Saturday, 1 February 2014

NIVA ATOKA NDUKI NA BOXER HOTELINI KISA KIKIDAIWA NI KUGOMBANA NA DEMU MPENZI WAKE

Niva
Mwigizaji wa filamu Swahiliwood Zuberi Mohamed‘Niva’ juzi kati alijikuta akipata fedheha baada ya kupigana na mtu anayesemekana kuwa ni mpenzi wake, sakata hilo la aibu lilitokea katika Hotel ya Ndeka iliyopo maeneo ya Magomeni mida ya saa tano usiku.
Shuhuda wa tukio hilo akizungumza na filamucentral alisema kuwa Niva alikuwa kapanga katika Hoteli hiyo na baadaye alikuja na binti huyo na kuagiza chakula na kupelekewa chumbani huko ambako ugomvi ulitokea na kusababisha vurugu zilizomfanya Niva kutoka nduki.

Kufuatia ugomvi huo uliotokea ghorofa ya tano chumba namba 5, msanii huyo alitoka nduki akiwa na nguo ya ndani tu na kukimbia hadi chini na kutoweka jambo lililofanya wahudumu kuingia katika chumba hicho na kushuhudia uharibifu uliofanywa na wapenzi hao, huku kuta za chumba hicho zikiwa zimetapakaa uchafu wa vyakula.
Msanii huyo katika tukio hilo alipoteza vito vya thamani kama vile saa, mkufu, simu na vitu vinginevyo, Hata hivyo Niva alipotafutwa na mtandao huo ili kutolea ufafanuzi issue hilo la aibu hakuweza kupatikana kupitia simu yake ya mkononi.

No comments:

Post a Comment