Friday, 21 February 2014

OMARY CLAYTON NA MWENZAKE WAMALIZA MGOGORO WAO KUHUSU FILAMU YA MDUNDIKO.

Mgogoro wa chini chini uliokuwepo kati ya Omary Clayton na Timothy Conrod kuhusu uandishi wa story ya filamu ya Mdundiko umeisha baada ya wawili hao kukaa chini na kuyamaliza. Akizungumza na swahiliworldplanet Clayton ambaye tayari ameshaandika filamu nyingi alisema "movie ya Mdundiko ambayo ilichukuwa tuzo nchini marekani jana ndiyo imezinduliwa rasmi. mimi ndio mtunzi wa story ile huku screenplay ikifanywa na Timothy Conrad.. huku kulikuwa na mgogoro wa credit nani mtunzi wa story but nashukuru now limeisha na kukubali kuwa mimi ndio mtunzi yeye akiwa ni screenplay"



Filamu hiyo imeongozwa na Jackson Kabirigi na excutive producer akiwa ni MFDI Tanzania. Mastaa humo ndani ni pamoja na Dokii, Tino, Lumolwe Motovolwa na wengineo.


Timothy Conrod

No comments:

Post a Comment