Dr.Cheni na mama yake Lulu |
Kesi
ya kuua bila kukusudia inayomkabiri muigizaji wa kike, Elizabeth
Michael maarufu kama Lulu imesikilizwa leo (February 17) katika mahakama
kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
Lulu
alikiri mbele ya Jaji Rose Temba kuwa alikuwa na uhusiano wa mapenzi na
marehemu Steven Kanumba na kwamba walikuwa na ugomvi, lakini alikana
mashitaka ya kumuua bila kukusudia.
Mbali
na kukiri kuwa na uhusianano wa mapenzi, muigizaji huyo pia alikiri
kuwa baada ya tukio hilo alitoka nje ya chumba walichokuwepo na kwenda
kumwambia mdogo wake marehemu Kanumba, Setti Bosco kuwa Kanumba
ametangulia mbele ya haki.
Akisoma
hati ya mashitaka, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Monica Mbogo, alidai
kuwa Aprili 7, mwaka 2012, Sinza Vatikani, Mkoa wa Dar es salaam,
mshitakiwa alimuua bila kukusudia Stevin Kanumba.
Wakili
Kombo, alidai kuwa pamoja na mambo mengine, marehemu Kanumba baada ya
kufa, mwili wake ilipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo majibu
yanaonyesha kwamba kifo chake kimesababishwa na uvimbe ndani ya ubongo.
Upande
wa serikali una mashahidi watano pamoja na vielelezo wakati upande wa
utetezi pia unatarajia kuwa na mashahidi watano na vielelezo.
No comments:
Post a Comment