Swahiliworldplanet
ilipata nafasi ya kuzungumza machache na star wa filamu nchini Salim
Ahmed "Gabo Zigamba" kuhusiana na kazi zake za filamu na maisha binafsi
hivi juzi kati. Gabo ambaye kipaji chake cha kuigiza hakijifichi huku
akiwa tayari amejizolea mashabiki wengi alitiririka kama ifuatavyo
katika interview hii ndogo.
SWP: Nani alikushawishi kuingia kwenye sanaa ya uigizaji?
GABO: Ni msukumo wa maisha baada ya plan A na mtazamo wa ndugu jamaa na marafiki
SWP: Umefaidika na nini mpaka sasa tangu uanze kuigiza filamu?
GABO: Kwa upande wa mafanikio bado naidai sanaa
SWP: Kitu gani huwa kinakukera zaidi unapokuwa location?
GABO: Kero kubwa ni mijadala ya pre-production ndani production....
SWP: Baadhi ya waigizaji nchini wapo
busy kutengeneza skendo ili kuandikwa kwenye media huku kazi zao zikiwa
chache na bado haziridhishi je unalizungumziaje hilo?
GABO: .Ni matumizi mabovu ya akili huwezi kuwa busy na skendo ikiwa huna kaz miliki.....
SWP: .Umeoa au una mchumba?
GABO: Nina mke na mtoto mmoja
SWP: Nini matarajio yako ndani ya miaka 3 ijayo kuanzia sasa?
GABO: Kufanya sanaa kimataifa
No comments:
Post a Comment