Monday, 7 April 2014

KAJALA AFUNGUKA KWA UCHUNGU KUHUSU BEEF LAKE NA WEMA NA KUTUKANWA NA TEAM WEMA.

Kajala Masanja ambaye ni star wa filamu Swahiliwood amefunguka kuwa hana tatizo na Wema ila anashangzwa sana kutukanwa matusi ya nguoni na "Team Wema" katika mitandao ya kijamii hasa Instagram kiasi cha mwanae aitwaye Paula kuona matusi hayo na kujisikia fedheha. Inadaiwa kuwa Kajala na Wema kwasasa hawapo katika urafiki mzuri kama zamani na zile millioni 13 alizowahi kulipiwa kama faini na Wema ili asifungwe gerezani zimekuwa kama wimbo wa taifa kwa team Wema kwenda kwa Kajala wakimtaka azirudishe.


Kajala akitoa maelezo kwa uchungu kudhihirisha urafiki wao wa sasa na Wema sio kama ule wa zamani

Vile vile inadaiwa kuwa wiki ilopita Wema na Kajala walikutana katika ukumbi wa Maisha Club uliopo Masaki na kushindana kumtunza Snura aliyekuwa na show lakini team Wema walipomuona Kajala wakaanza kutaka kuanzisha vurugu huku team Kajala nao wakijibu mapigo na kumlinda Kajala aliyetaka kuondoka eneo hilo kuepusha shari.

Kajala alipoulizwa na Globalpublishers kuhusu tukio hilo alikana kulishuhudia ila alikiri kutokuwa katika uhusiano mzuri na Wema kwa kusema "Mimi kwa upande wangu sina tatizo na Wema lakini natukanwa sana bila sababu. Sijui nimemfanyia nini kibaya, narudia tena sina tatizo na Wema halafu siyo yeye anayenitukana au kunisakama, ni kundi linalojiita TeamWema, sina uhakika kama yeye ndiye anawatuma, kuhusu milioni 13, sasa nitazirudishaje wakati hakunikopesha, alinilipia bure? Hata sijui kama nikizirudisha nitakuwa sahihi? Sielewi lakini kama ni matusi, kweli natukanwa sana hadi mwanangu anaona ninavyoitwa malaya" alikaririwa Kajala akisema kwa uchungu mkubwa.

No comments:

Post a Comment