Wednesday, 12 February 2014

MUIGIZAJI WA FILAMU TITO ZIMBWE ANUSURIKA KATIKA AJALI.

Tito
Muigizaji wa siku nyingi nchini Tito Zimbwe ambaye alianza kujipatia umaarufu tangu mwanzoni mwa miaka ya 2000 akiwa na kundi la Kaole amepata ajali ya pikipiki Ijumaa iliyopita njia ya Kigogo jijini Dar es salaam, Muigizaji huyo alikuwa amelazwa katika hospitali ya Dr.Mvungi iliyopo Kinondoni na leo ndiyo ameruhusiwa kurudi nyumbani. Akizungumza na mtandao huu Tito ambaye hufanya kweli kwenye filamu alisema .....

"Nimepata ajali ya Pikipiki Ijumaa usiku njia ya kigogo shule ya Rutihinda, nilipita kama siku mbili tatu hakukuwa na matuta sasa nilipopita nilijua hakuna matuta halafu usiku hakukuwa na alama yoyote ndio nikakutana na matuta nikapiga mzinga ni ajali tu mana siku zote nakua na gari na siku hiyo nilikua na gari lakini alitangulia nalo wife home so nikaazima pikipiki ya mshikaji nikapata nayo ajali"
 
Tito akiwa hospitalini

Tito alimalizia kwa kusema " Nashukuru ndugu jamaa na marafiki pamoja na wasanii walikuwa karibu yangu sana katika kipindi hiki cha matatizo sijavunjika ni mishtuko tu na majeraha mwilini"


Tito akiwa na Benny Blanco mmoja wa wasanii wenzake aliyeenda kumjulia hali
 Monalisa, Wastara na Amanda pia walienda kumjulia hali msanii mwenzao
Rais wa TAFF Simon Mwakifwamba pia alikuwepo kumjuliz hali Tito

Get well soon Tito

No comments:

Post a Comment