Kampuni iliyokuwa inakuja kwa kasi katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Timamu
Effects ambayo inamilikiwa na Jackson Kabirigi na Timoth Conrad au
maarufu kwa jina la Tico inasemekana kuwa imesambaratika kutokana na
kile kilichoitwa kuwa ni hujuma kwa mmojawapo wa wamiliki hao.
.
Akizungumza
na mtandao wa filamucentral kwa masharti ya kutotajwa jina lake, msanii mmoja ambaye
pia alishiriki katika kuigiza filamu hiyo alifunguka kuwa chanzo cha
kusambaratika kwa kampuni hiyo ni kitendo cha Tico ambaye alikuwa
mpigapicha na mhariri wa filamu hiyo kuandika kuwa filamu hiyo
imeongozwa na Issa Musa au Cloud 112 ambaye ni prodyuza wa muvi hiyo
badala ya Jackson Kabirigi ambaye ndiye aliongoza filamu hiyo.
Inasemekana kuwa baada ya kuona kosa hilo Jackson Kabirigi ambaye
anang’ara na filamu ya Kisate alimkabili Tico kumuuliza kulikoni lakini
badala ya Tico kufanya marekebisho alisema kuwa yeye anafuata
alichoambiwa na Cloud 112 jambo ambalo ni kinyume na kanuni za filamu
duniani kote kwa mtu kumpa sifa asiyestahili.
Baada ya majibizano makali kati ya wamiliki hao inasemekana kuwa kila mmoja aliamua kushika yake wakiiacha kampuni iko hewani.
Mtoa taarifa wetu aliyejibainisha kuwa anamkubali sana Kabirigi alienda
mbali zaidi kwa kudai kuwa huo ulikuwa ni mpango ambao tayari
ulishawekwa toka awali katika kumhujumu Kabirigi baada ya kuonekana
kung’ara katika upande wa uongozaji wa filamu hasa baada ya filamu
aliyoiongoza ya Mdundiko kushinda tuzo kadhaa za kimataifa.
FC ilijitahidi kuwapata Jackson Kabirigi na Timoth Conrad bila
mafanikio ila ilifanikiwa kuwasiliana na wasanii Wastara na Hidaya
Njaidi ili kujua ukweli kuwa ni nani aliyeongoza filamu hiyo kati ya
Jackson Kabirigi aliyeandikwa kama ‘2nd Director’ na Issa Mussa Cloud
112 aliyeandikwa kama ‘Director’ ambapo walifunguka kama ifuatavyo,
Wastara alisema ‘’Sinema iliongozwa na Jackson Kabirigi sijui wenyewe walivyoamua, ‘’
Pia aliulizwa mwigizaji mwingine ambaye ni Hidaya Njaidi naye alifunguka hivi
“Director ninayemjua ni Jack ambaye aliongoza filamu hiyo, kwani
Cloud alikuwa na scene nyingi za kuigiza hata kuna wakati ambao Jack
alikuwa anamwelekeza akimwambia siyo hivyo fanya hivi na Cloud kutii
kama jina la muongozaji kaandikwa yeye itakuwa ajabu labda
walisaidiana,”anasema Hidaya Njaidi
Bado wahusika wakuu wa habari hii, Jackson Kabirigi na
Timoth Conrad wanatafutwa Ili kuweka sawa jambo hilo sambamba na mtayarishaji mkuu
wa filamu hiyo maana siku hizi suala la Credit katika sinema linatumika
vibaya.
source: filamucentral
No comments:
Post a Comment