Monday, 24 March 2014

NISHA AJITOLEA KUMSAIDIA MTOTO MWATHIRIKA WA UKIMWI ASIYE NA MBELE WALA NYUMA.

Nisha akiwa na mtoto huyo huko Zanzibar
Star wa filamu nchini Salma Jabu Nisha ameonyesha moyo wa upendo na wa kuigwa katika jamii baada ya kuamua kumsaidia mtoto asiye na wazazi na muathirika wa virusi vya Ukimwi huko Zanzibar ambaye hutengwa na watoto wenzake.

 Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Nisha ameandika "Huyu mtoto ndio sababu hasa ilonifanya nikaja huku, yupo darasa la pili,ana miaka 9,baba yake alimkana akiwa tumboni kwa mama yake,mama yake alifariki pindi tu alipomzaa,mtoto huyu mdogo anaishi na virusi vya ukimwi,jamii inayomzuunguka imemtenga,wazazi hawataki watoto wao wacheze nae,shule mwanzo alikataliwa,kula yake Allah anajua,yupo mpweke,SISEMI HIVI KUMTANGAZA LA HASHA, ila ikumbukwe mimi ni msanii na ni kioo cha jamii, jamii inatakiwa ione na kujifunza, inauma sana, ila nipo hapa kwa ajili yake"

Mungu akubariki na kukuzidishia zaidi Nisha kwa kuamua kumsaidia mtoto huyo.

No comments:

Post a Comment