Jackie Cliff |
Hata hivyo baadhi ya mitandao leo iliweka habari za mwanamke mmoja wa kitanzania kukamatwa na dawa za kulevya huko china lakini bado habari hizo hazikubainisha mwanamke huyo ni nani na usiku huu ndiyo ikasemekana ni Jackie Cliff. Habari hiyo inasomeka ..........
"Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.
Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.
Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013."
Tunaendelea kuzifuatilia habari hizi tutakuletea updates zaidi...........
Tamaa ya pesa inawaponza wadada wenfi wa kibongo! Fanya kazi kwa bidii na Mwenyezi Mungu atazibariki kazi za mikono yako na utabarikiwa kwa kila kitu unaxhokitaka hapa duniani na hii Ni pamoja na kuishi maisha ya amanis na furaha! Ila Tamaa ya Pesa za haraka mwisho wake Ni mbaya sana!
ReplyDeletesikio la kufa halisikii dawa! wasanii mnatutia aibu mpaka inafikia mahali wabongo wote tunafananishwa na madawa ya kulevya! kwa sheria za china inaweza ikawa ndo mwisho wako lakini mungu yupo maombi yako na yetu ndo yatakuokoa!
ReplyDelete