Thursday, 24 July 2014

Naitumia Vizuri Fursa Kuwekeza Katika Ardhi Na Ujenzi Na Sio Kushindana Kuvaa Na Kwenda Club: Nisha

Star mkubwa wa filamu Tanzania Salma Jabu Nisha amesema kuwa anaitumia vizuri fursa anayoipata sasa katika kazi zake za sanaa kwa kuwekeza kwa ajili ya maisha yake ya baadae hususani katika ardhi na ujenzi na sio kushindana kuvaa, kwenda club na starehe nyinginezo zisizo na maana kama baadhi ya wasanii wengine halafu baadaye wanaishia kulalamikia maisha wakati wao wanaigiza maisha kwa kuendekeza starehe.

Nisha amesema kuwa katika sanaa ya filamu hawezi kuwa juu siku zote kuna wengine watakuja na kufanya vizuri zaidin yaken kama waliokuwepo mwanzoni ambao kwasasa baadhi wamechuja hivyo yeye anaitumia vizuri fursa aliyonayo sasa.

No comments:

Post a Comment