Saturday, 6 September 2014

Nisha Atoa Misaada Ya Magodoro, Vyandarua Na Mashuka Kwa Yatima.

Muigizaji maarufu wa filamu nchini Salma Jabu Nisha ametoa misaada ya magodoro, mashuka na vyandarua katika kituo cha watoto yatima kilichopo maeneo ya Kigamboni ,
Dar es salaam. 
Wiki iliyopita Nisha alisherehekea birthday yake na watoto wa kituo hicho na walezi wa kituo hicho kumwambia Nisha kuwa mojawapo ya changamoto walizonazo ni ukosefu wa magodoro, mashuka na vyandarua ndipo juzi tena Nisha akarudi kituoni hapo na kutoa misaada hiyo. Nisha alipoulizwa  alisema kuwa yeye hupenda kusaidia wenye uhitaji pale alipo na uwezo kuliko kuendekeza starehe zisizo na maana wakati k,una watu wanalala njaa na hawana sehemu nzuri ya kulala,.

Nisha amesema kuwa ni utaratibu wake kutoa misaada kwa yatima hususani kila mwisho wa mwezi ili kupata baraka zaidi kutoka kwa Mungu kwasabu kutoa ni moyo si utajiri.


No comments:

Post a Comment