Leo ni siku ya kumuenzi aliyekuwa muigizaji maarufu wa filamu nchini
hayati Steven Kanumba ikiwa ni miaka 2 tangu afariki dunia. Leo kuna
bonanza la muziki la kumenzi Kanumba huku watu wakiingia kwa kiingilio
kitu ambacho baadhi ya wasanii wenyewe wamesema sio sahihi hata kidogo
bali watu wachache wanataka kumuenzi Kanumba kwa kujiingizia pesa.
Baadhi ya wasanii waliondika kulalamikia hilo ni wasanii wa siku nyingi
nchini Michael Sangu "Mike" na Swebe.
"NIJUAVYO MIMI KANUMBA ALIKUWA MWANAKWAYA WA KANISANI AKUWAI KUWA
MWANAMUZIKI WA JAHAZI WALA WA TWANGA PEPETA IWEJE TUMUENZI KWA HAYO?
JAMANI PESA ZINATAFUTWA KWELI ILA KWA NJIA HIYO YA KANUMBA SIO VIZURI
WATANZANIA WENGI WANASIKITIKA SANA JAMANI ? HII NI AIBU KUBWA SANA KWA
FAMILIA NA KANISA ALILOKUWA AKIABUDU KANUMBA" ameandika Mike
Nae Swebe ameandika "R.I.P RAFIKI YANGU MPENDWA.. MIAKA 2 SASA..
HAUKO TENA NASI NA HAITOTOKEA... UMEKUA MTAJI KWA WALIO HAI... BADALA YA
KUOMBEWA DUWA WATU WANASHEREHEKA KWA MABENDI KUYAALIKA HUKU VIINGILIO
VIKITAWALA... AMA KWA HAKIKA UKISTAAJABU YA MUSA UTAYAONA
YA FIRAUNI.... HUKO ULIKO SALAMU ZANGU NAZITUMA... KWA SASA FILAMU
ZINAUZWA KWA MAJINA NA SURA NA SI UWEZO... YOTE KWA YOTE SOKO LA FILAMU
LIMEKUFA BONGO.... ZANGU DUA ZITAKUFIKIA NA MUNGU MWENYE SIFA YA
KUSAMEHE AKUSAMEHE.. NA WANAOFANYA DHIHAKA JUU YA HILI NAO AWASAMEHE....
HAKIKA.. KWA MUNGU SOTE TUTAREJEA.... NINA MENGI.. LAKINI KWA HAYA
MACHACHE WACHA TUU NIJIFUTE CHOZI NA DUA KUKUOMBEA.... R.I.P RAFIKI
YANGU MPENDWA STEVEN CHARLES KANUMBA"
Swebe ambaye aliigiza tamthilia na filamu kadhaa na Kanumba aliongeza kwa kuandika " R.I.P.... STEVEN CHARLEZ KANUMBA... ILA
NATAMKA KWA HERUFI KUU.. NDG, JAMAA, NA MARAFIKI WAMEKUSALITI... KWA
SABABU YA PESA... WACHACHE TUTAKUOMBEA UPUMZIKE KWA AMANI... KWA SABABU
TUKO MAPITONI TUNAPITA... WENGI LEO WANATOA PESA ZAO KWENDA
KUCHEZA MUZIKI ULIOANDALIWA KWA AJILI YA KUMBUKUMBU YAKO BADALA YA
KUKUOMBEA MAPUMZIKO YA MILELE... HAKIKA WATAFANYA YAMCHUKIZAYO MUUMBA..
WATAKUNYWA, WATAPIGANA, NA HATA KUFANYA YASIYOSTAHILI ILIMRADI TUWAONE
KWENYE MAGAZETI YAO NA KASHFA WALIZOZIZOEA... MUNGU ATAWALIPA KWA
WAYAFANYAYO.... NAMUOMBA MUNGU AKUWEKE MAHALA PA AMANI NA KUKUPA
MAPUMZIKO MEMA.. AAMEN.. ........KAMA UNAUNGANA NAMI..LIKE.. AU COMMENT
..AMEN.. PUMZIKA KWA AMANI STEVEN CHARLES KANUMBA."
No comments:
Post a Comment