Mr. Nice kutoka Tanzania ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya
aliyewahi kujipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi akiwa na style
yake ya Takeu kupitia nyimbo kama Kidali Po na Kikulacho amepata nafasi
ya kucheza filamu huko Denmark kupitia wasanii wa VAD productions wenye
asili ya kiafrika hasa kutoka nchini Congo ambao hufanya kazi na wasanii
wa nchi za Afrika hususani Afrika mashariki.
Mr. Nice amepata nafasi hiyo huku akiwa hajawahi hata siku moja kucheza
filamu nchini Tanzania na dalili za kucheza filamu Swahiliwood zikiwa
bado hakuna. Wasanii wa VAD kwa ujumla wamefurahi kuwa na MR. Nice
nchini humo.
Angalia picha za uchukuaji wa filamu hiyo na nyingine ambazo sio za uchukuaji wa filamu hiyo.....
credit:
Swahiliworldplanet
No comments:
Post a Comment