|
Nisha akiwa kwenye interview ya Tv |
Filamu ya "Gumzo" kutoka Nisha's Film Production inatarajiwa kutoka
tarehe 27 mwezi huu wa February. Kama zilivyo filamu nyingi kutoka kwa
Salma Jabu Nisha tayari filamu ya GUMZO imeshakuwa gumzo kweli kwenye
social media na TVs huku ikiwa bado kutoka kutokana na watengenezaji
kuifanyia promo ya kutosha kama ilivyo Hollywood na Bollywood kufanyia
filamu promo ya kutosha kabla haijatoka ili watu wajue kuwa kuna kazi
mpya inakuja. Kwa mujibu wa Nisha ni kuwa katika Gumzo wamekuja tofauti
na kazi zilizotangulia. Filamu hiyo ukiachilia mbali Nisha mastaa
wengine waliocheza ni King Majuto, Wastara Juma, Hemedy Suleiman na
Tausi ambaye amecheza kama mke wa Hemedy.
Vituo mbalimbali vya Tv kwasasa vinamhoji Nisha
kuhusiana na filamu hiyo vikwemo TBC na Channel Ten. Interview ya Nisha
na Channel Ten kupitia kipindi cha Action and Cut itaonyeshwa kesho
Jumatatu saa tatu usiku. Zinazoonekana ni baadhi ya picha wakati Nisha
akifanyiwa interview. Vile vile habari nyingine ni kuwa nchi mbalimbali
tayari zinaisumbia kwa hamu filamu hiyo kutoka kwa Nisha.
Nisha na Tausi aliyecheza kama mke wa Hemedy katika filamu ya Gumzo.
Team GUMZOOOOOO
No comments:
Post a Comment