Star wa filamu nchini Nice Mohamed 'Mtunisy' anadaiwa kuachana na mke
wake hivi karibuni. Chanzo kimoja kiliuambia mtandao huu kuwa Mtunisy
siku hizi yupo mwenyewe wameshaachana na mkewe sababu zikidaiwa ni
scenes za kimapenzi anazocheza Mtunisy na waigizaji wa kike ikiwemo
filamu ya Who's Bad kwa madai kuna scenes katika filamu hiyo mkewe
hakuzifurahia na kumnyima usingizi. "Mtunisy yupo single wameachana na
mkewe hivi karibuni, unajua Mtunisy kuigiza scenes za kimapenzi na
wasichana wazuri kumekuwa kukimnyima raha mkewe, kuna filamu ya Who's
Bad ndiyo imefanya mke wake uvumilivu kumshinda" kilisema chanzo hicho
juzi.
Mtunisy alipotafutwa na swahiliworldplanet kuulizwa kama ni kweli ameachana na mke wake
alikana madai hayo na kusema mtoa habari hizo atakuwa mwehu "Sio
kweli huyo aliyesema hivyo atakuwa mwehu kidogo" alisema Mtunisy
anayetamba katika tasnia ya filamu nchini ambapo baadhi ya watu
humfananisha na Ramsey Nouah wa Nollywood kimuonekano na hata kiugizaji
hasa katika scenes za kimapenzi.
Mtunisy
No comments:
Post a Comment