Tuesday, 11 November 2014

Nisha Kutwaa Tuzo ya Oscar 2015 !

kwa tetesi zilizotufikia hivi punde,filamu ya mwanadada,mwanaharakati anayejituma sana na asiye na ma-scandal kwenye kiwanda cha filamu Tanzania superstar  SALMA JABU NISHA ambayo tumekuwa tukiiona sana matangazo yake hivi karibuni katika filamu zinazotoka za Steps Entertainment iitwayo HAKUNA MATATA imetabiriwa kuchukua Tuzo za OSCAR na GOLDEN GLOBE AWARDS
,muda mfupi baada ya kutoka katika kikao na baadhi ya wawakilishi wake ambao wanatazama soko la nje sana kwa ajili ya kuitangaza sanaa ya Tanzania kufika mbali,msanii huyu mahiri na mpole ila mcheshi katika maisha ya kawaida ila machachari katika filamu zake (NISHA) asiye na majivuno na aliye makini sana katika kazi aliandika haya katika ukurasa wake wa facebook 

"ukiona kobe kainama basi anatunga sheria,ukimya huu mkubwa karibuni utapata suluhu,,,,, habari njema mashabiki zangu HAKUNA MATATA filamu yetu ambayo itatoka mwezi ujao tukijaaliwa imetabiriwa kuchukua tuzo za OSCAR na GOLDEN Globe Awards,,, kweli ni HAKUNA MATATA Dua zenu nawaomba katika hili,mengi zaidi ntawapa taarifa PICHA NDO LINAANZA STARING MWENYEWE CHAKARABOTI KAINGIA MTAMBONI"
King Majuto, NIsha naJB
TUNAKUOMBEA NDOTO ZAKO ZIZIDI KUTIMIA NA YALIYOTABIRIWA YAWE AMEN-

No comments:

Post a Comment