Thursday, 6 February 2014

SIASA ZIMENIMALIZA KISANII: MARLAW


"Nilikuwa juu sana nilifanikiwa kuuza nakala nyingi sana za albamu yangu ya kwanza "Bembeleza", lakini naamini kitu kilichonishusha kwenye ramani ya muziki ni siasa" alisema

"kwa maono yangu naona pale ndiyo nilikosea kwani mashabiki wa muziki ni wanachama wa pande zote na wengi si waelewa, msanii kushiriki siasa ni haki yake kwani anatafuta pesa lakini mpinzani anakuchukia. Unajua hakuna kitu kibaya kama masuala ya kidini, kikabila, kisiasa hata ukereketwa kwenye masuala ya mpira unaweza kugombana na mtu kwasababu ya haya mambo" aliongeza

"Mambo ya siasa bwana acha kabisa, lakini mimi ni msanii ninaweza kuburudisha watu wa aina yoyote hata kama ni wa chama kingine, kikubwa watu wanatakiwa kutambua kwamba msanii anatafuta pesa hata akiitwa kwenye sehemu nyingine yenye upinzani mkubwa kwa kiasi gani, atakwenda kwakuwa anatafuta pesa na kesho huenda ukamkuta upande mwingine haimaanishi kwamba amehama"

"Kikubwa ni ikiwa msanii amechukua kadi kutoka chama husika na kujitangaza kwamba yeye ni mkereketwa wa chama hicho, hata hivyo kwa upande wangu naoni ni haki ya msanii kujiamulia kwamba anataka awe mfuasi wa chama gani, haigombi na wala haina masharti eti ili uwe msanii lazima ujiondoe kushiriki siasa, sio kweli"

"sifikirii kabisa kama ninaweza kushiriki tena kwenye uchaguzi, kilichopo sasa ninajiuza mimi na kazi yangu. Hivi sasa nimeshaandaa albamu yangu mwenyewe yenye nyimbo nyingi tu" alisisitiza

Marlaw aliwahi kutamba na nyimbo nyingi zikiwemo Bembeleza, Rita, Missing My Baby(Pii Pii), Sorry Sana, Kirungu, Nifundishe na Busu La Pink.

Marlaw katika kampeni za CCM kwenye uchaguzi mkuu 2010

No comments:

Post a Comment