Uhusiano wa kimapenzi baina ya msanii wa filamu nchini
Elizabeth Michael ‘Lulu’ anayedaiwa kumuua bila kukusudia msanii
mwenzake, Marehemu Steven Kanumba, utaanza kukumbushwa tena hivi
karibuni pale Lulu atakaporudishwa katika Mahakakama Kuu Tanzania Kanda
ya Dar es Salaam Februari 17 mwaka huu. Lakini kabla kesi haijaanza
kusikilizwa kuna mambo ya muhimu inabidi uyajue ;-
-Lulu alizaliwa mwaka 1994 elimu ya Kidato cha Nne alihitimu katika
Shule ya Sekondari ya Midway, baada ya hapo aliendelea na shughuli za
sanaa ambazo alizianza tangu mwaka 2000. Lulu alifahamiana na Kanumba
kwa muda wa miaka 10 wakifanya kazi za sanaa na Januari mwaka 2012
ndipo walipoanza rasmi uhusiano ya kimapenzi.
-katika uhusiano huo hawakuwahi kuishi pamoja isipokuwa alikuwa
akienda kwa Kanumba anapojisikia na mara kadhaa aliwahi kulala huko.
- kipindi cha miezi minne ya uhusiano wao, walikuwa wakigombana mara
chache lakini sababu kubwa ilikuwa ni wivu wa mapenzi kwa sababu wote
walikuwa hawaaminiani.
-Siku ya tukio ilikuaje ? jioni ya siku hiyo Lulu alimpigia simu
Kanumba na baada ya muda mfupi alikwenda nyumbani kwake Sinza
Vatican.alipofika kwa Kanumba, alimkuta akiwa chumbani kwake akinywa
pombe ambayo ilikuwa imechanganywa na soda na ghafla simu yake iliita na
alipotoka nje kutaka kwenda kuisikiliza Kanumba alimfukuza hadi
barabarani. baada ya kumpiga kwa ubapa ghafla alitupa panga chini huku
akiwa amesimama alianza kupumua kwa taabu na baada ya muda mfupi
aliyumba na kujigonga ukutani na kuanguka chini.baada ya kuanguka, Lulu
alikimbia na kwenda kujifungia chooni kwa hofu na baada ya muda alitoka
na maji na kwenda kummwagia Kanumba lakini hakuamka.Alidai kuwa baada ya
kuona hali hiyo alishikwa na hofu na kuamua kukimbia kwenye ufukwe wa
Coco Beach. Alidai kuwa akiwa huko alipewa taarifa kuwa Kanumba
amefariki na ndipo alipompigia simu rafiki yake ili aende kumsaidia
kuendesha gari waelekee kwenye msiba (Haya ni maelezo yaliyotolewa mahakama ya kisutu )
-Uchunguzi wa awali wa polisi ulionyesha kuwa hakukuwa na jeraha lolote kuanzia kichwani hadi mwilini kwa Kanumba.
uchunguzi wa kifo hicho ulifanywa na jopo la madaktari watatu na
daktari mmoja wa familia kutoka hospitali ya Amana ambapo ulibaini kuwa
ubongo wa Kanumba ulikuwa umevimba na damu imevilia
-Januari 29 mwaka 2013 Lulu aliachiwa kwa dhamana baada ya kesi hiyo
kubadilishwa hati ya mashitaka kutoka kwenye kesi ya mauaji kwenda
mauaji ya bila kukusudia ambapo badiliko hilo lilimpa nafasi ya kupata
dhamana.
-Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Aprili 7 mwaka 2012 Sinza
Vatican jijini Dar es Salaam, Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia. Lulu
atarudishwa katika Mahakakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar es
Salaam Februari 17 mwaka huu. Tumuombee aweze kushinda kesi hii.
credit: vibe
No comments:
Post a Comment