Tuesday, 24 December 2013

KAJALA AKANA MADAI YA KUTEMBEA NA MUME WA SHAMIM MWASHA.

Shamim na Kajala
Jana gazeti la SANI lilikuwa na habari ukurasa wa mbele ikidai star wa Swahiliwood Kajala Masanja anatembea na mume wa Shamim Mwasha ambaye ni blogger maarufu wa 8020fashions. Baada ya habari hiyo kutoka leo Kajala amejibu mapigo ya habri hiyo akionekana kuchukizwa na habri hiyo. Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Kajala ameandika "nadhani namjua huyu dada siku nyingi sana hata kabla ya wengine wenu kumjua, tunaheshimiana sana na hatujawahi kukoseana sasa sijui nanai aliyeanzisha habari ya mimi kutembea na mume wake na sijui alifanya hivyo kwa makusudi gani, naumia kila siku kwa ajili ya ujinga wa watu na hayo magazeti nikiwaambia nipeni ushahidi wa kuwa natembea na mume wa Shamim sijui kama mtafanya daah sijui niseme nini @ 8020fashions mpenzi enjoy ndoa yako achana na wapumbavu, nimevumilia nimeona bora leo niandike unajua sipendagi kuongea lakini gazeti la jana limenikwaza sana"





credit: swahiliworldplanet

Gazeti lenyewe liliandika hivi

No comments:

Post a Comment