Star wa filamu Swahiliwood Kulwa Kikumba"Dude" amesema kuwa risala
iliyosomwa juzi katika sherehe za kuadhimisha miaka 3 ya kundi la Bongo
Movie Unity imepikwa kwani haikuegemea katika ukweli kuhusu waanzilishi
wa Kundi hilo. Akizungumza na Globalpublishers Dude ambaye ametamba na
filamu nyingi sokoni na pia igizo la Bongo Dar es salaam alisema "Ile
risala imepotosha, Bongo Muvi ilianzishwa na wasanii wa muziki na
filamu wakiwemo mimi, William Mtitu, H.Baba, Simon Mwakifwamba,
MwanaFA na Fid Q na wengineo kwa lengo maalum, nimeshangaa kusikia vile"
Maelezo ya Dude yanashabihiana na alichokisema Simon
Mwakifwamba ambaye ni msanii pia na Rais wa Shirikisho La Filamu
Tanzania kuhusu waanzilishi wa kundi hilo huku Mwakifwamba akisema kuwa
Bongo movie sio chama bali ni kampuni inayomilikiwa na watu tisa na pia
sio wanachama wa TAFF na kuongeza kuwa wengine katika kundi hilo
wanafuata tu mkumbo wa wasichokijua.
No comments:
Post a Comment