Mainda akilia
ENEO LA TUKIOTimbwili hilo la aina yake lilijiri kwenye Kanisa la Kiroho la Huduma ya Inuka Uangaze lililopo maeneo ya Sinza-Lion jijini Dar hivi karibuni baada ya waandishi wetu kutinga kanisani hapo kwa lengo la kuzungumza na mchungaji wake aliyetajwa kwa jina la Mwamposa.
Ishu kubwa ilikuwa ni kujua undani wa skendo iliyoenea mjini kuwa, Mainda anadaiwa kukwapua baadhi ya waume wa waumini wa kanisa hilo na kwamba yupo kwenye maandalizi kabambe ya kufunga ndoa na mchungaji.
ANAJIPENDEKEZA KWA WAUME ZA WATU?
Ilisemekana kwamba madai hayo yalirushwa na baadhi ya waumini ikidaiwa kuwa Mainda amekuwa na tabia ya kujipendekeza kwa baadhi ya waume za watu huku wengine wakidai anataka kuolewa na mchungaji.
MCHUNGAJI AFUNGUKA
Waandishi wetu walipozinyaka habari hizo ambazo zilizua gumzo kwa baadhi ya watu hasa kwenye mitandao ya kijamii, walifunga safari hadi kanisani hapo ili kuzungumza na mchungaji huyo baada ya Mainda kukataa kupokea simu ya mapaparazi ambapo alipopatikana mchungaji huyo alifunguka anachokijua juu ya skendo hiyo.
“Mainda ni binti kama mabinti wengine ninaowalea kiroho hapa kanisani na amekuwa akijituma sana.
“Mainda ni tofauti na waumini wasanii wengine labda ndiyo sababu ya watu kumchafua.
“Kuhusiana na ukaribu na waume za watu ni uongo, hao wanaoeneza habari hizo wana nia ya kumchafua kabisa kwa sababu wameona ametoka eneo lile na kumfuata Mungu,” alisema baba mchungaji huyo.
Mchungaji huyo aliendelea kufunguka kwamba, Mainda amekuwa akikutana naye na viongozi wengine siku ya Jumatatu kwenye kamati yao ya utendaji kazi, si kwa mengine na amekuwa mstari wa mbele kwenye kazi za kujitolea huduma za kanisani.
ANAJITUMA SANA KANISANI
“Unaweza kuamini kutokana na ufanisi wake wa kazi na kujituma, ndiye muumini ambaye tumempa nafasi ya kuwa mbele watu wanapotoa ushuhuda kwa sababu ana uwezo kwa sasa na amekuwa akifanya kila analoweza kuweka safi mazingira ya kanisa,” alisema mchunga kondoo huyo wa Mungu.
KUHUSU KUMUOA
Kuhusu suala la kumuoa Mainda, mchungaji alisema kwamba yeye hana wazo la kumuoa Mainda na wala staa huyo hajawahi kuingia kwenye gari lake.
“Ni binti mwenye heshima sana na kila kukicha anakuwa muumini mwenye uwezo wa kutoa huduma kwa waumini wenzake,” aligongea msumari.
MAINDA AOMBWA AFUNGUE MOYO
Baada ya mazungumzo hayo mchungaji alimuomba msaidizi wake kumwita Mainda ili aufungue moyo wake kwa kuzungumza na waandishi wa habari ambao walikwenda pale kwa lengo la kupata ufafanuzi.
Hata hivyo, Mainda alipotoka tu na kuwaona waandishi wetu alikataa kuzungumza na kuanza kuangua kilio cha kufa mtu.
Kufuatia tukio hilo, waumini waliokuwa wakiendelea na shughuli zao kanisani hapo walimshangaa Mainda huku wakimbeba msobemsobe kumpeleka pembeni na kumbembeleza.
“Maweee…Sitakiii…Nasema sitakii…nyiii…waandishi wameniharibia sifa yangu, sitaki kuongea nao jambo lolote,” alisikika Mainda wakati akiangua kilio.
Kwa muda mrefu sasa, Mainda amekuwa akitumia muda wake mwingi kanisani akisali na kufanya usafi hivyo kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.
source: Globalpublishers
No comments:
Post a Comment