Wednesday, 5 March 2014

NISHA, KING MAJUTO, WASTARA NA HEMEDY WAIFANYA GUMZO KUUZA SANA SOKONI.

Filamu ya Gumzo iliyoingia sokoni hivi karibuni kutoa Nisha's Film Production inadaiwa kufanya vizuri sokoni katika nchi mbalimbali za Africa mashariki na kati. Vile vile kupitia mtandao mmoja wa kijamii Nisha amendika "Habari Tanzania na dunia kwa ujumla.. siku zote naamini asoshukuru si muungwana,mm naomba nichukue fursa hii niwashukuru sana kwa mapokezi ya filamu ya NISHA'S FILM PRODUCTION.. filamu ya ‪#‎GUMZO‬ kiukweli hadi sasa idadi ya mauzo yanayotokea siachi kusema ahsante Mungu.. na nyinyi mashabiki zangu,maana naamini ninyi ndio muliyoyafanya maajabu haya.. nawapenda sana.. na kwa wasionunua #GUMZO hujachelewa,ipo madukani pata nakala yako sasa... humu hamna watoto ila nawashukuru sana maana wao ndio wamevunja record"

Filamu ya Gumzo imewakutanisha mastaa wakubwa kama Nisha, King Majuto, Wastara na Hemedy. Hakikisha unapata nakala yako halisi kama bado hujaiona Gumzo.


No comments:

Post a Comment