Sunday, 31 May 2015

WASANII WACHANGA WAONYESHA UWEZO WAO NDANI YA MTAA KWA MTAA

Kama ilivyokawaida ya Nisha's film production huwa haiwaachi wasanii wachanga basi humo kwenye MTAA KWA MTAA wamefanya yao. Katika kitu ambacho hakikutegemewa ni wasanii hao wachanga kuonyesha uwezo wao wahali ya juu mpaka mtu ushindwe kutambua kama kweli hawa ndio mara yao ya kwanza au ni wakongwe katika sanaa. Kama huja nunua Dvd ya MTAA KWA MTAA kanunue sasa ili uweze kujionea uwezo wa wasanii hao wachanga katika sanaa ya uigizaji. Nisha's film production lengo lake kubwa ni kuwainua wasanii wa changa hivyo huwapa nafasi za kucheza katika movie zinazotoka Nisha's film zam kwa zam. Kama na wewe ni msanii mchanga na unahitaji kushiriki katika movie za Nisha's film basi fanya ku follow page zetu za instagram ambazo ni @nishabebee @nishasfilmproduction @ochu_255 na kwa wale waliopo facebook unaweza ku join katika group letu ambalo ni Team nisha films production au unaweza kulike page yetu Nisha's film production pia kama upo whatsapp unaweza kuwasiliana na Production manager wa Nisha's film bwana Othman kwa no 0789 586057.











Thursday, 28 May 2015

MTAA KWA MTAA YAWA LULU

Habari kutoka Steps Entertainment Ltd asubuhi yaleo wamepokea oda nyingine kubwa ya movie mpya iliyo toka leo inayojulikana kama MTAA KWA MTAA. Tuliwasiliana na mmoja wa wafanya kazi wa hapo steps alisema wanajiandaa kutoa copy nyengine maana zilizopo hazitotosha kwani mpaka sasa washa pokea oda nyingi za hapa Dar es salaam ukiashilia mbali za mikoani. Steps walimpongeza msanii. Salma jabu nisha kwa kazi nzuri nakudai yeye ndio anaongoza kwa mauzo sokoni.

Wednesday, 27 May 2015

NISHA ASHANGAZA MAMILION YA WATU


Msanii wa filamu mwenye jina kubwa na heshima kwa jamii Salma Jabu Nisha ashangaza watu wengi baada ya filamu yake ya MTAA KWA MTAA inayotoka kesho siku ya alhamis tarehe 28/05/2015 kuisha steps na mwakala nchi nzima kugombaniana,hivyo kuwapa kuwapa kazi tena steps intertainment kutoa nakala nyingi zaidi za filamu hiyo ya MTAA KWA MTAA ambayo  imeoneshwa kupendwa na kukubaliwa  sana na mashabiki  kabla haijatoka, imeitwa maajabu kutokana kwamba filamu za star huyo asiyekuwa na scandals,mwenye sifa uchapakazi ‘’NISHA’’ kuvunja  record kazi zake kwa mauzo na kumfanya azidi kung’ara na kutoa filamu kali kupita zote kila atoapo,filamu hiyo kali ya MTAA KWA MTAA amewashirikisha  waigizaji mahiri kama Asha book,Hemedy Suleiman,Tausi Mdegela,Diana Kimary huku motto wake Nisha Iptysam Othman akionesha kung’ara zaidi naye,MTAA KWA MTAA imekuwa kiburudisho kikubwa haswa kwa kuonekana Nisha na Asha Boko kwenye mavazi ya Kitrafic huku kila mtu akitamani kujua ndani kuna nini na imekuwaje wakali hawa kuwa katika mavazi hayo. MTAA KWA MTAA itatoka kesho tarehe 28/05/2015 Mungu ibariki Mtaa kwa Mtaa ,ibariki Nisha’s film production,wabariki wasanii wanaojituma Tanzania.
Hongera Nisha MTAA KWA MTAA itazidi kufanya maajabu na kushangaza zaidi



Tuesday, 26 May 2015

MTAA KWA MTAA Toka Kwa Nisha, Hemedy, Asha Boko, Diana Kimaro Alhamisi Hii Kuingia Sokoni.

Filamu kali sana ya MTAA KWA MTAA toka kwa mastaa wa filamu nchini Salma Jabu Nisha, Hemedy, Diana Kimaro, Tausi mdegela, Asha Boko na Manaiki Sanga inatarajiwa kuingia rasmi sokoni alhamisi ya wikii. Filamu hiyo iliyoongozwa na Lamata Leah Mwendamseke tayari imeonekana kuwabamba watu wengi kupitia promo za picha mbali mbali. Utaikosaje sasa !. Hakikisha unanunua nakala yako halisi. Anaglia baaadhi ya picha toka filamu hiyo........

