Sunday, 17 May 2015

NISHA KUJA NA ZAWADI YA 2015

Kwanza namshukuru M/mungu kwa kunijalia afya njema pili namshukuru mama yangu mzazi kwa kuweza kuwa namimi toka ananizaa mpaka leo hii bado yuko pamoja nami namwambia ahsante na nampenda sana vilevile napenda kushukuru uongozi mzima wa Nisha's film production na crew nzima ya Leah Richad Mwendamseke, watoto wangu wa Team nisha na wote wanaoniunga mkono nawaambia nawapenda sana. Na kuwadhibitishia hilo mwaka huu wa 2015 nimewaletea zawadi zawadi ambayo ipo tofauti na miaka yote. MTAA KWA MTAA nizawadi ambayo nimewaletea watanzania waweze kuburudika na kuelimika pia kwani ndani yake kuna mafunzo mengi ninacho waomba watanzania wasikose kununua nakala original ili kuokoa sanaa ya Tanzania.  MTAA KWA MTAA INATOKA MWISHO WA MWEZI HUU.
                                          MTAA KWA MTAA MWISHO WA MWEZI HUU 5

No comments:

Post a Comment