Wednesday, 30 April 2014

NITAWACHUKULIA HATUA WASANII WASIOVAA NGUO ZA NDANI: STEVE NYERERE.

Steve Nyerere
Haya ni makubwa ! Mwenyekiti wa kundi la Bongo Movie Unity Steve Nyerere amesema kuwa atawachukulia hatua na kuwatenga baadhi ya wasanii wa kundi hilo wenye tabia ya kutovaa nguo za ndani na kupenda kukaa mikao ya kihasara wanapokuwa kwenye mizunguko yao na shughuli za kijamii na kupelekea kupigwa picha na kusambaa kwenye media na mitandaoni kwa madi wanaichafua tasnia.

 "tumechoka kunyooshewa vidole na watanzania, ni kweli kuna baadhi ya wasanii wana tabia ya kutovaa nguo za ndani na kukaa mikao ya ajabu na wakati mwingine hupigwa picha na kuwekwa mitandaoni, hiyo huwa inaidhalilisha fani hii na sasa tutakuwa wakali kupita maelezo" alisema Steve Nyerere ambaye mwenyewe anatafunwa na skendo ya kudaiwa kuwa mstari wa mbele kuwakuwadia baadhi ya wasanii wa kike kwa vigogo wa serikali na wafanyabiashara wakubwa.

No comments:

Post a Comment