Sunday, 24 May 2015

TUKUTANE SOKONI-NISHA

Kwanza napenda kumshuru m/mungu kwa kila kitu pia napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mashabiki zangu kwa kuweza kunipigia kura yaliyo pita sindwele tugange yajayo. Ninachopenda kuwaambia mshabiki zangu zitovunjika moyo nitaendelea kuwapa burudani na mwisho wa mwezi huu filamu mpya kutoka Nisha's film inayojulikana kama MTAA KWA MTAA itaingia sokoni hivyo msikose kununua nakala original. Napia napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa baba yangu kipenzi King Majuto kwa kuweza kuchukua tuzo na wote kwa ujumla nawaambia nawapenda sana kikubwa tuongeze juhudi katika kazi na upendo naimani tutafika pale tunapopataka.        
                       MTAA KWA MTAA MWISHO WA MWEZI HUU KUWA MTAANI

Thursday, 21 May 2015

Nisha Awa Kimbilio La Wanyonge Na Wasanii Chipukizi.


Kwa takriban miaka 4 tangu aanze kufanya filamu zake mwenyewe,Star machachari wa filamu,anayejielewa,asiye na scandals na tishio kwa wasanii wote Tanzania (wakike kwa wanaume)mwenye uoga wa M'Mungu bi Salma Jabu Nisha,amekuwa kimbilio la wanyonge kwa kuwa number moja ya msanii asiye mbinafsi na kusaidia wasanii wachanga kwa kuwachezesha ktk movie zake na kusaidia wasiojiweza (yatima,wajane,walemavu n.k)Nisha amekuwa si mtu wa maneno sana zaidi ya vitendo,na kikubwa zaidi si mtu wa kujigamba ana nini na nn,ndio maana tunaamini M'Mungu anambariki kwa njia hizo.

Wednesday, 20 May 2015

SIKU ZIMEKWISHA-NISHA

 Siku zinazidi kusonga mbele na ile kitu tunayoisubiriria kwa hamu kubwa ndio inakaribia kutoka. MTAA KWA MTAA ndio movie inayo bamba kila kona ya nchi nimepata taarifa hadi nchi za jirani nazo wanasubiria kwa hamu kubwa. Ninacho waomba mashabiki zangu tununue nakala halisi ili mimi msanii wako niweze kuendelea kukupa burudani. Ili kuitambua DVD original kuna stika za TRA na STEPS zilizobandikwa katika DVD hizo mbazo stika hizo zinashikika na DVD fake stika zake hazishikiki yani zimepigwa copy zile kava original hiyo ninjia moja wapo yakujua DVD original na DVD fake.
                                                 NISHA BEBEE NA ASHA BOKO
                                   MTAA KWA MTAA MWISHO WA MWEZI HUU   
SALMA JABU NISHA NI MMOJA KATI YA WANOWANIA TUZO YA MCHEKESHAJI BORA KWA UPANDE WA WANAWAKE KATIKA TUZO ZA TANZANIA FILM AWARDS 2015 ILI KUMUWEZESHA KUSHINDA NENDA KWENYE UWANJA WA MSG ANDIKA TFA 150 KWENDA NO 15522 UNAWEZA KUPIGA KURA KADRI UWEZAVYO SIKU ZIMEBAKI CHACHE. PIGA KURA YAKO SASA

JISHINDIE ZAWADI NA MTAA KWA MTAA


Mwana dada Salma Jabu Nisha amwaga zawadi kwa mashabiki wake.
Salma Jabu Nisha amekuwa akitoa maswali kupitia account yake ya Instagram maswali yanayohusu movie yake mpya inayojulikana kama MTAA KWA MTAA. Kama we ni mshabiki wa Nisha na unataka kushriki kujibu maswali na kushinda nenda kwenye instagram mfollow @nishabebee au
kama unatumia facebook mu add Said Salma Jabu uweze kujibu maswali na kujishindia zawadi kibao

