Baby Madaha ambaye ni star wa filamu Swahiliwood na pia mwanamuziki wa
Bongofleva amesema kuwa mpenzi wake wa sasa Joe Kariuki kutoka nchini
Kenya ambaye pia ni meneja wake na pedeshee wa label ya Candy n Candy
anamkoleza sana kimapenzi na hawezi kumuacha kamwe bali anatamani
ahamie nchini Kenya kabisa.
Akizungumza na Globalpublishers
Madaha anayetamba na wimbo wa Summer Holiday kwasasa alisema "Kusema
kweli huyu kaka kanikoleza jamani japo watu watachonga mengi
lakini abadani sitosikiliza maneno yao, kwa kuwa awali sikuwa na
uhusiano naye ila porojo za watu zilipelekea kuchukua maamuzi hayo
natamani niamie Kenya ili tuwe karibu wakati wote".
Baby Madaha
No comments:
Post a Comment