Filamu mpya ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa kwasasa ni JICHO LANGU
toka kampuni ya J-Film 4 Life inayomilikiwa na Odama Jennifer Kyaka.
Filamu hiyo inadaiwa ni moto wa kuotea mbali kiasi cha wamachinga
kuisubiri kwa hamu kubwa. Odama, Salim Ahmed(Gabo), Thadeo Alexander na
Grace Wapunda wameonyesha uwezo mkubwa humo ndani yenye funzo kubwa kwa
jamii. JICHO LANGU itaingia sokoni rasmi tarehe 31 mwezi huu wa tatu.
usikose kununua nakala yako halisi.
No comments:
Post a Comment