Tuesday, 19 May 2015

TANZANIA FILM AWARDS (TAFA) 2015 BADO WIKI MOJA

Natumaini wote ni wazima wa afya kwa wale wenye matatizo nawombea kwa M/mungu awaondoshe na awajalie afya njema napenda kuwaambia mashabiki zangu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa tumebakiwa na wiki moja  ya kupiga kura kwa msanii unayempenda. Ili kuniwezesha mimi kushinda tuzo ya mchekeshaji bora kwa upande wa wanawake nenda kwenye uwanja wa msg andika TFA 150 kwenda no 15522 na unaweza kupiga kura mara nyingi uwezavyo.  PIGA KURA SASAAA.
    MTAA KWA MTAA  COMING SOON

Sunday, 17 May 2015

NISHA KUJA NA ZAWADI YA 2015

Kwanza namshukuru M/mungu kwa kunijalia afya njema pili namshukuru mama yangu mzazi kwa kuweza kuwa namimi toka ananizaa mpaka leo hii bado yuko pamoja nami namwambia ahsante na nampenda sana vilevile napenda kushukuru uongozi mzima wa Nisha's film production na crew nzima ya Leah Richad Mwendamseke, watoto wangu wa Team nisha na wote wanaoniunga mkono nawaambia nawapenda sana. Na kuwadhibitishia hilo mwaka huu wa 2015 nimewaletea zawadi zawadi ambayo ipo tofauti na miaka yote. MTAA KWA MTAA nizawadi ambayo nimewaletea watanzania waweze kuburudika na kuelimika pia kwani ndani yake kuna mafunzo mengi ninacho waomba watanzania wasikose kununua nakala original ili kuokoa sanaa ya Tanzania.  MTAA KWA MTAA INATOKA MWISHO WA MWEZI HUU.
                                          MTAA KWA MTAA MWISHO WA MWEZI HUU 5

Thursday, 14 May 2015

Nisha's Film Yapania Kuibua Vipaji Vipya





Kampuni kubwa ya Nisha's film yadhamiria kuwasaidi wasanii wachanga. Katika kulitekeleza hilo Nisha's film imejiwekea mikakati mingi moja wapo ni kuwachukua wasanii hao na kuwapa nafasi ya kucheza katika kila movie inayotoka Nisha's film au kampuni yoyote itakoyotoa movie na kusimiwa na Nisha's film.  MWISHO WA MWEZI HUU NISHA'S FILM PRODUCTION INATOA MOVIE MPYA INAYOKWENDA KWA JINA LA MTAA KWA MTAA PATA NAKALA YAKO ORIGINAL KUOKOA SANAA YA TANZANIA


Tuesday, 12 May 2015

IPTYSAMA OTHMAN AMLIZA MAMA YAKE KWENYE MTAA KWA MTAA



Nyota njema huonekana asubuhi, namshukuru M'Mungu kwa hiki kipaji alichompa mwanangu Iptysam,aliweza kuonesha kwny Angel akiwa na miaka mi4.. tu ila haijatosha kwny zilizofata.. kikubwa zaiidi ktk MTAA KWA MTAA hadi nilijikuta machozi yananitoka,sasa humu ni TAUSI MDEGELA na IPTYSAM wanachuanaje 😂😂😂 utacheka pale Tausi anapoambiwa na Ipty akitaka aamkiwe na amuone mkubwa amshike kichwa wakiwa wamesimama wote 😅😅😅 nawapenda sanaa dah!!! #MTAAKWAMTAA coming soon!!!




                                             IPTYSAM  OTHMAN
                                 IPTYSAM  OTHMAN
                                      TAUSI MDEGELA NA IPTYSAM  OTHMAN




Monday, 11 May 2015

MTAA KWA MTAA NDIO HABARI YA MJINI

 Hellow Tanzania ule wakati wakusahau matatizo ndio umefika ni muda wa kufurahi na kujifunza sasa kupitia movie mzipendazo zinazotoka Nisha's film production hii inaitwa MTAA KWA MTAA utapata kujifunza na kuelimika kupitia movie hii inaweza kutazamwa na rika zote kwani imezingatia maadili. Mwisho wa mwezi huu mzigo utakuwa mitaani kote pata nakala yako original kuokoa sanaa ya bongo
MTAA KWA MTAA NDIO HABARI YAO!!!!!
 ASHA BOKO NA SALMA JABU NISHA
SALMA JABU NISHA

Saturday, 9 May 2015

Nisha Kutoa Filamu Mpya Muda Si Mrefu.

Star wa filamu nchini Salma Jabu Nisha anatarajia kutoa kazi yake mpya ya filamu muda si mrefu baada ya kutamba na hakuna matata na Zena Na Betina.

Nisha Aguswa Na Wahanga Wa Mafuriko Nchini.

Huu ndio ujumbe wa Nisha kuhusu wahanga wa mafuriko nchini........