka nchini Rwanda, Star mkubwa wa filamu Swahiliwood Irene Uwoya
anadaiwa kuwa katika mishe mishe za kufunga ndoa na jamaa mmoja
mfanyabiashara wa Madini mwenye pesa zake ambaye anaishi Sinza, Dar es
salaam. Habari zaidi zinadadavua kuwa jamaa huyo ameoza kwenye penzi la
Uwoya ambaye alifunga ndoa ya kifahari na Ndikumana miaka michache nyuma
na kuishia kuwa katika gogoro la mara kwa mara. Jamaa ndiye anataka
kumuoa Uwoya haraka iwezekanavyo huku mashosti wa Uwoya wakimshangaa
star huyo kama ataiweza ndoa hiyo baada ya kushindwa kwa Ndiku.
"Inashangaza sana kwasababu hata Uwoya mwenyewe anaridhia hicho kitu,
sasa sisi mashosti zake tunajiuliza alishindwa nini kwa Ndiku mpaka leo
hii atake kuingia kwenye ndoa mpya?" Chanzo kililiambia gazeti la
Visa
Chanzo hicho kilizidi kumwaga habari kwa kusema "huyo kijana kadata na
Uwoya kwa kweli, hasikii la bibi yake wala la shangazi zake, kaamua na
yeye ndiye kiherehere kutaka kumuoa Uwoya, na hizo pesa zake ndizo
zinazomzuzua hata Uwoya mwenyewe"
Mashosti hao wa Uwoya walimalizia kwa kusema kuwa hata hivyo Uwoya
atakuwa na wakati mgumu kwani mpaka sasa wazazi wake hawajui kuhusu
issue hiyo ya ndoa mpya kwasababu wao ni waaminifu kwa dini yao ya
kikiristu na pia bado wanamtambua Ndikumana kama mkwe wao kwasababu ndoa
za kikiristu huwa hazivunjiki.
Hahaahaahaaa jaman tulia Uwoya jipange usikurupuke maaana majuto ni mjukuu
ReplyDelete